Friday 30 January 2015

Re: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

Yona;
Safi sana na hiyo ndo demokrasia.....
Mada zake hazina kitu cha kuchangia au kubishana kwa hoja,wewe hujaona ilo.
Zaidi zinatufanya tuendelee kumshangaa kulingana na wasifu alionao/aliokwishawahi kuuleta hapa pindi anaanza kazi UB.
Unayaona kama mashambulizi lakini yapo katika njia ya kumsaidia asiendelee kuharibikiwa japo yeye hana habari, Yona meseji yako ipo vague,sijui unamponda au kweli unamhimiza kushika barabara iyoiyo.


Reuben
--------------------------------------------



On Fri, 1/30/15, Yona Fares Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:

Subject: Re: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: ipyana75@yahoo.com, ipyana75@yahoo.com
Date: Friday, January 30, 2015, 12:44 PM

Hongera
hapo kwa kutumia uhuru wako kujieleza na kueleza hisia zako
.
Usikubali mtu
akunyamazishe hata hata , hata babako akikosea unamwambia ,
unaandika , unatoa mawazo yako .
Kama tunataka kupiga hatua kwenye
maendeleo na mambo mengine mbalimbali lazima tukubali mawazo
ya wengi lazima tukubali maoni na chochote ambacho anaandika
mwingine .
Hongera
tena na tena hilo tatizo la herufi , lugha na mengine ni
mambo ya kawaida watu hujifunza kila siku .
Endelea kujifunza naamini siku moja
hawa wanakushambulia utawapiku na kuwaacha mbali kwa sababu
hawatoi mawazo yao tuwasikie na kuwasoma kazi yao ni
kushambulia watu binafsi badala ya hoja .
On Friday,
January 30, 2015 at 10:11:07 AM UTC+3, Reuben Mwandumbya
wrote:Mwambapa;Happy hajui kuna kesho,upeo wake unaishia
leo.Hapa jukwaani nina
imani kuna maelfu ya wanajukwaa na wana nafasi tofauti
katika kila fani hapa duniani.Wanapata kumjua hata bila ya kumuona,hivyo
hata siku ukikutana naye kama ni issue ya kutoa maamuzi juu
yake unakuwa huna kazi kubwa ya
kufanya. Reuben
 

      On Thursday, January
29, 2015 9:37 PM, Adam Mwambapa <adammwambapa@ymail.com>
wrote:
   
 

  Pengine ningempongeza
mwanangu Happness Katabazi, kutokana na jinsi alivyotumia
uhuru na haki yake ya Kikatiba kuongea. Hilo kwa kweli
amejitahidi sana kulifanikisha.Isipokuwa ningemwomba kama ataupata ujumbe wangu
huu, na kama alimsikia vizuri sana Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, Mhe. James Mbatia, ambaye alikuwa ni mtoa hoja
namna alivyohitimisha kwa umahiri mkubwa sana hoja
yake.
Hii ilionesha jinsi ambavyo Mbatia ni mweledi na
mjuvi wa mambo. Moja ya point ambazo Mbatia alizitoa kwa
wote wanaonekana kushabikia kupigwa kwa Prof. Ibrahimu
Lipumba, kama afanyavyo leo Happness kushangilia na kuona
ndivyo inavyopaswa iwe.
Alisema kuwa, inawapasa
wote hao ambao wanashangilia na kushabikia waelewe kuwa
wanashabikia na kushangilia kutokana na nafasi walizonazo
sasa. Ambazo zinawawekea kinga kwa namna fulani ya kutopatwa
na adha pamoja na kadhia ya namna hii. Lakini wakumbuke kuwa
pindi watakapoondoka na kuwa mbali na nyadhifa zao
walizonazo leo, na wao watakuwa ni raia wa kawaida ndipo
watakumbana na haya wanayokumbana nayo Watanzania walioko
huku.
Hivyo basi kwa pointi kama hii, nisingetegemea
Happness kushabikia matukio ya uvunjifu wa amani kama haya
kwa kuwa tu wanaofanya ni sehemu ya mahali alikokuwa na
ajira. Je, ni kwa kuwa ndugu zake, jirani zake na watu wake
wa karibu hawakukumbwa na kipigo hiki au ni sababu
gani?
Pointi nyingine ni ile ya Mhe. Nasari aliyosema
kuwa, askari wakumbuke kuwa wananchi ndiyo wanaoishi na wake
zao, watoto zao na ndugu zao huko uraiani wakati wao wapo
kazini. Sasa isingekuwa vema kuwatendea mabaya watu wengine
wakati familia na watu wengine kwenye makazi yako, wapo
kwenye uangalizi wa jamii hiyo hiyo ambayo wewe unaifanyia
unyama na ukatili wa kutisha kiasi hicho. Je, na wao waamue
kuwatendea vivyo familia na nduguzo uliowaacha nyumba? Kwa
maana hiyo nchi hii hatakalika.
Happness, leo uko kwenye
ajira ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikishwa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM). Na kwa maana hiyo umekuwa ukisifia hata
lisilohitaji sifa, na kutumia mwanya huo kuandika kwa nyodo
na kiburi kwa kutusi upinzani. Kumbuka kuwa ajira ni dhamana
tu!
Mwisho wa siku utajikuta unarudi na kujiunga na
hawahawa kwenye masuala fulani ya kufanikisha shughuli zako
za kikazi na zile za kijamii wakati fulani.


 

      On Thursday, January
29, 2015 5:35 PM, "'allanlawa@yahoo.co.uk'
via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
wrote:
     

  Am so sorry for the
vulgar language Happiness has been using against MPs from
the opposition particularly lately against Hon. Mbatia
following the motion he moved in parliament after  Prof.
Lipumba was battered by police. She is an ambarrasment to
Bagamoyo.UNiversity. For some of us who know the genesis of
UB, Mbatia is one of those who agitated for its
establishment. For Happines to disparage him is like bitting
the hand which feeds her. UB, take note that your public
affairs officer has disengaged from her emisary work of
promoting a positive image of the college to spoilling the
integrity the college had already built.
Sent from
Yahoo Mail on Android
             
                 
                     

                     
                         
                             
                             
                                 From:
                             
                             'Happiness Katabazi' via
Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
                           

                             
                                 To:
                             
                             WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>;
                                                             
               

                             
                                 Subject:
                             
                             [wanabidii] 'WELI SPANA
' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI                   
         

                             
                                 Sent:
                             
                             Thu, Jan 29, 2015 2:11:52 PM   
                       

                         
                             

                             
'WELI SPANA
' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

* MBUNGE LUSINDE MUNGU AKUPE
MAISHA MAREFU
Na Happiness Katabazi
LEO nimepata fursa ya kutaza tena Kipindi cha
Bunge kilipoanza hadi kumalizika mchana kupitia Televisheni
ya Taifa TBC 1 nakuona michango mbalimbali ya maoni kuhusu
Hoja ya Dharula iliyawasilisha na Mbunge wa kuteuliwa watoto
wa mjini wanawaita ni wabunge wa kuteuliwa ni ' Wabunge
wa Lifti', James Mbatia.

Awali ya yote na kwa moyo mkunjufu napenda
kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mbunge wa Mtera
,Livingstone Lusinde kwa mchango wake alioutoa Leo bungeni
asubuhi  Kwani umejaa ukweli mchungu kwa wa wakorofi
,wazushi na wanasiasa uchwara wa vyama baadhi ya vyama Vya
upinzani ambao ni wazi wamefirisika kiajenda na walikuwa
wamekusudia kuigeuza Kesi inayomkabili Ya Jinai Na. 25/2015
.

Iliyofunguliwa na Jamhuri
dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi wa
  CUF, Jana Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es
Salaam, Kuwa ni Gia ya kujipatia Umaarufu wa kisiasa, kutaka
kufanya jaribio la kumuundia mtego mwingine Waziri Mkuu
Mizengo Pinda ili ang'olewe madarakani Kama walivyozoea
lakini  jaribio Hilo Leo tena limekufa  kifo cha Mende
mapema kabisa.

Ama kweli
Ngoma ya kitoto yaani 'Ngoma ya wapinzani' ,Na kweli
Ngoma ilivyoanzishwa na wapinzani Jana bungeni na Kuzusha
tafrani hadi Bunge likaairishwa haijakesha ,hoja ya Mbatia
aliyoianzisha kwa mbwembwe imemalizwa na Chikawe,
Masaju,Lusinde, Said Mkumba ,Henri Shekifu , Sadifa Hamis
Juma 'kilainiii Kama wana nawaa'

Nilimtazama na kumsikiliza Tundu Lissu na
baadhi ya wabunge wenzake wa upinzani ,kwanza wakati
wakachangia mada zao walikuwa wakionekana Kuwa na jazba Hali
iliyosababisha kushindwa kujadili kwa vielezo kinzani
taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani , Mathias Chikawe.

Hali iliyosabisha taarifa hiyo
ya Chikawe ambaye ni
  msomi wa sheria na alishawahi kuwa Mwanasheria wa Serikali
kama alivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju
ambaye naye aliwahi kuwa Mwanasheria mzuri tu wa serikali na
kazi alizozifanya na kusaidia serikali kushinda kesi kubwa
Si za Kutafuta, zipo wazi.

Taarifa yake kubaki Kama ilivyo kwasababu
walioleta hoja ya dharula na wachangiaji wa vyama ya
upinzani wameshindwa kuilarua kwa vielezo taarifa hiyo ya
Chikawe ambaye Profesa Ibrahim Lipumba yeye upenda kumuita
Chikawe Kuwa ni ' Cheki Bob'.

Licha Lissu ambaye alikuwa ni mchangiaji wa
kwanza alifanikiwa kumtikisa Spika Makinda kuhusu suala la
uchache wa muda na Makinda akatikisa na Akaamua kuufuta
uamuzi wake wa awali wa kuwapatia dakika Tatu kila mbunge
kuchangia,badala ya Lissu Kumtikisa ndiyo Akaamua Kusema
kila mbunge atachangia dakika Kumi .

Huo ni ushindi kwa msomi Lissu ambaye ujasiri
wake siyo tu ni wa kuzaliwa nao pia una changiwa na fani ya
Sheria aliyosoma pale Chuo
  Kikuu cha Dar es Salaam.Hongera Lissu kwa ujasiri huo Kwani
katika Hilo ulikumbuka Kanuni inasema je na ukainukuu.Wasomi
wa Sheria tunasema ulifanya 'citation'.
 
Nilichojifunza kwa kwa
wabunge wachache wa upinzani Leo kupitia michango Yao kwanza
Wengi wao wanapenda kukuza jambo dogo lionekane kubwa,
Kutenda matendo ambayo yanazidi kuporomosha heshima ya
viongozi wa upinzani na upinzani kwa ujumla, uongo na unafki
na kushindwa kujadili mada iliyopo mezani na kuamua kuingiza
mada ambazo siyo mada iliyokuwa imepangwa kujadiliwa Leo.

Baadhi ya wabunge wa upinzani
Leo waliochangia Walijikuta kujitolea Mifano Yao binafsi
Kuwa wamewahi kupigwa na kubambikiwa Kesi na Polisi na
kuzungumzia kifo cha Mwanahabai Daud Mwangosi.

Kwa hiyo  ni wazi hawa Tayari
wanaupande(bias). Na wakasahau taarifa ya waziri Chikawe
ilikuwa ikielezea tukio Moja tu la Temeke lilitokea Januari
27 Mwaka huu ,lilomuusisha Lipumba na Si vinginevyo.

Mfano
  mzuri Mbowe alipokuwa akichangia pamoja na Kusema alikaa
muda mrefu Polisi Central Dar es Salaam, kuakikisha Lipumba
anapata dhamana alitumia muda mwingi kueleza eti na yeye
alishawahi kupigwa na Bomu, mashine gun na Hao Hao
Polisi.

Sasa watu wenye
akili timamu tunajiuliza HIvi kweli MTu upigwe na silaha
zote hizo nzito yaani Bomu, Mashine Gun halafu uendelee Kuwa
mzima tu?Huu sio uongo Mkuu jamani ?

Si ni Mbowe huyu huyu Bunge lilopita baada ya
Bunge Hilo kutaja maazimio ya Bunge kuhusu Sakata la Escrow
, Mbowe alisimama Bungeni na kumtaka waziri Mkuu Pinda
azidishe Ukali maana eti Pinda amezidi Kuwa mpole ndiyo
mAana mambo yanavurugika.

Haya tusaidieni Tushike la Mwenyekiti wa
Chadema,Mbowe aliyemtaka Pinda awe Mkali au Tushike
Mwanasheria wa Chadema, Lissu anayetaka kwa Nguvu zote Pinda
aachie ngazi?

Pia
Nilichojifunza wabunge wa upinzani wengine ni wasahaulifu
akiwemo Lissu.Wametaka Pinda ajiuzuru kwasababu Juni 20
mwaka
  2013  ,Pinda alisema ndani ya Bunge wale wote watakao
kaidi sheia za nchi watapigwa  na kwamba kauli hiyo eti
Ndiyo maana polisi wanaendelea kupiga watu na kwa sababu
hiyo Pinda ajiuzuru.Ni aibu ya aina yake.

Kwa faida yenu Nyie wabunge
wasahaulifu na msiotaka kufanya utafiti Kabla ya kuzungumza
.

Kituo Cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC),  Chama cha Wanasheria Tanganyika,
Agosti Mosi Mwaka 2013 kulifungua Kesi ya Kikatiba
Na.24/2013 Katika Mahakama Kuu Kandaya Dar es Salaam, dhidi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Pinda

Juni 6 Mwaka 2014 , jopo la majaji watatu
Dk.Fauz Twaibu, Augustine Mwarija na Fakhi Junfu, walitoa
uamuzi wa awali wa Kesi hiyo ambapo jopo hilo lilikubaliana
na pingamizi la awali lilokuwa limewasilishwa na Wakili wa
wadaiwa ambaye alikuwa ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali
ambaye kwa sasa ndiye Mwanasheria Mkuu wa serikali Masaju
Kuwa walalamikaji walikuwa hawana haki ya kuwashitaki
  washitakiwa , waliokuwa wanahaki ya kumshitaki Pinda na
Mwanasheria Mkuu kuhusu Kauli hiyo ya Pinda ni wanachi na
siyo Taasisi hizo  (Legal Person) .

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu kuhusu Kauli hiyo ya
Pinda upo na hadi sasa naandika makala hii bado Mahakama ya
Rufaa haijatengua uamuzi huo hivyo bado ni uamuzi halali na
Unatakiwa uwafuatwe na sisi wasomi wa Sheria tunautumia Kama
'refence'.

Sasa
nashangaa sana wabunge wetu Hao wanaotaka  Pinda  ajiuzuru
wakati Mahakama Kuu ilishatoa uamuzi wa Kesi hiyo na Kesi
ile ilifutwa Katika Hatua za awali.

Kweli sasa nalazimika kuamini maneno ambayo
yamekuwa yalisemwa na Pinda  aka ' Mchawi' ,Kuwa
anaandamwa kwa uzushi na kuchafuliwa kwasababu tu ametangaza
kimya kimya Kugombea urais.

Maana misioni 'connection' ya hoja ya
dharula ya Mbatia hapa na wabunge wa upinzani kulazimisha
Pinda, ajiuzuru.

Kupitia
michango hiyo ni wazi kabisa kuna baadhi ya wanasiasa
  wanamchukia Pinda.Haiwasaidii na ni dhambi kumchukia
binadamu mwenzako.

Jana
Bungeni wabunge wa upinzani walichukua muda mwingi kuleta
tafrani bungeni hadi bunge likaairishwa , tukajua leo
watakuja na michango kabambe kumbe hakuna kitu ,wameshindwa
kujadili taarifa ya waziri Chikawe.

Na matokeo yake mbunge mmoja wa CUf akaishia
kuligeuza Bunge Hilo lisijui ni Kanisa Ka ufufuo na uzima wa
kufufua marehemu waliokufa na kuanza kusoma Majina
aliyedaiwa ni ya marehemu waliouwawa Unguja na Pemba.

Minajiuliza kuna ufufuo wa
marehemu pale Bungeni?  Hayo Majina ya marehemu ingekuwa ni
vyema angeyaleka kwenye makanisa yanayofufua wafu Kama yapo
lakini siyo bungeni.

Mbunge
Habib Mnyaa amesema Lipumba alishasemehe Mauji yale ya
Unguja na Pemba, haya Nyie baadhi ya wabunge wa CUF Kama
siyo kiherehere cha kujadili bungeni Mauji ya marehemu yake
na kuyataja Majina ya marehemu wale ni kitu gani?

Ni kiherehere na Kufirisika
  Kiajenda .Maana Mwenyekiti wa Chama chenu cha CUF Lipumba,
alishasemehe Mauji Yale, kilichowawasha kitu gani Kuja
kujadili Mauji yake bungeni kitu gani?

Nafahamu nitawakera sana wale watu wanaopenda
ukorofi na wasiyoaka kutii sheria bila shuruti na ambayo
kutwa wamekuwa wakishitiki maandamano haramu.Mtanisamehe
sana.

Leo katika makala hii
namuomba sana Waziri Chikawe katika bajeti ijayo aliombee
jeshi ka polisi fedha za kununulia Weel Spana nyingi sana
ili zianze kutumiwa na jeshi ka polisi kuwarekebisha akili
wananchi wakorofi ambao wameonekana ngozi,akili zao kuwa
ngumu sana kama gari aina ya Fiati hali inayosababisha
wakipigwa virungu ,virungu vinavunjika.

Weel Spana Katika zama hizi hasa kuelekea
Katika wakati wa kupiga kura za maoni ya Katiba Pendekezwa
Aprili 30 na uchaguzi Mkuu Mwaka huu unatarajiwa kufanyika
Oktoba Mwaka huu, Polisi wa zitumie sana Katika kurekebisha
akili za wananchi wakorofi ambao wamekuwa wagumu kutii
  Sheria Kama shuruti na Miili Yao imekuwa ni migumu Kama
Gari aina ya Fiati hivyo Weel Spana ni matumizi sahihi
kabisa kwa watu waina hiyo.

Polisi msitumie tena silaha za Moto wala
virungu,tumieni Weel Spana kurekebisha akili za hawa wavunja
Sheria za nchi kwa makusudi Hali inayo sababisha wananchi
wasiyo na hatia na mali zao kuumizwa , wananchi kuishi na
wasiwasi na shughuli za uchumi kwenda kwa kusuasua kwasababu
ya wapumbavu wachache wenye Malengo ya kujipatia Mtani wa
kisiasa kwa kuvunja Sheria za nchini.

Mtu ambaye siyo mkorofi, na havunji Sheria ni
Nadra sana kukutana na Weel Spana wala virungu Vya
Polisi.

Kumbukeni hata
Katiba ya Nchi inatoa haki na inamtaka aliyepewa haki hiyo
ambaye ni Mwananchi kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa
Sheria.

Katiba inasema kila
Mwananchi anajukumu la kulinda Sheria za nchi zisivunjwe.Pia
Mhimili wa serikali upo pale kutekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa Sheria na kamwe haiwezi kumuona
  Mwananchi anafungwa Sheria kwa makusudi halafu imuache bila
kumchukulia Hatua.

  Kwa
maoni yangu Matumizi ya Weel Spana kwa Jeshi la Polisi HIvi
sasa ni muhimu sana ili Weel Spana ziweze kurekebisha akili
za hawa wananchi ,wanasiasa wakorofi na wavunja Sheria za
nchi.

Baadhi ya wapinzani 
wanajifanya hawana akili wanaovunja Sheria makusudi hivyo
basi Weel span zikitumiwa kwenye Miili Yao Sitasaidia sana
kurekebisha akili zao zikae sawa.

Naheshimu mchango wa vyama Vya upinzani nchini
,ila nawashauri kadri siku zinavyozidi kwenda waanze Kujenga
tabia ya Kuwa na subira, Kuwa wa kweli Katika baadhi ya
mambo mnayo ya jadili Bunge Kwani watu wengine
wanaowaaminiwa sana kila macho sema sasa inapotokea kiongozi
wa upinzani  nayeye Kusema uongo watu watapoteza Imani na
Nyie Kama baadhi ya wananchi walivyopoteza Imani na viongozi
wa CCM na serikali.

Binafsi
Lissu namheshimu sana lakini kwa kitendo alichokifanya Leo
cha
  kusimama ndani ya Bunge na Kusema uongo Kuwa eti TBC 
wamezima Matangazo Yao ili umma usiangalie kinachojadiliwa
Bunge wakati sisi tulikuwa tu naendelea kutazama Bunge na
kumuona yeye kupitia Televisheni jinsi anavyosema uongo wa
wazi ambao umemshushia asilimia Fulani ya uaminifu  kwa
wafuasi wake Leo, siyo tabia nzuri.

Lissu msomi wa Sheria ni lazima alisoma somo la
Legal Research wakati akisoma shahada ya Sheria ambalo somo
Hilo linamtaka msomi yoyote wa Sheria anapojadili jambo
lazima awe amelifanyia utafiti.

Sasa Leo Lissu kaka yangu uliteleza kwa kwa
Kusema Bila kufanya utafiti Kuwa TBC imezima matangazo yake
wakati TBC hadi kufanya hivyo.

Nguvu nyingi na vitendo Vya Fedha Jana wapunge
wa upinzani mlevi fanya bungeni kushinikiza Jana hoja ya
Mbatia ijadiliwe lakini hao kujadiliwa ikajadiliwa Leo na
Leo yenyewe Nyie mliojifanya mnauchungu wa kuijadili Wengi
wenu mlitoka nje ya mada.

Matokeo yake Spika Makinda
  kamaliza kwa Kusema Bunge lake lina Ruhusu Kesi
inayomkabili Lipumba iendelee na anamshukuru wabunge
waliochangia hawajaingilia Mwenendo wa Kesi.

Hivyo Lipumba watoto wa mjini
kwa hitimisho Hilo la Bunge kuhusu hoja ya Mbatia iliyokuwa
ikikuhusu wewe ni kwamba ' hadithi yetu imeishaa
hapo'.

Kashda ,na
vibweka vyote Vya wana UKAWA wenzio bungeni vikijaribu
kukunusuru wewe vimegonga mwambwa, na hivyo unaendelea
kuangaika na Kesi hiyo ya jinai inayokukabili ,Mbatia na
Mbowe na wabunge wengine waliokuwa wanajaribu kukusemea
bungeni Jana na Leo muda Si mrefu hutawaona Jijini Dar es
Salaam, watakuwa kwenye kampeni Katika majimbo yao yanafanya
kampeni, hutawaona tena wakikusindikiza Katika Mahakama ya
Kisutu. Hiyo inaitwa kila Mtu atabeba  msalaba wake
Mwenyewe.

Nasisitiza tena
Weli Spana ni kifaha muhimu sana HIvi sasa kutumiwa na
Polisi  kurekebisha akili za wapinzani wakorofi na wavunja
Sheria za nchi.

Mungu
ibariki
  Tanzania
Chanzo: Facebook: Happy
Katabazi
0716 774494
Januari
29 Mwaka 2015



Sent from my iPad

--
Send
Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com  Utapata
Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to
this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements
and facts must be presented responsibly. Your continued
membership signifies that you agree to this disclaimer and
pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message
because you are subscribed to the Google Groups
"Wanabidii" group.
To unsubscribe
from this group and stop receiving emails from it, send an
email to
  wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com.
For more options,
visit https://groups.google.com/d/
optout.
                     
                 
             



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.


     


--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@
googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.


       




--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment