Thursday, 29 January 2015

Re: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

Huyu binti uandishi wake ni wa kulazimisha yaani hata spelling ya neno wheel spana ndo huandikwa hivo

On Jan 29, 2015 8:14 PM, 'Abdul Karim' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Mungu yupi huyo anayefurahi wakati viumbe wake wakidhalilishwa mpaka ampe Lusinde maisha marefu?

Kwa ndugu wa karibu wa mheshimiwa Lusinde, napenda wamshauri ndugu yao kuwa kuna maisha baada ya CCM na kuna maisha baada ya Ubunge!
 

From: 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: WANABIDII <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, January 29, 2015 5:11 PM
Subject: [wanabidii] 'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI


'WELI SPANA ' NI DAWA TOSHA YA WANASIASA WAKOROFI

* MBUNGE LUSINDE MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU
Na Happiness Katabazi
LEO nimepata fursa ya kutaza tena Kipindi cha Bunge kilipoanza hadi kumalizika mchana kupitia Televisheni ya Taifa TBC 1 nakuona michango mbalimbali ya maoni kuhusu Hoja ya Dharula iliyawasilisha na Mbunge wa kuteuliwa watoto wa mjini wanawaita ni wabunge wa kuteuliwa ni ' Wabunge wa Lifti', James Mbatia.

Awali ya yote na kwa moyo mkunjufu napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mbunge wa Mtera ,Livingstone Lusinde kwa mchango wake alioutoa Leo bungeni asubuhi  Kwani umejaa ukweli mchungu kwa wa wakorofi ,wazushi na wanasiasa uchwara wa vyama baadhi ya vyama Vya upinzani ambao ni wazi wamefirisika kiajenda na walikuwa wamekusudia kuigeuza Kesi inayomkabili Ya Jinai Na. 25/2015 .

Iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi wa CUF, Jana Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Da es Salaam, Kuwa ni Gia ya kujipatia Umaarufu wa kisiasa, kutaka kufanya jaribio la kumuundia mtego mwingine Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili ang'olewe madarakani Kama walivyozoea lakini  jaribio Hilo Leo tena limekufa  kifo cha Mende mapema kabisa.

Ama kweli Ngoma ya kitoto yaani 'Ngoma ya wapinzani' ,Na kweli Ngoma ilivyoanzishwa na wapinzani Jana bungeni na Kuzusha tafrani hadi Bunge likaairishwa haijakesha ,hoja ya Mbatia aliyoianzisha kwa mbwembwe imemalizwa na Chikawe, Masaju,Lusinde, Said Mkumba ,Henri Shekifu , Sadifa Hamis Juma 'kilainiii Kama wana nawaa'

Nilimtazama na kumsikiliza Tundu Lissu na baadhi ya wabunge wenzake wa upinzani ,kwanza wakati wakachangia mada zao walikuwa wakionekana Kuwa na jazba Hali iliyosababisha kushindwa kujadili kwa vielezo kinzani taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani , Mathias Chikawe.

Hali iliyosabisha taarifa hiyo ya Chikawe ambaye ni msomi wa sheria na alishawahi kuwa Mwanasheria wa Serikali kama alivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju ambaye naye aliwahi kuwa Mwanasheria mzuri tu wa serikali na kazi alizozifanya na kusaidia serikali kushinda kesi kubwa Si za Kutafuta, zipo wazi.

Taarifa yake kubaki Kama ilivyo kwasababu walioleta hoja ya dharula na wachangiaji wa vyama ya upinzani wameshindwa kuilarua kwa vielezo taarifa hiyo ya Chikawe ambaye Profesa Ibrahim Lipumba yeye upenda kumuita Chikawe Kuwa ni ' Cheki Bob'.

Licha Lissu ambaye alikuwa ni mchangiaji wa kwanza alifanikiwa kumtikisa Spika Makinda kuhusu suala la uchache wa muda na Makinda akatikisa na Akaamua kuufuta uamuzi wake wa awali wa kuwapatia dakika Tatu kila mbunge kuchangia,badala ya Lissu Kumtikisa ndiyo Akaamua Kusema kila mbunge atachangia dakika Kumi .

Huo ni ushindi kwa msomi Lissu ambaye ujasiri wake siyo tu ni wa kuzaliwa nao pia una changiwa na fani ya Sheria aliyosoma pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Hongera Lissu kwa ujasiri huo Kwani katika Hilo ulikumbuka Kanuni inasema je na ukainukuu.Wasomi wa Sheria tunasema ulifanya 'citation'.

Nilichojifunza kwa kwa wabunge wachache wa upinzani Leo kupitia michango Yao kwanza Wengi wao wanapenda kukuza jambo dogo lionekane kubwa, Kutenda matendo ambayo yanazidi kuporomosha heshima ya vi

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment