Monday 29 December 2014

[wanabidii]

FALAKI
(Dkt. Muhmmed Seif Khatib)

Ulimwengu ni vitu vyote vilimo ndani ya dunia na nje ya dunia.Miongoni mwa vitu vilivyoumba ulimwengu ni sayari - umbile lilioko angani na kuelea ambalo
huzunguka jua.Dunia yetu ni moja kati ya sayari zieleazo angani bila kuanguka au
kugongana.Ulimwengu ni pamoja na nyota ionekanayo kama mpira ambayo ni gesi
inayoungua na kutoa mwanga usiku.Lipo jua ambalo ni nyota itoayo mwangaza
mchana na kuipa joto dunia.Upo mwezi kitu kinachong'ara na kutoa mwangaza usiku.
Mwezi huizunguka dunia kwa siku ishirini na nane.Vitu vyote ikiwemo majini,mashetani,binadamu,wanyama,wadudu,viumbe vya bahari,miti,mimea na vyengine ambavyo tujuavyo na tusivyovijua kwa ujmla wake ndiyo ulimwengu.Mwanadmu ni kiumbe
mwenye maarifa na ujuzi.Anatambuwa uwepo wa ulimwengu,wakaazi wake na yeye
ndiye mmiliki wa yote.Moja ya taaluma na maarifa yahusuyo misimu na namna nyota
zinavyochukua maumbo mbalimbali na maana yake huitwa falaki. Mienendo hiyo ya nyota na sayari wapo wanaoamini na kuhuhusisha na matokeo mbalimbali ya mwanadamu.
Mwaka wenye miezi kumi na mbili unafikia ukingoni.Katika mwaka uliopita matukio
mengi yametokea na kuathiri minenendo ya watu.Katika uwanja wa siasa vifo kadha
wa kadha. vimetokea.Msemo kufa kufaana ulijiri.Madiwani kama binadamu walipoteza maisha
kwa mfulilizo wa vifo.Chaguzi katika awamu mbili ulitokea.'Chopper' tatu
na viti vitatu vilivyodonolewa na chama cha upinzani huku chama tawala kujizolea
kwa mzo.Awamu ya pili uchaguzi wa madiwani waliofanyika.Wenye 'Chopper',
nao waliporomoka na wa Chama cha Mapinduzi kikapaa.
Chaguzi maalum za katika majimbo katika awamu mbili zikendeshwa.Wenye 'Chopper'
wakapaa lakini hawakufika katika eneo la Wingu litakiwalo.Kama kawaida chama
cha CCM kikafanya kazi na kuzoa viti vingi vya ubunge.Genge la vyma vya siasa
vya upinzani vikasarambatika huku wakabaki hawaamini yaliyojiri.Ni kama kawaida
yao hawakuacha kulalamika.Kwa yale maeneo machache walioshinda uchaguzi
ulikuwa huru na haki. Maeneo waliyogaragazwa uchaguzi umechakachuliwa.

Bunge la Katiba likachukua nafasi yake.Mijadala mizito ikaibuka tokea ya Hati
ya Muungano kuwa haipo hata kufika kuumbuliwa kwa waasisi wa Taifa letu
Nyerere na Karume.Kura ya siri na dhahiri ikaleta kichfuchefu. Mwisho muundo
wa serekali mbili na tatu ukalipasua bunge.Kambi ya vyama vinne tu vya upinzani
ikaachia ngazi ya bunge wakabaki kipiga makelele kupitia madirishani,katika majukwa,
makongamano na warsha.Safari ya kuisaka Katiba inayopendekezwa ikapamba
moto. Msituko ukatokea pale kura za Zanzibar na Bara zikaikubali katiba inayopendekezwa.Wapinzani walioko nje ya bunge wakashuka mabega na Chkupwelewa..Ndani ya bunge chama cha CCM na makundi mengine wakaongoza.Katiba
inopendekezwa inasubiri Kura ya Maoni mwezi April mwakani.Kugua kwa vidole kwa
vyama vya upinzani katika siasa havikuacha kulumbana na CCM.
Uchaguzi wa
Serekali za Mitaa,vijiji na vitongoji vikahitimisha safari ya mwaka mzima ya
la upinzani kuingia katika korongo.Zipo sehemu wameendeshwa mrisi! Zipo
sehemu wamekwenda kapa!Kedi na viburi vyao vimekwisha.Bakora za ushindi

zimewachapa wapinzani kila mahali.Bado wanaendelea kulia kwa kwikwi na kite!Kwakutumia taaluma ya falaki wajiulize kwa nini wamdoda kwa kila tukio kwa mwakahuu unaokwisha?Chaguzi za madiwani wamegaragazwa.Chaguzi za wabunge wamekula mtama.
Katiba inopendekezwa wameachwa solemba! Uchaguzi wa serekali za mitaa,
vijiji na vitongoji wapo katika chumba cha wagonjwa mahututiz!
Kwa kuwa mwaka
unakwishwa tufumbe macho.Tuinuwe mikono yetu juu kuwaombea duwa na sala
wapinzani, ' Mungu uwajaaliye kwa mwaka mpya wa 2015 uwe na nuhusi kwao.Wanguke katika kila uchaguzi.Kila wanalolitaka wasilipate.Mungu uwajaaliye wawe wanagombana
na kipigana wenyewe kwa wenyewe - AMIN'





Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment