Tuesday 30 December 2014

Re: [wanabidii] 'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA TIBAIJUKA

Mhegera nimekupata vizuri sana lakini mimi naamini kupitia maandiko anayoandika Happiness Katabazi kuunga mkono ufisadi wa ajabu unaoendelea nchini huku wananchi wengi wakiwa katika umaskini uliokithiri, nadhani kama huyu dada yako unayemtetea asiittwe debe tupu yaani tabula rasa, unamkosea sana. Ni bora ungekubali aitwe hivyo halafu umwombe au umwelekeze arudi kwenye mijadala ya kuleta mantiki badala ya blaablaa anazoandika  katika huu mtandao. Anasema "KASINGE MNO PROFESA TIBAIJUKA" kisha anatoa tafsri ya neno hilo huku akimpongeza kwa jinsi alivyowabeza hata hao waandishi wa habari wenzie kwa kuwaambia hivi mnadhani nimekuja hapa kusema ntajiuzuru ndio maana mmekuja wengi? Kama ningelikuwa mimi ni mwandishi wa habari ningeondoka katika huo mkutano wa huyo prof. maana alikosa staha na heshima kwa waandishi wa habari na watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii. Inakuwaje umewaalika watu nyumbani kwako wameitikia wito wako halafu unaanza kuwacharua eti kwa nini wamekuja wengi wakati wewe ndiye uliyewapa mwaliko huo? hayo si matusi kwa waandishi wa habari na watanzania kwa ujumla? Halafu anajitokeza mwandishi wa habari ambaye ni mwanafunzi wa a noble profession yaani sheria anaanza kumsifu mtu wa namna hiyo. Unataka mtu kama huyu tumweke kundi gani kama siyo kwenye kundi la matabula rasa?Ingekuwa ni bora baada ya Rais kumtosa huyo profesa wake angejitokeza tena kwenye mtandao huu akaandika kuomba msamaha kwa kauli yake halafu aueleze pia umma wa watanzania kuwa pamoja na kwamba rais amemfukuza kazi Tibaijuka, bado hajakidhi kiu ya watanzania kwa sababu amekuwa mbaguzi kwa kumfukuza Tibaijuka tu na baadae kufuatia kusimamishwa ukatibu mkuu wa Maswi tu. Nilitegemea huyo Happiness amwulize rais mbona akina Mnikulu wake wa hapo ikulu na RITA, na TRA, na wengineo waliotajwa kwenye taarifa ya PAC na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali hawajasimamishwa kupisha uchunguzi dhidi yao? Au hao wako kwenye hekalu takatifu ambalo halipaswi kuguswa? To me this is not fair and it is an indicator of discrimination. All people involved in the Tegeta Escrow A/C are supposed to be taken before the TEMPLE OF JUSTICE,that is the Court to face charges against their acts. Wameachwa wote. Katiba yetu inazuia ubaguzi wa aina yoyote ile na kuwa watu wote wako sawa mbele ya macho ya sharia na mlinzi mkuu wa katiba ni rais. Mbona amekuwa mbaguzi kwa kuchukulia hatua wengine na wengine kuwaacha. Si lazima kuwafukuza lakini angalau angetoa maelekezo wasimamishwe kazi wakati uchunguzi dhidi yao unafanyika. Hajafanya hivyo, je huo si ubaguzi? Simtetei Tibaijuka ila nahoji ni kwa nini na wengine wenye kutuhumiwa kwa makosa kama ya kwake nao wasingechukuliwa hatua stahiki kama alivyochukuliwa Tibaijuka na Maswi? Au hao watumishi wa Ikulu na RITA si watumishi wa umma wanaostahili kutendewa kama watumishi wengine wa Umma? Kuhusu majaji, anamtwisha mzigo jaji mkuu kwa nini wakati katiba iko wazi kwamba rais ana mamlaka ya kuunda tume ya uchunguzi wa jaji juu ya maadili yake ya kazi(Majaji wasiopungua watatu na mmojawapo atoke nje ya nchi katika nchi za jumuiya ya madola? Nilitegemea huyu anayejiita msomi wa sheria ahoji hayo na siyo kuja na blaablaa za kitabula rasa halafu sisi wenye akili zetu, wenye macho yet na, wenye midomo yetu na wenye masikio yetu tukae kimya tu kumsikiliza huyu kilaza. Unahoji kuhusu kuajiriwa na UB? Kwani nani amekwambia katika kipindi cha Serikali hii (Awamu hii ya nne) qualification ni kigezo cha ajira? Kama bado una mawazo hayo pole sana ndugu yangu. Wewe ulikuwa wapi wakati ajira za uhamiaji zimeleta utata na baadae tume ikaja na ilichogundua?Wewe uko wapi? Huulizi hata waajiriwa wa BoT na TRA wanapatikanaje? wewe tangu upate akili zako kama una umri kama wangu ulishawahi kuona wapi usaili (Interview) inafanyika uwanja wa Taifa kwa wasailiwa elfu kumi wakati nafasi za kazi ni watu sabini? Huo ndo utaratibu wa ajira serikalini na kokote? Uliona wapi mambo hayo yanafanyika kwenye awamu ya kwanza? Ya pili? Ya tatu? uliona hayo mambo yakifanyika? Kama uliona ni wewe peke yako lakini sisi tumeyaona kwenye awamu hii ya NNE. Kwa hiyo kwa watu  tabula rasa kama Katabazi kuajiriwa UB na baadae kupata usajili wa kusomea sheria bila kujali uwezo wao kitaaluma ni jambo la kawaida tu. Mimi na mama Ananile Nkya tulishampa ushauri wa bure kabisa kwamba Happiness Katabazi asiwe anakurupuka tu na kujiandikia chochote tu eti kwa sababu tu anataka kuuonesha ulimwengu wote kuwa naye ni msomi wa sheria. Tulimshauri awaone walimu wa sheria waliobobea kama Prof Palamagamba Kabudi, Prof. Gamaliel Mgongo Fimbo, Prof Shaidi, Prof Kanywanyi,Prof,Ibrahim JUma (JA), Prof,N.Nditi, Prof. Mtaki na madokta wa sheria wengine weledi wamfundishe sheria hata kwa kuwaomba tu maana hao maprofesa wetu ni weledi mno wa sheria na wanapoona  mtu kama Katabazi anaboronga katika profession yao sidhani kama wanafurahi. Tatizo la huyu mwanadada ana kiburi sana na nadhani hata watumishi wenzake wanapata taabu sana kufanya naye kazi. She pretends to know every thing while in fact she knows nothing. Mimi nadhani kuna kipindi kimoja katika television ya STAR TV kinaitwa FUTUHI na kuna Mhusika (I think he is the main character) katiaka igizo hilo anaitwa Brother "K" au kwa jina  maarufu anaitwa wa kukurupuka. Watoto wangu wanakipenda sana kipindi hicho kwa sababu ya vitendo vya kukurupuka vya msanii huyo maarufu. Naona na mimi kuanzia leo wanabidii wote tuanze kumwita Happiness Katabazi WA KUKURUPUKA, Na hilo liwe ni jina lake la ubatizo katika mtandao huu kuanzia leo.
Adios, amigos,
IT'S I
Leonard Magwayega, ESQUIRE 


On Monday, December 29, 2014 8:49 PM, 'elias mhegera' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Kwa heshima niliyokuwa nayo kwa mdogo wangu Happiness Katabazi sikutaka kuchangia mada yake ya 'kasinge' lakini binafsi sidhani kama ni sahihi sana kumuita tabula rasa yaani 'empty minded' na kwa Kiswahili chepesi 'debe-shinda!' binafsi nimemfahamu binti huyu miaka mingi toka alipokuwa mwanafunzi wa sekondari tukiwa majirani Sinza Mugabe. Kisha akajiunga Habari Corporation kabla ya kwenda katika gazeti la Tanzania Daima akaandika mambo mengi mazuri nakumbuka niliusoma wasifu ulioandikwa na binti huyo baada ya kifo cha Prof Chachage niliupenda sana kwa sasa yeye ni muajiriwa katika Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB).  Siamini chuo kikuu chochote chenye vigezo kinaweza kuajiri 'tabula rasa'. Niweke wazi kwamba kuna exaggeration katika hukumu inayotolewa kwake. Kinyume chake mimi nadhani binti huyu amekuwa 'victim of circumstances' baada ya kusoma sheria na akili yake ikamtuma kwamba mtu ukijua sheria basi ndiyo umejua kila kitu! Toka Happiness asome sheria 'logical sequence' yake imekuwa 'very poor' na anahitaji msaada.  siamini  kama kweli Tanzania inaongozwa na sheria kwa kiwango kinachotakiwa, na hii ni kwa sababu tupo chini ya mfumo wa 'kutwaa' yaani 'authoritarianism' kiasi kwamba hata majaji wan-succumb  kwa immoral and unethical politicians
no wonder judiciary imekuwa contaminated na escrow scandal, achana na mtangulizi wake EPA, nadhani hiyo itifungue macho tuone tatizo lipo wapi badala ya kutumia risasi (submachne gun) kumuua sungura! Hapiness ni kiwakilishi cha fikra za baadhi ya Watanzania na wala si kwamba yeye ni a separate individual 'it is a chain of thinking!' lipo tatizo kubwa kwenye mfumo wa siasa za nchi kiasi kwamba nchi hii inapenda sana wanafiki 'hypocrites' kulikoni watu wanaosema ukweli. Tumsadie binti yetu kwa sababu tayari kaonesha ujasiri isipokuwa tunahitaji kuutumia katika dira chanya kulikoni huko anakoelekea sasa, naomba kuwasilisha...
 
Elias Mhegera
Pan African Human Rights Defender
Director of Research and Investigations 
Tanzania Journalists for Human Rights Association (Journorights)
Journalist and Counselor
Tel: 255-0754-826272
        255-0715-076272
Email: mhegeraelias@yahoo.com 
             mhegera@gmail.com 
The only thing we have to fear is fear itself


From: 'leonard magwayega' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, December 29, 2014 4:22 PM
Subject: Re: [wanabidii] 'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA TIBAIJUKA

Of course Mr.Allan we have a duty to educate that young lady on how to address this network as we think it is high time for us to discuss serious matters like that of ESCROW a/c seriously and vehemently not like the so said Happiness Katabazi does. It is the time which we need critical thinkers who can come up with critical discussions through this network in order that we at least assist the Nation to move positively from where we are currently. If we stick to ideas of people like Happiness Katabazi we shall bury the Nation which in my considered opinion is at ICU. Let every critical thinker play his/her positive role to stop the rotten acts like that of escrow so that we can at least save something little left for our children and the future generation.
I believe that together we can bring positive changes for the benefit of our poorest people who can not afford even a single meal per day while very few people have accumulated a very huge amount of all possible resources for their own benefits and their so called blessed generation. I wish you all a happy new year 2015.
adios, it's I,
Leonard Elias Advocate, ESQ.


On Monday, December 22, 2014 11:25 AM, "'allanlawa@yahoo.co.uk' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


Hon. Magweyaga lets keep on knocking sense into her head one day she will realize.


From: 'leonard magwayega' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] 'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA TIBAIJUKA
Sent: Mon, Dec 22, 2014 6:35:23 AM

Katabazi, Happiness ni tabularasa msimsikilize. She has no brain in her head. She is an empty headed, so for us who went to school perfectly we should not waste our time to discuss the business of a tabularasa woman.
Advocate Leonard Elias Magwayega-ESQUIRE.


On Friday, December 19, 2014 10:03 AM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA  TIBAIJUKA
Na Happiness Katabazi
KASINGE ni neno linalotumiwa watu wa Kabila la Wahaya wanaotokea Bukoba Mjini,Bukoba Vijijini na Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo,Mwanamke wa Shoka ,msomi wa Kiwango Cha Juu wa ngazi ya Kimataifa amabye ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ni Mhaya.

Neno  Kasinge hutumika kumwambia mtu aliyefanya jambo fulani ambalo wewe umeliona jambo Hilo ni Zuri hivyo umshukuru  kwa kumwambia Kasinge.

Leo namwambia Nshomile, Profesa Tibaijuka ambaye ni Mwasisi wa Baraza la Wanawake (BAWATA) ambalo lilitikisa nchini enzi zile za Utawala wa serikali awamu ya Tatu hadi kufikia Mwanasheria Mkuu wa serikali kulipinga mahakamani, kwa msimamo wake aliouonyesha jana katika Mkutano wake na waandishi wa habari na alisema;

' Yeye msomi mwenzake Profesa Sospeter Muhongo ni majembe ya Baraza la mawaziri na ajihudhuru ng'o Kwani Haoni Sababu ya kufanya hivyo.Minamuunga mkono Kwani Hana kosa alilolitenda na msimamo wangu ndiyo huo siku zote.

Tena ' Nshomile' Tibaijuka umenikosha Katika Moja ya sentensi yako ambayo umesema hata Mungu aliwapa nafasi ya kujieleza Adamu na Eva Katika Bustani ya Edeni walipotuhumiwa. 

Nasema umenikosha Kwani Katika makala yangu ya wiki iliyopita nilitaka  watuhumiwa wa Escrow Wapewe haki Yao ya Msingi ya kusikilzwa Kwani hata Mungu alimpatia Eva na Adamu haki hiyo ambayo sisi wasomi wa Sheria tunaiita ' Right to be heard'.

Makala yangu hiyo ilikuwa na kichwa Cha Habari kisemacho: KIKWETE USIWASIKILIZE ' BUSH LAWYER KATIKA ESCROW'.

Nshomile m Tibaijuka ,kwa maelezo yako ya Jana naimani hata wale mabongolala wa Sakata la Akaunti ya Escrow watakuwa wameanza kukueleza.Maana nchi hii kuna baadhi ya watu yaani ni mabongolala wanajadili mambo wasiyoyajua uhalisia wake na wanawahukumu watu bila hatia.

Nshomile Tibaijuka, achana na mabongolala yaani watu wasiyo na akili na wana ajenda zao chafu za siyo tu za Kukupaka matope  pia Profesa Muhongo na serikali pia isitawalike kwa Amani.

Songa Mbele ,na minaamini muda Si mrefu mabongolala ,wazandiki ,wazushi na Wapika majungu kuhusu Akaunti ya Escrow wataumbuliwa hadharani.Imefika zamu Yao kuvuliwa nguo hadharani. Kasinge mno Nshomilie Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, Omukama akubele.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Disemba 19 Mwaka 2014.




Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment