Wednesday 31 December 2014

Re: [wanabidii] 'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA TIBAIJUKA

Huyu binti anaweza kuwa na wazo kichwani lakini anakosa muda wa kuliweka vizuri anahitaji msaada badala ya kumshambulia. Kama hana tatizo lolote anaweza kuwa mwanasheria wa ajabu kabisa asiyeweza kupanga hoja anayowasilisha kwa umakini. Tumsaidie aweze kufika anakotaka kufika. Mungu wa Tibaijuka ni yule aliyemteua, ametuambia alimpa nafasi ya kujitetea lakini maelezo yake hayamkumridhisha kama vile utetezi wa Adamu kudanganywa na Eva ulivyokosa kumridhisha Mungu akaadhibiwa. Sisi tulio "mabongolala" tumeona, inakuwaje wewe nshomile usione?


From: 'Gikaro Ryoba' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, December 30, 2014 8:26 PM
Subject: Re: [wanabidii] 'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA TIBAIJUKA

katabati,
naona umeanza kuweweseka tena. ni kwanini unawatukana wanaCCM kwa kuwaita mabongolala? huogopi kuitwa kuhojiwa kwenye vikao vya chama chenu? kama unadhani wanaCCM ni bongolala huoni kwamba hata wewe ni bongolala au wewe umeishajitoa?


On Friday, December 19, 2014 10:03 AM, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:


'KASINGE MNO 'PROFESA ANNA  TIBAIJUKA
Na Happiness Katabazi
KASINGE ni neno linalotumiwa watu wa Kabila la Wahaya wanaotokea Bukoba Mjini,Bukoba Vijijini na Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo,Mwanamke wa Shoka ,msomi wa Kiwango Cha Juu wa ngazi ya Kimataifa amabye ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ni Mhaya.

Neno  Kasinge hutumika kumwambia mtu aliyefanya jambo fulani ambalo wewe umeliona jambo Hilo ni Zuri hivyo umshukuru  kwa kumwambia Kasinge.

Leo namwambia Nshomile, Profesa Tibaijuka ambaye ni Mwasisi wa Baraza la Wanawake (BAWATA) ambalo lilitikisa nchini enzi zile za Utawala wa serikali awamu ya Tatu hadi kufikia Mwanasheria Mkuu wa serikali kulipinga mahakamani, kwa msimamo wake aliouonyesha jana katika Mkutano wake na waandishi wa habari na alisema;

' Yeye msomi mwenzake Profesa Sospeter Muhongo ni majembe ya Baraza la mawaziri na ajihudhuru ng'o Kwani Haoni Sababu ya kufanya hivyo.Minamuunga mkono Kwani Hana kosa alilolitenda na msimamo wangu ndiyo huo siku zote.

Tena ' Nshomile' Tibaijuka umenikosha Katika Moja ya sentensi yako ambayo umesema hata Mungu aliwapa nafasi ya kujieleza Adamu na Eva Katika Bustani ya Edeni walipotuhumiwa. 

Nasema umenikosha Kwani Katika makala yangu ya wiki iliyopita nilitaka  watuhumiwa wa Escrow Wapewe haki Yao ya Msingi ya kusikilzwa Kwani hata Mungu alimpatia Eva na Adamu haki hiyo ambayo sisi wasomi wa Sheria tunaiita ' Right to be heard'.

Makala yangu hiyo ilikuwa na kichwa Cha Habari kisemacho: KIKWETE USIWASIKILIZE ' BUSH LAWYER KATIKA ESCROW'.

Nshomile m Tibaijuka ,kwa maelezo yako ya Jana naimani hata wale mabongolala wa Sakata la Akaunti ya Escrow watakuwa wameanza kukueleza.Maana nchi hii kuna baadhi ya watu yaani ni mabongolala wanajadili mambo wasiyoyajua uhalisia wake na wanawahukumu watu bila hatia.

Nshomile Tibaijuka, achana na mabongolala yaani watu wasiyo na akili na wana ajenda zao chafu za siyo tu za Kukupaka matope  pia Profesa Muhongo na serikali pia isitawalike kwa Amani.

Songa Mbele ,na minaamini muda Si mrefu mabongolala ,wazandiki ,wazushi na Wapika majungu kuhusu Akaunti ya Escrow wataumbuliwa hadharani.Imefika zamu Yao kuvuliwa nguo hadharani. Kasinge mno Nshomilie Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, Omukama akubele.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
0716 774494
Disemba 19 Mwaka 2014.




Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment