Monday 29 September 2014

[wanabidii] VIONGOZI WA CHADEMA WILAYA YA LUSHOTO WAHAMIA CCM


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Ismail Semkunde aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema na kuamua kurejea CCM.
 Mzee Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 inavyoendelea.
 Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema. Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde,aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha

Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji.


Umati wa watu waliohudhuria mkutano.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mzee Charles Kagonji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment