Sunday, 28 September 2014

[wanabidii] Unavyoweza kufikia mafanikio bila kujali kiwango cha elimu

Elimu ni muhimu sana ili kuweza kupata utaalamu na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye maisha. Katika baadhi ya taaluma ili uweze kufikia mafanikio makubwa ni muhimu uwe na elimu kubwa hasa ya chuo kikuu. Lakini pia bado kila mtu anaweza kufikia mafanikio makubwa hata kama hajapata elimu hii ya chuo kikuu. Kuna idadi kubwa sana ya watu waliofanikiwa lakini hawana elimu kubwa.

Leo tutaona ni jinsi gani unavyoweza kufikia mafanikio makubwa bila ya kujali kiwango chako cha elimu. Iwe una elimu ya darasa la saba, sekondari au hata chuo kikuu, una uhakika wa kufikia mafanikio makubwa kama utafanya yafuatayo;

1. Anza mapema.

Tafuta kitu unachopenda kukifanya na anza mapema kukifanya. Kipende sana kitu hiko na kifanye kwa moyo mmoja.Kuwa na shauku kubwa ya kufanikiwa kupitia kitu hiko na usikate tamaa au 
kuyumbishwa. Kumbuka kama unataka kufanikiwa usifanye kazi. Soma makala hiyo kujifunza zaidi.

2. Tafuta mtu wa kukuongoza(Mentor).

Katika kazi au biashara uliyochagua kufanya iwe una elimu au la tafuta mtu aliyefanikiwa kwenye fani hiyo ambaye unaweza kumuamini kisha mfanye awe anakuongoza. Mtu huyu ndiye atakayekupa ushauri na uzoefu kwa sababu alishapita unakopita wewe. Pia atakushika mkono wakati ambapo mambo yanakuwa magumu na unafikiria kukata tamaa.

3. Jifunze jinsi ya kuuza.

Haijalishi umeajiriwa au umejiajiri, unafanya kazi au unafanya biashara kila mmoja wetu ni muuzaji. Kama umeajiriwa unauza muda wako na utaalamu wako na kama ni mfanya biashara unauza bidhaa/huduma na pia unauza haiba yako, maneno yako na kadhalika. Wale ambao wanajua jinsi ya kuuza vizuri ndio wanaofanikiwa kwenye kila nyanja ya maisha. Hivyo jifunze mbinu za uuzaji(sales) ili uweze kujua njia bora ya kuuza kile unachouza.

4. Kuza mtandao wako.

Kumbuka haijalishi unajua nini, bali unamjua nani. Mafanikio ya sasa yanatokana na mahusiano na ushirikiano mzuri na watu. Kuza mtandao wako kutokana na kazi au biashara unayoifanya. Ni kupitia mtandao huo ndio utapata wateja na hata fursa zaidi zitakazokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

5. Soma sana.

Soma vitabu vingi sana kulingana na kile unachofanya. Uzuri wa dunia ya sasa vitabu vinapatikana kwa urahisi sana na vina elimu kubwa sana. Kama umekosa mtu wa kukushika mkono(mentor) basi vitabu vinaweza kuchukua hatua hiyo. Soma sana, sana, sana.

Ni vitabu vingapi unahitaji kusoma? Vitabu vingi sana, havina kikomo ila visipungue 500 katika wakati wote wa kazi au biashara yako.

6. Kuwa kiongozi.

Bila ya kujali kiwango chako cha elimu, jifunze tabia za uongozi na uwe kiongozi mzuri. Hii itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana. Kama umejiajiri au unafanya biashara hii ni sifa moja itakayokuwezesha kutengeneza timu nzuri itakayokuletea mafanikio. Kama umeajiriwa hii ni sifa ambayo itakuwezesha kupanda cheo haraka na kushika nafasi za juu zitakazokuwezesha kufikia mafanikio.

7. Fanya kazi.

Pamoja na yote tuliyojadili mpaka sasa, kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ndio msingi wa maendeleo. Watu wengi wamekuwa na dhana kwamba ukisoma sana hufanyi kazi ngumu, na hii ndio inasababisha watu wengi wanashindwa kufikia mafanikio. Pia watu walioajiriwa huamini muda wao wa kufanya kazi ni pale anapoingia na kutoka kazini tu, ndio maana nao wanachelewa sana kufikia mafanikio makubwa. Mpaka sasa sijaona mtu aliyefikia mafanikio makubwa ambaye hajafanya kazi sana, unahitaji kufanya kazi sana.

8. Jifunze jinsi ya kukubaliana(negotiate).

Hii ni sifa ambayo kila mtu anayetaka kufikia mafanikio ni muhimu kuwa nayo. Haijalishi ni kiwango gani cha elimu unacho, uwezo wa kujadili na kukubaliana na wengine utakuwezesha kupata fursa nzuri ambazo zitakufanya uweze kufikia mafanikio makubwa.

9. Tatua matatizo.

Kila mtu na kila jamii ina tatizo fulani ambalo bado halijatatuliwa. Ukiweza kutatua tatizo hilo, watu watakuwa tayari kukupa fedha ili kupata suluhisho la tatizo lao. Kujua na kutatua matatizo ya aina hii haihitaji uwe na degree, uwezo wako mkubwa wa kujifunza kutokana na mazingira yako ndio utakaokuwezesha kujua na kutatua matatizo hayo ya watu.

10. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Kama unavyojua, kukosa maarifa ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye kazi, biashara, familia na hata maisha kwa ujumla. KISIMA CHA MAARIFA ni mtandao maalumu ambao utakupatia wewe maarifa ya kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye kile unachofanya na hata kwa maisha yako kwa ujumla. Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kuchota na kunufaika na maarifa haya. Bonyeza maandishi hayo yanayofuata KUJUA JINSI YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA 

Usifikiri tena ya kwamba kwa kuwa hukupata elimu kubwa basi huwezi kufikia mafanikio makubwa. Mambo ya kufanya ndio hayo hapo, anza kuyafanyia kazi sasa na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio makubwa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment