Sunday, 28 September 2014

[wanabidii] Re: TAHADHARI BUNGE MAALUM LA KATIBA-KAMA NI LAZIMA KUPIGA KURA TUMIENI BUSARA

Leo ni siku ya kupigia kura rasimu ya katiba inayopendekezwa. Ni siku itakayoweka historia muhimu kwa nchi yetu kuandaa katiba mpya.  Ni siku itakayotuthibitishia Watanzania kuwa gharama ya fedha na muda tulizowekeza katika mchakato huu zimeleta manufaa tuliyotarajia. Kwa wote wnaofuatlia mchakato huu, ni wazi kuwa Watanzania tumegawanyika katika makundi tofauti ya wanaoona kuwa mchakato umeharibika na hautaleta manufaa na wengine  wanaoona kuwa tuaendelea vizuri. Lakini pia kuna kundi jingine, tea hili ni kuwa sana la wasiojua kinachoendelea na hawajali mwisho wake-wao wanasubiri katiba itoke tu. Kwa upande wangu, kuwa na tofauti ya mawazo ni kitu chema kwani ndicho kitakachozaa tunda jema. Tatizo ninaloliona ni hii tabia ya kukosa uvumulivu wa kusikiliza mawazo ya wengine kwa utulivu na ustaarabu hata kama hukubaliano nayo! Wajumbe wa bunge  maalum la katiba waliteuliwa kwa nia ya kuthibitisha kuwa maoni ya Watanzania katika rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba yalizingatiwa katika rasimu iliyowakilishwa na tume hiyo. Lakini sote tumeona magawanyiko wa wajumbe hawa, ambao kimsingi wamesukumwa na itikadi za vyama vyao.

Leo wanakwenda kupiga kura wakiwa katika mgawanyiko huo na wengine hawapo kabisa! Sina uhakika kama leo ni kupiga kura kweli au ni kupitisha yaliyojadiliwa na upande mmoja wa makundi haya. Naiona hii ni hatari, na hofu yangu ni kuwa hata kama mapendekezo haya yatapita, tutaenda katika awamu ya kura a moni na mgawanyiko huu na ambao unaweza kuwa mkubwa zaidi. Tumeanza kuona makundi hayo ya wajumbe waliogawanyika wakijiandaa kwenda kuwahamasisha wananchi kutetea hoja zao hata kabla ya muda wa kura za maoni kufika. Sote tunajua athari za mgawanyiko wa wajumbe waliodhaniwa kuwa kuwa timu moja ya uhamisishaji  wa katiba mpya kwa jamii...... Namwomba Mwenyezi Mungu  atuepushe.

Nimesema leo ni siku muhimu kwa wajumbe hawa kuonyesha uzalendo wao kwa kaifa hili lililojaa kila aina ya heshima katika kulinda amani na utulivu. Ni siku ambayo budsara za hawa wajumbe zitathibitika na kutuongoza katika njia hiyo hiyo ya amani na utlivu wakati wa kura za maoni au mchakato mwingine utakaoamuliwa kumalizia ngwe hii ya kupata katiba mpya. Tahadhari ninayoitoa ni kuwa wajumbe wote walio Dodoma kwa kupiga kura leo wavae Utanzania wa kweli. Watakuwa wanaweka rekodi kaika histori ya nchi na sidhani kama watataka kuwa kwenye rekodi ya sifa mbaya kwa vizazi vijavyo. Siwezi kuwashawish zaidi ya yaliyokwisha zunguzwa na wengi huko numa lakini bila shaka mtayazingatia kwa kila uamuzi utakafikiwa leo.

. Historia imetuonyesha kuwa siku zote SAUTI YA UMMA hushinda kwa vile ni ya UMMA na si vinginevyo.

Mimi ni sehemu ya SAUTI YA UMMA

Makongo

----------------------------------------------------------------
Japhet Maingu Makongo
Director, Ubunifu Associates Ltd
P.O. Box 32971, Dar es Salaam,
TANZANIA
Website: www.ubunifu.co.tz, info@ubunifu.co.tz,
Tel: +255 22 2762027, Mobile:+255 754 571 256

0 comments:

Post a Comment