misangocharles via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Kinachokera katika mjadala huu ni watu kujifanya vipofu kutoangalia upande wa pili badala yake kuonesha ubaya wa ukawa tu. Nani alifurahishwa na mwenendo ule wa bunge maalum la katiba? Upendeleo wa waziwazi wa kiti, dharau, kejeli na matusi mazito! Haya hayasemwi! Mkoje ninyi watu?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
From: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 1 Aug 2014 17:07:19 +0100
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] VIONGOZI WA UKAWA WANAZIDI KUKATISHA TAMAA
Hapa inaonekana nia ya masuala yao si katiba. wana lingine ndani ya kificho cha UKAWA na katiba. Waafrika sisi Mungu atupe nini? Kil;a mara nchi zetu ni ubinafsi, malumbano mpaka kufikia vita vya kuharibu nchi, kuua na kuharibu uchumi. hao wa Libya, Misri wamepata nini. Congo nako, Nigeria na nchi nyingine Africa utata mtupu.Mzuingu anafurahi kuona monkeys tunaendelea kuota na kukuza mikia yetu badala ya kushirikiana, kuelewana na kuleta maendeleo. Mmakonde kasema-Yonda ni Yonda tu mtupie tu ndizi!! Mungu tusaidie tufunuke tuache misifa na ubinafsi.
On Friday, 1 August 2014, 18:16, Leila Abdul <hifadhi@gmail.com> wrote:
VIONGOZI wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Kataba ya Wananchi (Ukawa), wanadaiwa kumkatisha tamaa na kumvunja moyo Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, katika kufikia maridhiano ya pande mbili zinazotishia kukwamisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha maridhiano kati ya wajumbe wa Ukawa na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kilichokutana kutwa nzima ya jana katika hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam, na baadaye kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa Ofisa ya Msajili waliokuwa eneo hilo la hoteli, zinasema wajumbe wa Ukawa wamekuwa ni watu wasioeleweka kutokana na tabia yao kuibua mambo mapya kila kinapoitishwa kikao baina ya pande mbili hizo.
Kikao hicho cha jana kilichofanyika chini ya upatanishi wa Msajili wa
Vyama, Jaji Mutungi, kinaelezwa kuwa cha nne tangu Msajili huyo aanze
juhudi za kuwaweka pamoja wajumbe wa pande mbili hizo za Ukawa na CCM, ili pamoja na mambo mengine, vikao vya Bunge Maalum la Katiba kwa ajili ya kutafuta Katiba mpya viweze kuendelea kama kawaida mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa habari hizo, kikao hicho cha jana kilitarajiwa kuwa kikao cha mwisho cha maridhiano katika juhudi hizo za kukwamua mchakato huo ili kuwapa wajumbe wa Ukawa, ambao pia ni wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, nafasi ya kujiandaa na safari ya kuelekea Dodoma kwenye vikao vya Bunge hilo vinavyotarajiwa kuanza rasmi Jumanne ijayo, Agosti 5, mwaka huu.
Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni jana, kulikuwa na taarifa za ndani ya kikao hicho zinazoeleza wazi kwamba hakukuwa na uwezekano wowote wa pande mbili hizo kufikia maridhiano baada ya Ukawa kuwasilisha hoja zao tisa mpya, badala ya hoja mbili ambazo ziliridhiwa na pande mbili hizo katika kikao kilichopita ambacho kilikuwa ni cha tatu, kwamba zingejadiliwa katika kikao jana na kufikia hitimisho la majadiliano hayo.
Kwa mujibu wa habari hizo, hoja tisa hizo zilizowasilishwa na Ukawa katika kikao hicho cha jana, zilishajadiliwa na kufikiwa muafaka na pande mbili hizo katika kikao kilichopita, zikawekwa kiporo hoja mbili ambazo ndizo zilipaswa kujadiliwa jana kabla ya kufikia hitimisho.
"Hawa Ukawa wanamvuruga tu Msajili kwa sababu hawaeleweki ni kitu gani hasa wanachokitaka…kwa kweli wamem-put off (kuvunja moyo, kuvunja nguvu) Msajili wa vyama vya siasa, uwezekano wa kufikia maafikiano na maridhiano ili tuweze kurejea bungeni kuendelea na mchakato wa kutafuta Katiba mpya ni mdogo sana," kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya kikao kwa sharti la kutotajwa.
Nje ya kikao hicho, baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Msajili walionyesha
kushangazwa na hali hiyo ya kutofikia muafaka, --
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment