Thursday, 28 August 2014

Re: [wanabidii] Re: URAIS 2015 - MIGOGORO NDANI YA CHADEMA

Uchaguzi wa CHADEMA Mkoa wa Mara waibua mazito.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara, jana Tarehe 27/08/2014 kilifanya uchaguzi wa ngazi ya Mkoa na kupata viongozi wapya watakaoongoza jahazi la kuing'oa CCM madarakani 2014/2015.

Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa "Musoma Club" uliopo ndani ya mtaa wa Mkendo, manispaa ya mji wa Musoma, mkabala na Jengo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa.

Uchaguzi ulikuwa wa Uhuru na Haki kwa nafasi zote zilizofanya uchaguzi, isipokuwa nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa iliyoahirishwa kutokana na badhi ya wagombea wa nafasi hizo kuwekewa pingamizi zilizotokana na tuhuma mbalimbali zilizopaswa kushughulikiwa na ngazi za juu za Chama.

Miongoni mwa wagombea waliowekewa pingamizi hizo ni Mwita Waitara ambaye ni Kiongozi mwandamizi wa Chama Makao Makuu.

Waitara anakabiriwa na tuhuma ya;
* Kuhusika na sakata la madiwani wa Shinyanga waliokisaliti Chama na baadae kuomba radhi.

* Kuwa anahusika na sakata la usaliti wa akina Zitto, Kitila Mkumbo na Mwigamba, maana kwenye shitaka hilo lililowasilishwa kwenye Kamati na kusomwa na Mwanasheria wa Kanda ya Ziwa Mashariki, mlalamikaji anadai kwamba anao ushahidi wa kudhibitisha pasi na shaka kwamba Mwita Waitara ndiye M2 aliyewahi kutajwa kwenye waraka wa akina Zitto Kabwe.

* Kuwa alikutwa akitoa rushwa ya fedha, vyakula na nauli za safari kwa wapiga kura.

* Kuwatukana na kuwakashifu wagombea wenzake bila sababu.

NB:Tuhuma hizi ni kwa mujibu wa ushahidi wa Sauti iliyorekodiwa na Picha zinazoonyesha na kuakisi matukio hayo.

Nafasi nyingine iliyoachwa wazi ni nafasi ya Katibu wa Vijana kutokana akidi ya kura kutotimia angalau nusu ya wapiga kura wa nafasi hiyo.


On Wednesday, August 27, 2014 10:49:57 PM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:
sasa ni sasa nne dakika 33
ni siku mbaya kwa mtoto wa mfugaji na mkulima wa kutoka kijiji cha kangarian wilaya ya tarime.
nilikuwa nashiriki uchaguzi wa mkoa wa mara.
kesho nitasema kwa kujikumbusha historia yangu katika mapambano.
Nimetuhumiwa nimeumia sana
tuwe wapole wakati natafuta haki yangu.


On Wednesday, August 27, 2014 6:56:31 PM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:
MWENYEKITI WA CHADEMA WA MKOA WA TABORA NDUGU K. MBAROUK AMEJIUZURU LEO, SABABU ZA KUJIUZURU KWAKE NI KUTOKANA NA UONGOZI WA JUU KUTO KUSHUGHULIKIA MIGOGORO ILIYO NDANI YA CHAMA NA KUKIACHA CHAMA NA WANACHAMA WAKE KUFARAKANA.
SAMBAMBA NA MWENYEKITI HUYO PIA KADA MAARUFU KUTOKA HUKO HUKO TABORA BWANA M. KWITIME NAE PIA AMEJIUZURU KWA SABABU HIZO HIZO.

On Wednesday, August 27, 2014 6:55:50 PM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:
Vijana Wa Red brigerd Wa chadema Arusha wakuongozwa na kamanda wao krisi ambaye ndiye kamanda wa Red brigerd Arusha jimbo wamepigana hadi kumwagana damu maeneo ya Ostabey unga LTD kuelekea Sombetini ambapo walikuwa wanatangaza mkutano wao Wa hadhara 

Baada ya kuumizana mziki ulizimwa ghafla na kurudi kuelekea ofisini kwao Ngarenaro

On Wednesday, August 27, 2014 8:54:18 AM UTC+3, Lusajo Mwasampeta wrote:
Asante Muganda kwa angalizo, natatizwa zaidi pale uongozi wa jukwaa unapofumbia macho hidden identities! 

Lusajo

Sent from my iPhone

On 26 Aug 2014, at 10:15 pm, Emmanuel Muganda <emug...@gmail.com> wrote:

Lusajo
Wala usitegemee kupata jibu.
He is on a one way mission to disseminate 
and misinform. 
em

Sent from my iPhone

On Aug 24, 2014, at 5:08 PM, Lusajo Mwasampeta <sirjo...@gmail.com> wrote:

Ndiyo ndugu, umetumiwa email! Lakini wewe ni nani? Mabadiliko Chadema nahisi si jina lako halisi!
Nisaidie kitendawili hiki kwanza

Sent from my iPhone

On 25 Aug 2014, at 12:01 am, MABADILIKO CHADEMA <mabadili...@gmail.com> wrote:

taarifa toka ndani ya chama hicho kwa email niliyotumiwa zinaonyesha kuwa viongozi wa kubwa wa chadema wanamhofia sana kijana huyu kuwa anaweza kutumika kukiathiri chama hicho kama ambavyo alitumika kuwaathiri baadhi ya wanasiasa waliokuwa na nguvu kubwa ndani ya chadema

mara baada ya maamuzi hayo kufanyika ilibidi wamtafutie sababu ya kumuengua kwenye mchakato wakugombea uenyekiti wa bavicha taifa kwa kumwambia kuwa amezidi umri kwa miezi isiyozidi 15,,,ili kutomtia hasira kijana huyo na kuanza kukishambulia chama

watu wa karibu na ben wanasema kuwa ben amekubali barua hiyo ya kuzidi umri kinafiki lakini anapambana kuhakikisha maadui zake ndani wa chadema wana malizika na yeye anapata nafasi kubwa akiwa chadema

taarifa zisizo rasmi zinasema pia kuwa bensaanane ameshaanza mazungumzo na katibu wa ACT- TANZANIA ENDAPO WATAMPA UENYEKITI WA VIJANA WA CHAMA HICHO,ATAJIUNGA NAO


On Sunday, August 24, 2014 10:44:45 AM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:

ANGALIZO
Chama chetu CHADEMA kimekuwa tumaini kubwa la WATANZANIA wanaofanyiwa kila aina ya uovu na Chama cha majambazi na vibaka Ccm!
Hivyo tunatakiwa kuonesha jamii kuwa sisi ni chama ambacho wananchi wanakiota ndotoni kila siku kuja Kuongoza Tanzania 2015!

Kuna mambo ambayo baadhi ya ndugu zetu wanakosea si vema endapo nikayasema tukarekebishana hususani katika CHAGUZI zetu ndani ya chama!
Kuna watu wameweka makundi
Wewe unayeweka makundi tafadhali tunaomba acha mara moja, Chadema haina makundi, Sisi sio wahaini Ccm ambao wanafanya biashara ya kuwaweka watu wasio na sifa katika uongozi, ambao wanashabikia majambazi mafisadi na magaidi kwa makundi ili wapate kula na uongozi mfano Kundi la Jambazi kuu Lowassa, Kundi la anayetaka kupita kindugu jambazi Membe, Kundi la ndumilakuwili mzee wa Ccj Sitta na kundi la gaidi Idd Amini Dadaa Mwigullu Nchemba na wengine, hawa ni mahasimu na maadui ambao wako tayari watoane roho ingawa wapo Chama kimoja cha Mafisadi Ccm wote kwahiyo tuendelee kujijengea heshima ya kutokuwa na makundi 2015 Tuongoze nchi yetu.

Tukemee kwa pamoja Rushwa,
Tunataka tupate viongozi wenye sifa za uongozi na si wafanyabiashara wa kununua uongozi, mfanyabiashara yeyote yule anataka apate faida kubwa sana isiyo ya kawaida kitaalamu tunaita Super normal profit! Hivyo tukatae Rushwa kwasababu inamnyima mtu mwenye uwezo haki yake ya kutumia ujuzi wake aliojaaliwa kutuongoza.

Tukemee unafki,dharau, matusi na kejeli
Uchaguzi wa ndani ya Chama ni kama yai ambalo linatakiwa libebwe kwa mikono miwili, tukikosea tu na kuwekeana dharau,unafki, matusi na kejeli tutakuwa tunaichoma moto nyumba ambayo sisi sote tumo ndani yake, ukitumia mbinu chafu ni dhahiri kuwa hautaweza kuwaongoza uliowafanyia mbinu hizo na hawatakuwa na imani na wewe hivyo utasababisha chama kujigawa,
Sisi ni familia moja, tupeane moyo hata kama sote ni wagombea wa nafasi moja kwasababu yeyote kati yetu atakayeshinda atakwenda kutuwakilisha, Sisi ni timu moja tunaelewana na kupeana pasi na yeyote akifunga goli tunashangilia kwa pamoja bila kujali aliyefunga anacheza namba ngapi.
Kuwatumia viongozi, watu maarufu na media! Kuna watu wanapitia migongo ya watu wengine ili kutuharibia chama, wanatumia vibaya media, Viongozi wanatumika kuwasapoti watu wao wa karibu hata kama hawana uwezo wa kutuongoza pamoja na watu maarufu, Niliwahi kusema kuwa hayati Mwalimu Nyerere angeweza kuweka ukoo wake wote madarakani ila kwa kutambua kuwa yeye alikuwa na sifa za uongozi ila ndugu zake hawakuwa nazo ndio maana hakuwaweka ndugu zake madarakani hivyo tujifunze kupitia yeye! Tukiwekana kindugu hatutakuwa tofauti na ajira za wizara ya uhamiaji.
Nna mengi ya kuandika lakini la mwisho ni kwamba lazima tuweke akilini kuwa CHADEMA hatuna ALIYESHINDWA wala ALIYESHINDA ila kuna tunaowapa RIDHAA wakatuwakilishe kwa kuwapigia kura nyingi, TUTAKAOKOSA RIDHAA HII au TULIOKOSA RIDHAA HII tusikate tamaa, nilipata kujifunza kitu fulani toka kwenye historia ya John Heche, kuna nafasi aligombea na alipata kura chache sana na za aibu kwa mtu mwenye moyo wa nyama kama mimi na wewe huenda tungekata tamaa lakini alipiga moyo konde na kusimama na kuonesha ukomavu wa kisiasa na baadae akashinda kwa kishindo na kishujaa na mpaka sasa ni kiongozi wa Taifa Bavicha na ni Mbunge wa Tarime anayesubiriwa kwa hamu kutangazwa!
Nimeyasema haya yote kutokana na primitive politics za vijembe na mipasho ambazo zilikuwa zinamlenga my comrade in arms Ben Wa Saanane, kilichonisikitisha na kusikitisha wapambanaji na wakomavu wa kisiasa wa kweli wengi zaidi ni kwamba huyu mtu hata fomu hakuwa amechukua ila hwakusita kupambana na kivuli chake, aibu na uchawi wanajishika wenyewe sasa kwa kutambua kuwa Ben hagombei!
Hivi mnajisikiaje?
Mtamtazamaje Ben mkionana?
Zaidi ya kuinamisha nyuso zenu chini kwa aibu?
Kwa niaba yao naomba watu wote tunaoitakia mema CHADEMA tuwasamehe na tuwafundishe kwa upendo na hekima jinsi ya kugombea na kuishi maisha ya kifamilia ndani ya chama
Tutiane moyo na si kuvunjana, mwenye mapungufu tumsaidie kuondoa udhaifu wake na tuifiche aibu na udhaifu wake kwa kumfundisha akapate kuwa mwanachama na kiongozi bora!
Niwatakie usiku mwema
Alamsiki!
Aluta continuer, Victory Ascerta!


On Saturday, August 23, 2014 1:45:32 PM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:

MENE MENE TEKEL NA PERES.... BAVICHA SASA I SALAMA.

Nilisema kuna mgombea anataka kwenda mahakamani kuzia uchaguzi wa BAVICHA kwa sababu ya kanuni ili agombee, nilim-pre-empty mapema baada ya kuinasa, tayari mwanasheria wake alishadraft, nashukuru public reaction ilikuwa kubwa sana dhidi yake. teh teh teh teh! Mkakati ulikuwa hivi - official complaints dhidi ya kanuni zingekwama, PLAN B ilikuwa kwenda mahakamani.... Nikamuwahi, akasitisha.

Sina nukta wala chembe ya shaka dhidi ya wagombea wengine wa Bavicha kuhusu UZOEFU na UADILIFU wao... Imekaa poa!! SASA Bavicha itakuwa salama salimini kwenye mikono MISAFI na SALAMA...

Utawezaje kupanga mikakati na kutangaza nia ya kugombea huku ukijua you don't qualify??? Imenikumbusha mwanasiasa mmoja anayefanya juhudi za kugombea Urais 2015 wakati akijua mwaka huo atakuwa na miaka 39...!!! kwi kwi kwi kwi... Imenikumbusha ya MFALME JUHA.

Una GPA ya 2.1 halafu unapanga mikakati ya kutaka Urais wa DARUSO wakati kigezo mojawapo ni GPA ya 3.5....!!!

"uwendawazimu ni kufanya jambo lilelile kwa namna ile ile huku ukitegemea majibu tofauti" Msigwa.

"Akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa" Msigwa.

"Chama ni kikubwa zaidi ya mtu binafisi" Mbowe.

Nyuki hakumbatiwi, ncha ya mkuki haipigwi konzi, msumeno haupigiwi mswaki..maji ya betri hayaendewi msalani" Dady Igogo.


On Saturday, August 23, 2014 1:16:11 PM UTC+3, MABADILIKO CHADEMA wrote:

Maamuzi Rasmi juu ya barua yangu ya mgogoro wa kikanuni/masharti ya uchaguzi wa baraza la vijana Chadema(BAVICHA) Taifa yamefanyika.

Fomu za uchaguzi zilizotolewa tarehe 12/08/2014 , liliwekwa sharti kuwa mgombea awe na miaka 18-30(Awe amezaliwa 1984 na kuendelea).

Sharti hili lililowekwa kwenye mabano lilinisukuma ku-challenge kanuni/masharti/mahesabu hayo pamoja na masharti mengine kwa kufuata taratibu za chama kama nilivyowaeleza na nikaahidi kusubiri uamuzi

Hoja yangu ilikua kama aliyezaliwa tarehe 01.01.1984 ana haki ya kugombea kwanini isiwe mimi niliyezaliwa tarehe 13/12/1983 yaani wiki mbili na nusu kabla yake kwa kuwa hadi siku ya uchaguzi atakua na miaka 30 na miezi 9 na siku 10 wakati mimi nitakua na miaka 30 na miezi 9 na siku 28 halikadhalika yule aliyezaliwa tarehe 11/09/1983 atakua na miaka 30 na miezi 11 na siku 30 hadi siku ya uchaguzi tarehe 10.09.2014.

Na kwamba ingekua sahihi kama sharti hilo "SHARTI NDANI YA MABANO" lingetamka sawi kuwa mgombea asiwe amefikisha miaka zaidi hadi ifikapo siku ya uchaguzi.Hii ndio ilikua hoja yangu.

Nilirejea katiba na miongozo yetu na kanuni za uchaguzi uliopita wa Baraza la Vijana uliofanyika Mwezi Mei 2011.

Maamuzi ni kuwa wagombea waliozaliwa kuanzia mwaka 1984 ndio watakaokuwa eligible kugombea kama inavyoonekana kwenye fomu zitakazojazwa na wagombea na zipo pia kwenye tovuti ya chama.

Kutokana na maamuzi haya nasikitika kuwatangazia vijana wenzangu kuwa ,kufuatia "SHARTI HILO NDANI YA MABANO " NIMEJIENGUA RASMI KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI KUWANIA NAFASI YA JUU KUONGOZA BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA).

Maandalizi mliyonishauri niendelee nayo wakati nasubiri uamuzi yatasitishwa

Maandalizi yote ya mkutano na waandishi wa habari kesho Travertine Hotel tumeyasitisha rasmi,Maandalizi ya kurejesha fomu jumatatu ambayo jeshi la polisi liliarifiwa na kukiri kupokea barua iliyoandikwa na vijana waliotaka kunisindikiza kurejesha fomu kuanzia viwanja vya BIAFRA kuelekea Makao makuu yamesitishwa.

Kwa moyo wa kipekee na kwa unyenyekevu mkubwa,nawashukuru marafiki zangu wa karibu na wa mbali,nawashukuru marafiki wa BAVICHA kwa maandalizi kabambe ya kampeni,Nawashukuru ninyi marafiki zangu hapa Facebook na mitandao mingine kwa kuniunga mkono kwa wingi wenu na kujitolea kupambana na dhuluma na hila chafu chafu za watu wachache sana waliokua wakifanya siasa chafu katika safari hii.Mlijitolea kulinda haki,misingi na falsafa ya chama chetu na pia principle zenu kwa kile mnachoamini bila woga.Mlis

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment