Friday, 1 August 2014

Re: e: [wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?

mobhare
U are right na uchambuzi wako upo vzr kaka


On Friday, August 1, 2014 2:53 AM, "hosea.ndaki@gmail.com" <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:


Miruko tusiseme wakurya wengi bila data, kumbuka mzanaki sio mkurya.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Miruko <rsmiruko@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, August 1, 2014 11:12:56 AM GMT+0300
Subject: Re:Re: [wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?

Ndaki, wewe ulikuwa  jeshini au JKT?

hosea.ndaki@gmail.com wrote:

Wanaosema wakurya wengi jeshini mtupatie idadi yao, binafsi kikosi nilichokuwepo wakurya walikuwa wawili meja chacha na mp koplo marwa, pia kutopewa nafasi za juu inawezekana kutokuwa na elimu, jeshini hupandi cheo kwa kulenga shabaha tu ni pamoja na kuhudhuria mafunzo mbalimbali.    ---------- Sent from my Nokia phone  ------Original message------ From: Abdalah Hamis To: Date: Thursday, July 31, 2014 11:05:20 PM GMT-0700 Subject: [wanabidii] NANI HASA ALIWAINGIZA WAKURYA WENGI JESHINI?    NA MOBHARE MATINYI  Naomba niwapatie ukweli ninaoujua kwa kutafiti na kufuatilia kuhusu uwepo  wa Wakurya wengi jeshini na madai kwamba Nyerere aliwapeleka jeshini - si  kwa kuwa mimi ni mkurya! La hasha! Kwanza niseme hivi, ni kweli kwamba Wakurya ni wengi sana jeshini  kulinganisha na makabila mengine ya Tanzania ingawa katika miaka ya  karibuni wamekuwawakipungua kutokana na sababu nyingi ambazo hapa si  mjadalawake.  NANI ALIWAINGIZA JESHINI 1. Wakurya waliingizwa jeshini kwa mara ya kwanza na Waingereza wakati wa  kuandaa jeshi la kikoloni ambapo ilipotokea vita ya pili ya dunia,  Waingereza walikwenda vijijini kwa Wakurya na kuwakamata amakuwahamasisha  vijana wao waingie jeshini ili kwenda kupigana. Baadhi yao waliporejea,  akiwemo Marehemu babu yangu mzaa mama na baba yangu mkubwa, walikataa  kuingia jeshini wakisema wana mali nyingi na wakaenda kuangalia ng'ombe  zao. Hawawalipigania nchini Burma huko Asia. Utamaduni huu wakuingia  jeshini ukaanzia hapo na kuendelea.  2. Kwa nini Waingereza waliwachukua Wakurya wengi kwenda jeshini? Ni kwa  sababu ya dhana kwamba makabila ya Waafrika yana vipaji tofauti na kwamba  ili kuwatawala Waafrika kwa urahisi, inabidi kuvitumia vipaji hivyo.  Mfano,Waingereza walisema kwamba ukitaka madaktari wengi watiifu na wapole  wachukue Wasukuma kwa sababu ya upole wao na utiifu na kweli tunao wengi  sana. Waingereza wakasema tena, wafanyakazi wazuri wa ndani ni Wanyasa -  kweli, wafanyakazi wa ndani wa balozi na maofisa ubalozi wa Uingereza hata  sasa hivi ni Wanyasa kwa sababu ya uaminifu wao. Walisema pia kwenye elimu  weka Wachaga na Wahaya na ni kweli hadi leo waliobobea shuleni zaidi nchini  na nani? Tunajua wote! Wakasema, kule Kenya, ukitaka wasomi chukua Wajaluo  na Uganda wakasema ukitaka wasomi chukua Waganda. Kwenye uaskari walisema  kwamba kwa Uganda chukua Walango, Waacholina ikibidi sana Wakakwa (kabila  la Idi Amin). Nchini Kenya walisemakwamba kwa askari bora uchukue Wakamba.  Kwa Tanganyika wakasema chukua Wakurya na ongeza Wangoni na Wahehe.  Wakaongeza zaidi na zaidi kwenye mpangilio wao. Ipo orodha ndefu.  Waingereza walifanya utafiti mzuri na walipoondoka walimwachia kila  kiongozi wa Afrika (makolonini) matokeo ya utafiti wao ingawa akina Nyerere  hawakuzifuata.  MATOKEO YA SERA YA WAINGEREZA 3. Nini matokeo ya mpangilio huu wa Waingereza? Kule Uganda karibu  wanajeshi wote wakati Amin anaichukua nchi (walikuwa 8,000 hivi), walikuwa  Walango, Waacholi na Wakakwa lakini kwa kuhofia kupinduliwa akaanza  kuwauaWaacholi na Walango na kuwajaza Wakakwa na baadaye akawaweka mpaka  Wazaire na Wanubi wa Sudankusini na kaskazini mwa Uganda. Kule Kenya hadi  kesho, majeshi ya Kenya yamejaa Wakamba na kwa mnaofuatilia mtamkumbuka  Jenerali Muringe. Kwa kuwa Wakikuyu wamekuwa wakishika dola, Wakamba  waliminywa kwenye vyeo vya chini lakini wamejaa majeshini Kenya kupita  kiasi, hasa kutokana na umaskini wa nchi yao ya Ukambani ambayo ni kame pia.  NYERERE KUUNDA JWTZ 1964 4. Kwa Tanganyika Wakurya walijaa jeshini mno wakati tunapata uhuru kiasi  kwambaNyerere akasema hili ni tatizo.Alipovunja Kings African Rifles na  kuunda JWTZ baada ya maasi ya 1964, Nyerere aliamua kuweka sera kimya kimya  kwamba jeshi hili litakuwa na watu wa makabila yote. Ilikuwa kazi ngumu  kwake kwa kuwa waliokuwawanakuja kujiandikisha kwa wingi walikuwa ni  Wakurya zaidi kutokana na utamaduni wa kawaida wa Wakurya wa kupenda  kupigana, vita, ukakamavu, umwamba, n.k. Wakurya, kama Wakamba,Waacholi,  Walango, na Wakakwa waliitwa na Waingereza "Marshal Tribes" -yaani makabila  ya wapiganaji. Hata hivyo, Nyerere alifanikiwa kuwapunguza mno lakini bado  alibakia nao wengi kutokana na utamaduni, historia na ukweli wa  mambo,kwamba ukitaka askari mzuri chukua anayependa vita, siyo mtu mwoga.  Kama si Nyerere, jeshi lingekuwa wakurya watupu, siyo wakurya wengi, bali  wao wenyewe kwa hata 90%.  WAKURYA NA NYERERE 5. Wakurya hawakuwa na urafiki wowote na Nyerere kama watu wanavyodhani  kutokana na fikra za Kiafrika kwamba kilakitu kina nguvu za siri nyuma  yake, iwe baraka za Mungu, rushwa, udini, mapenzi, ukabila, uchawi, fitna,  mkosi, n.k. Mwafrika haamini kwamba kitu kinaweza kutokea kwa sababu zake  chenyewe bali mpaka kuwe na mtu mwingine anayekifanya kitokee. Kati ya watu  waliotaka kumpindua Nyererekwenye miaka ya 1960 mwishoni, kwa mnaofuatilia,  walikuwepo akina Chacha(nahifadhi jina lake kamili), na kutokana na tabia  ya Wakurya kumtukana Nyerere alipokwenda ziarani Tarime, aliamua kuacha  kufanya ziara huko. Si hivyo tu, Nyerere alikwepa hatakuwapa nafasi za juu  Wakurya na mkurya pekee aliyewahi kushika uwaziri katika miaka 25 ya  Nyerere ni Bhoke Munanka ambaye walikorofishana hata hivyo (waziri pekee  aliyemwambia kwamba huu ujamaa wako utaumiza watu na hakuna anayeutaka).  Kamamjuavyo, Munanka alikuwa mfanyabiashara mkubwa katikati ya ujamaa.  6. Aidha, Rais Nyerere hakuwahi kumteua mkurya kuwa mkuu wa majeshi wala  msaidizi wala chochote cha juu ingawa ukiongea na watuwanakwambia mambo  mengine kabisa. Mkuu wa kwanza wa JWTZ alikuwa Sarakikya kutoka Meru; akaja  Twalipo kutoka Songea; akajaMusuguli kutoka Bunda (si mkurya). Rais Mwinyi  ndiye aliyekuwa wa kwanza kumteua mkurya kuwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali  Kyaro, na baadaye Mkapa akamteua Jenerali Waitara. Hata kwenyeVita ya  Uganda, Nyerere hakumpa mkurya kuongoza vita ile ingawa kwenye makamanda wa  chini Wakurya walijazana kama utitiri, achilia mbali askari wa kawaida. Ni  Mwita Marwa pekee ndiye aliyekuwa kwenye makamanda wa kuongoza brigedia,  lakini wengine wote walibanwa pembeni........Nyerere hakutaka taabu baadaye.  WAKURYA KUPENDA VITA/JESHI 7. Kwa wenye kumbukumbu na wanaofuatilia, tulipovamiwa na Amin Oktoba 31,  1978, na baadaye Nyerere kutangaza vita, serikali ilitoa mwito kwa wananchi  kujiunga na mgambo/jeshi kwa hiari. Nafasi zilikuwa 2,000 kwa kilamkoa.  Wakurya walilaani kitendo hicho cha kuweka ukomo wa idadi na wakatuma  wajumbe kwenda kulalamika kwa Nyerere kwamba idadi ya 2,000 ni ndogo mno  kwa mkoa wa mashujaa. Nyerere akasema hawezi kuondoa ukomo huo. Wakatuma  tena ujumbe wa pili, na Nyerere akashauriwa na makamanda wake kwamba kwa  kuwa mikoa mingine imeshindwa hata kufikisha 500 tu, basi ni heri Wakurya  waachiwe waje tu. Nyerere akasema kwamba basi anaruhusu nafasi 4,000 kwa  mkoa wa Mara. Hii imeandikwa kwenye vitabu na waandishi wasiokuwa  Watanzania.  8. Wazee wa mkoa wa Mara walikerwa mno na uamuzi waNyerere wa kuweka ukomo  mwingine wa 4,000 na wakaamua kwamba dawa ni rahisi sana, kwamba vijana wao  waende kwenye mikoa ambayo ilikuwa imeshindwa kufikisha idadi ya 2,000 ya  awali. Huu si utani. Kaka yangu alikwenda Morogoro. Baba yangu mkubwa  alikwenda Moshi na ndugu yangu mwingine alikwenda Usukumani na wote  wakaenda vitani na wakarejea kwa ushindi na furaha. Wote wapo hai hadi leo  na kaka yangu huyu aliingia Magereza baadaye. Kwa kifupi, Nyerere aliwabana  Wakurya wasiendevitani kwa wingi kama walivyotaka. Mjomba wangu Nyaronyo  Kicheere alipata medani ya vita pia kwa kujitolea kwenda vitani akitokea  JKT - yumo humuukumbini muulizeni.  KWA NINI WAKIMBILIE JESHINI 9. Mimi binafsi, wakati ninamaliza kidato cha sita na huku nikiwa  nimefaulu, uamuzi wangu ulikuwa kwenda JWTZ kwanza na mambo mengine yafuate  baadaye. Kama si wazee wangu kunikatalia, leo hii ningekuwa kwenye  magwanda. Naomba Kivuyo na LKK mniambie, mimi niliyezaliwa mjini, nikakulia  Dar es Salaam, simjuiNyerere wala hanijui, ninahusika vipi na Nyerere  wakati aliacha urais nikiwa sijafika miaka 18? Nyerere ametoka kwenye urais  mwaka 1985 lakini miaka 27 baadaye bado Wakurya wamejaa jeshini ingawa  wananyanyaswa kutokana na maneno ya kipuuzi kama haya, je, Nyerere  anahusika vipi na kuwepo kwao? Mkurya wa miaka 20 leo, aliyeko jeshini,  anahusika vipi na Nyerere? Kwa ufupi ni hivi ........... Wakurya  tunalipenda jeshi, basi! Nenda hata Kenya utawakuta jeshini, mpaka hapa  Marekani wamo jeshini. Je, Nyerere aliitawala Kenya na Marekani?  10. Pili, kutokana na maendeleo kuwa nyuma sana mkoani Mara, sehemu pekee  ya ajira ilikuwa jeshini kwa miaka mingi hadi walipoanza kuchimba dhahabu  kwa wingi kule Nyamongo,na kuuza ng'ombe kwa magendo nchini Kenya. Wilaya  ya Tarime, wakati ule wa Nyerere, ilikuwa kama sehemu ya Kenya kwani  magharibi ilizibwa na Ziwa Viktoria, kusini na mbuga ya Serengeti, na kuja  Mwanza kulikuwa na mto usiokuwa nadaraja (Mwinyi alilijenga baadaye), kule  mashariki na kaskazini ilikuwa nchi ya Kenya. Nyerere hakutaka hatakufanya  ziara tu, achilia mbalikujenga walau shule moja. Hivyo, jeshi likawa kama  kimbilio la ajira lakini hii ikiwa ni baada ya kuangalia kwanza hulka na  silka ya Wakurya kwenye masuala ya kupigana/jeshi/ushujaa, n.k.  Ndugu zanguni Kivuyo na LKK, siwalaumu kwa kudhani hivyo kwa kuwa haya  maneno yako hivyo lakini kama nilivyosema, ndivyo Waafrika tulivyo.  Ushahidi ulioponi kwamba Nyerere hakuelewana na Wakurya hata mara moja na  aliwabana wasiingie jeshini lakini akafika mahali akashindwa. Ushahidi ni  wa kutosha na mkitaka nitawapa kwenye barua pepe zenu binafsi kwa kuwa hapa  si vema kuyataja majina ya watu bila vibali vyao.  Wakurya tuna vitu vitano tunavyovipenda sana: Kupigana, familia, ng'ombe,  ukweli na utaifa. Ni fahari kubwa kwa mkurya kuingia jeshini, fahari kubwa  mno; wanangu madume wote wawili, mmoja miaka 9 na mwingine 6, wako hapa  Marekani lakini wanapenda kuvaa nguo za jeshi na kucheza na matoi ya  vifaru, ndege za jeshi, n.k. Jeshi liko damuni kwa Wakurya!  CHANZO: MOBHARE MATINYI, na MHADHIRI MWANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES  SALAAM  --  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com  Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma  Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifiesthat you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. ---  You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout. --  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com  Kujiondoa Tuma Email kwenda  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma  Disclaimer: Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines. ---  You received this message because you are subscribed to the GoogleGroups "Wanabidii" group. To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com. For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
  --
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Yourcontinued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups"Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment