Thursday, 1 May 2014

Re: [wanabidii] VIONGOZI WA CHADEMA MEATU WAHAMIA CCM

Mama Nkya
Naungana na wewe kuwa upinzani wenye nguvu ni chachu ya maendeleo. Ila sikubaliani kuwa mtu kuhama chama ni usaliti au kutumiwa au alipenyezwa toka awali ili kudhoofisha nguvu ya umma.Kwanza tukumbuke kuwa hao viongozi wa upinzani karibu wote walikuwa CCM na walihama na kujiunga na upinzani kwa hiyari yao uku wakisukumwa na utashi wa kuleta mabadiliko anuwai. Je na hawa nao ni wasaliti? Au wanatumiwa? Na wanatumiwa na nani? Ni nguvu gani ya uma inayodhoofishwa?
Kwa upande mwingine lazima tukubali pia ndani ya upinzani kuna udhaifu mkubwa sana,haiwezekani kila siku kunazuka swala la usaliti na watu kutumiwa na chama tawala. Ukisema kuwa fulani ni msaliti na anatumiwa na chama tawala ni wazi kuwa unakiri kuwa ndani ya taasisi yako kuna udhaifu mkubwa unaotoa mwanya kwa mtu kupenyeza sumu ya usaliti na kikivuruga chama. Ingekuwa jambo la busara kama mtu kaamua kuhamia chama kingine kumwacha aende na uku mkiendelea na mambo mengine kwani huo ni uhuru wa kikatiba na ameutumia ipasavyo.

Magere  J.

On Apr 24, 2014 6:48 PM, "MABADILIKO CHADEMA" <mabadilikochadema@gmail.com> wrote:

Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema wilaya ya Meatu Kimwaga Jackson Ndibo akirudisha vitu vya Chadema zikiwemo kadi, bendera na katiba kwa viongozi wa CCM baada ya kurudi rasmi.

Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga alikabidhi kadi ya CCM kwa viongozi wa Chadema Meatu waliorudi CCM.

Mwenyekiti wa Vijana mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga alihutubia wakazi wa wilaya ya Meatu na kuwahakikishia wananchi hao CCM imejipanga kuendelea kuleta maendeleo ya nchini.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment