Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika shida zake, Sheikh Sharrif ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Sheikh Sharrif aliye matatizoni, kufunga safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na Mogadishu.
Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.
Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif Ahmed.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.
Wikiendi Njema.
Maggid.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment