Saturday, 28 September 2013

[wanabidii] RE: [Mabadiliko] Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..

Mtaalamu wangu Maggid,
 
Rais wa Somalia alishabadilishwa, siyo Sheikh Shariff tena. Itakumbukwa kuwa walifanya uchaguzi maalum bungeni Septemba 10, 2012 na kumchagua Hassan Sheikh Mohamed.
 
Lakini ujumbe wako umefika na unaeleweka.
 
Matinyi.
 

Date: Sat, 28 Sep 2013 06:36:06 +0300
Subject: [Mabadiliko] Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..
From: mjengwamaggid@gmail.com
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com; wanabidii@googlegroups.com



Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika shida zake, Sheikh Sharrif ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Sheikh Sharrif aliye matatizoni, kufunga safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na Mogadishu.

Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.

Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.

Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif Ahmed.

Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.

Wikiendi Njema.
Maggid.
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment