Nimenangalia kazi inayofanywa na hii kampuni ya Kijerumani ya kujenga barabara za mwendo kasi lakini nimeshindwa kupata majibu yafuatayo:
1. Wasafiri wataingiaje na kuondoka kituoni cha mabasi? Itabidi waruke barabara za mwendo kazi, barabara za magari ya kawaida na barabara za baiskeli na waenda kwa miguu. Swali usalama wao uko wapi hapa? na kuvuka kwao hakutafanya magari yasimame ili wasafiri wanaoingia kituoni waingie na kutoka?. Je hii haitafanya ile nia ya kuwa na usafiri wa mwendo kasi kuwa mwendo polepole na kusababisha ajali?
2. Barabara za kuingia na kutoka mjini zimejengwa kupitisha gari moja tu. Je itakuwaje gari likiharibika katikati ya njia. Litavutwa mpaka kituoni au litatengenezwa papo kwa hapo? Je hii haitasababisha mwendo kasi kuwa mwendo polepole?
3. Sijaelewa magari ya mwendo kasi yatakuwa juu usawa wa kituo ili wanaoingia na kutoka iwe rahisi kwao?.
4. Je walemavu na watumia baiskeli za magurudumu na mikongojo wamefikiriwa vipi kwenye mpango mzima?
Nitashukuru kuelimishwa kwani si ajabu tuko wengi tunajiuliza maswali haya lakini hatuna majibu
Shukrani
Herment A. Mrema

0 comments:
Post a Comment