Friday, 27 September 2013

Re: [wanabidii] 'Taja jina la bibi mzaa mama wa Yesu Kristu!'

La kuongezea ndugu Rupia, ni kuwa Jeshi letu la polisi nalo
lijiangalia kwa macho manne. Hizi ni kweli polisi hawa wanaobambia
raia wema kesi, watapata ushirikiano uliodhabiti kutoka kwa hao raia,
nadahani jibu unalo mwenyewe, Uhamiaji wetu wanaotegemea rushwa toka
kwa wahamiaji haramu ndio waendeshe maisha yao watatusaidia kuwa
salaama.

Nina rafiki yangu mmoja amelibahatika kupata kazi uhamiaji yupo
airport Dsm, hana cheo chochote ndani ya miaka 2 alikuwa na GX 100
PAMOJA BODABODA za kumwaga huwa namuuliza unapata wapi pesa yote hiyo
anasema we achaa anauhakika wa kupata zaidi ya mshahara wake kwa wiki,
huyu naye anaweza kutulinda dhidi hawa wahamiaji haramu

On 9/27/13, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
> Ndugu Rupia naungana na wewe kwa asilimia 100 lakini tuwe tunatafuta
> chanzo cha haya mambo tatizo lake ni nini na kwa sababu gani wanafanya
> hayo wanayoyafanya na hapo ndipo tutaweza kuyadhibiti, binadamu huwa
> hatari zaidi ya simba pale anapokwazwa na jambo halafu akapuuzwa, sasa
> tujaribu kuuliza kwanini wanafanya haya wanayoyafanya leo, wanafanya
> unyama na ushetania ambao unatakiwa kulaaniwa na kila binadamu mwenye
> akili timamu. isipokuwa kabla ya kulaani tutafute sababu ya wao
> kufanya hivyo. huenda ikaleta ufumbuzi wa yanayotokea leo
>
> On 9/27/13, Joseph Beda Rupia <rupia.joseph@gmail.com> wrote:
>> RAI, Alhamisi, Septemba 26, 2013; Na Joe Beda
>> <http://www.rai.co.tz/index.php?option=com_mailto&tmpl=component&link=542b9fededd1937d0cc36dbe3aa4f12ba14de6d5><http://www.rai.co.tz/index.php?view=article&catid=28%3Ajamii&id=501%3Ataja-jina-la-bibi-mzaa-mama-wa-yesu-kristu&tmpl=component&print=1&layout=default&page=&option=com_content&Itemid=39><http://www.rai.co.tz/index.php?view=article&catid=28%3Ajamii&id=501%3Ataja-jina-la-bibi-mzaa-mama-wa-yesu-kristu&format=pdf&option=com_content&Itemid=39>
>>
>> MIAKA zaidi ya 10 iliyopita nilisoma katuni moja kwenye gazeti la SANI
>> ambayo huenda ndiyo katuni yangu bora niliyowahi kuiona kwani
>> ilinifikirisha na kunichekesha kuliko nyingine nyingi. Kipindi hicho
>> kulikuwa na vuguvugu kubwa la haki za mtoto na hasa mtoto wa kike, huku
>> kukiwa na wimbi la walimu kadhaa wa kiume kushitakiwa mahakamani kwa kuwa
>> na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa kike.
>>
>> Sijui kama suala hilo kwa sasa limekwisha, limepungua au limeacha
>> kuripotiwa kwa sababu ya kupitwa na wakati, lakini inavyoonekana hali kwa
>> sasa si sawa na kipindi kile.
>>
>> Katuni ile ilimwonyesha mtoto wa kike akiwa amelala chini huku mwalimu wa
>> kiume akimtandika bakora mfululizo na kumuuliza swali hili: "Nakuuliza,
>> Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 9 Desemba mwaka 1961, ilikuwa juma
>> ngapi?"
>>
>> Mchoraji wa katuni ile aliiwekea maandishi ya utangulizi yaliyosemeka;
>> 'ukiona mwalimu anauliza swali hili, ujue ana lake jambo!' Hakika
>> lilikuwapo jambo kati ya binti huyo, mwalimu, na swali lile la 'kizushi'.
>>
>> Naam, nilicheka. Lakini nikajiuliza iwapo swali hilo ningeulizwa mimi
>> ningekuwa na jibu? Tarehe ya Uhuru wa Tanganyika na hata Uhuru wa nchi
>> nyingine kadhaa za Afrika tumekuwa tukikaririshwa miaka nenda rudi,
>> lakini
>> siku haswa ya tukio! Hapana.
>>
>> Kumbukumbu za katuni hiyo zikanirudia majuzi baada ya watu wanaoaminika
>> kuwa ni magaidi (wana mgambo) wa kundi la Al-Shaabab kuvamia mlolongo wa
>> maduka ya Westgate Mall jijini Nairobi.
>>
>> Mashuhuda walionusurika kuuawa kwenye tukio hilo, wameviambia vyombo
>> mbalimbali vya habari kwamba magaidi hao walikuwa wakijitahidi
>> kuwatenganisha 'walengwa' wao na 'wenzao' kwa kuwauliza jina la mama wa
>> Mtume Mohammad (SAW)!
>>
>> Sina uhakika na ugumu au wepesi wa swali hilo kwa 'muumini' mzuri, lakini
>> nilicho na uhakika nacho ni kwamba, hata swali jepesi kama 'jina lako
>> nani'
>> unaweza kushindwa kulijibu kwa wakati ukiwa umeelekezewa mtutu wa bunduki
>> na mtu asiye na masihara hata kidogo!
>>
>> Mtu aliyeamua kwamba siku hiyo ndiyo siku yake ya kufa, labda itokee
>> bahati
>> mbaya, ni mtu hatari sana. Fikiria, tayari umeshuhudia watu wanne au
>> watano
>> wakipigwa risasi mbele yako baada ya kuulizwa swali, inafika zamu yako na
>> kuulizwa 'jina lako nani?' hakika unaweza kushindwa kujibu!
>>
>> Nikafikiria hivi kuna 'waamini' wenzangu wangapi wanaoweza kuulizwa
>> ghafla
>> na kutaja jina la bibi yake na Yesu mzaa mama? Tena hilo linaweza kuwa
>> jepesi, lakini ni nani analijua jina la bibi yake Yesu mzaa baba mlezi?
>>
>> Kwa kumbukumbu za haraka, nikakumbuka jina la Anna (Mtakatifu Anna) kuwa
>> ndilo jina la mama yake Bikira Maria (bibi yake Yesu upande wa mama),
>> lakini upande wa baba mlezi! Hatari.
>>
>> Sasa hapo hakukuwa na shinikizo lolote, je ningekuwa nimeelekezewa
>> bunduki?
>> Hakika nikaikumbuka ile katuni kwamba ukiona mtu anauliza swali kwa
>> mtindo
>> huo, ujue ana lake jambo.
>>
>> Nikawaza kuwa kama ingetokea bahati mbaya nikawa mmoja wa waathirika wa
>> tukio la Nairobi, swali la haraka ambalo ningewajibu jamaa wale bila
>> kusita
>> ni kama wangeniuliza jina la mke (mkubwa) wa Mtume (SAW).
>>
>> Haya mambo nikuomba Mungu yasikutokee. Ni mambo ya kusikitisha sana na
>> hata
>> kwa fikra za kawaida unashindwa kuelewa chuki hizi zinapandikizwa
>> miongoni
>> mwa binadamu kwa lengo gani?
>>
>> Swali gumu zaidi ni jinsi gani ya kuzuia matukio ya kishenzi kama haya
>> kutokea katika dunia hii ya utandawazi.
>>
>> Jeshi la Polisi nchini limesema kwamba liko tayari, eti limejiandaa
>> kuyakabili matukio kama haya; ni jambo la kushukuru kama kweli tuko
>> tayari,
>> lakini kikubwa ni kuyakinga yasitokee.
>>
>> Ni hapo ndipo Watanzania wote tunapaswa kushirikiana. Ulinzi na usalama
>> wetu unaanzia kwetu wenyewe, kwa kutoa taarifa kwa viongozi kuhusu
>> mienendo
>> ya kutia shaka ya kundi la watu au mtu yeyote unayemfahamu au
>> usiyemfahamu.
>>
>> Ipo tabia yetu ya kutowaamini watendaji kadhaa serikalini kwamba unaweza
>> kutoa taarifa, kumbe unayemtaarifu anahusika au kuhusiana na kundi hilo
>> matokeo yake usalama wako ukawa hatarini.
>>
>> Sasa ushauri wangu katika jambo hilo ni kwamba, mtafute kiongozi
>> unayemwamini hata wa chama cha upinzani, mtaarifu suala hilo na ninaamini
>> yeye hataogopa kulipeleka serikalini; au basi mdokezee mwandishi wa
>> habari
>> unayemwamini kwani nao katika tasnia yao ni 'risk takers'.
>>
>> Lakini serikali nayo inapaswa kuwa makini. Iweke mtandao mpana wa
>> kugundua
>> uingizwaji nchini wa 'fedha chafu' au hata kama ni safi, lakini
>> zinapoingizwa kwa wingi kwa kundi au mtu asiyeaminika, ni vyema zikazuiwa
>> hadi itakapofahamika kazi ya fedha hizo nchini ni ipi hasa.
>>
>> Ni wazi maandalizi ya shambulio kama hili la Nairobi yaligharimu fedha
>> nyingi. Sasa. Fedha hizo ziliingizwaje nchini? Zilipitia benki gani?
>> Zilikwenda kwa nani?
>>
>> Tusiruhusu fedha chafu kufika mikononi mwa watu ambao mienendo yao inatia
>> shaka.
>>
>> Nimalizie kwa kuwakumbusha 'wazee' wenzangu muziki mmoja wa miaka ya 1970
>> uliokuwa na maneno 'wanyama wabaya maana yake, sio simba wala si tembo,
>> ni
>> wanadamu wenye choyo…'
>>
>> *Nawasilisha
>> 0684 419 506*
>>
>> --
>> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>> ---
>> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
>> "Wanabidii" group.
>> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
>> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment