Mrema
Nimependa sana hoja yako hii hapa Jukwaani. Sio kwa sababu tu inagusa maeneo ya kazi yangu bali pili umuhimu wa maswali yenyewe kwa jamii na watumiaji wengi wanaotegemewa kutumia usafiri huu wa mabasi yaendayo kasi. Mimi siyo msemaji wa DART lakini kwa kuwa hapa Jukwaani wapo basi watasaidia kuelewesha zaidi.
Nafahamu wengine hawataki kuonekana hapa lakini basi niwaombe watumie njia yoyote ili watanzania hawa na hasa huyu aliyeuliza maswali haya muhimu aweze kufahamu
Nichangie kidogo kwa kile ninachokielewa kuhusu barabara hizi:-
1. Zipo namna mbili za wasafiri kuingia kituoni. Moja ni kwa vile vituo vikuu ambavyo wasafiri wamejengewa njia za juu kutokea sehemu za pembeni mwa barabara na kuingia katikati ya kituo kama inavyooneshwa katika mojawapo ya picha alizoambatanisha hapa bwana Mwasaga. Njia ya pili ni ile ya kutumia Zebra crossing ambazo zitakuwa zinapita kwa barabara za kawaida hadi kwenye kituo husika ambacho kiko katikati ya barabara za kawaida. la muhimu hapa ni kwamba barabara hizi bado zitaongozwa na sheria na kanuni za barabara zote nchini.
2. Kama gari litaharibika angalia vizuri kila kituo kina njia mbili kila upande. Hata hivyo vituo hivi viko karibu kiasi kwamba kama inatokea shida kwa gari moja kulipeleka kwenye kituo cha karibu kwenye njia ya pili ni rahisi. Sehemu nyingine zimeachiwa central bays kwa kusudi kama hilo japokuwa katika uhandisi wa siku hizi sehemu kama hizo zinatakiwa kuwa na umbali usiopungua kilomita 3 ili hata kama ndege zikipata tatizo ziweze kutua au pia kutumiwa na chopa kwa matumizi ya dharula kama kupambana na magaidi nk. Huu ni mtazamo wa kisasa mno kwa siku hizi.
3. Kwa kawaida vituo hivi vimejengwa kwa namna ambayo abiria ataingia akiwa usawa na mlango (raised platform) wa kuingia kwenye gari husika. Kama utakumbuka enzi hizo kukiwa na magari ya UDA ya Ikarus yalikuwa na vitu kama hivi yaani yameinuka. Kwa hiyo magari haya yanatakiwa kushusha tu kwenye kituo husika ambacho kimejengwa kwa kusudi husika.
4. Walemavu wamefikiriwa sana katika mpango huu. Kwanza kwenye njia za juu ili kuingia kituoni hakuna ngazi yote imejengwa kwa kushuka tu kama unateleza lakini ambayo ni salama kutumiwa na waenda kwa miguu pia bila usumbufu wenyewe wanaita Ramp. Aidha kwenye kuingia kwenye vitua vya kati angalia kwa makini sehemu za kuingia kwenye kituo zote zimejengwa kwa mfumo wa kuteleza (ramp). Kuingia kwenye magari hakuna tatizo kwa kuwa kituo kimeinuliwa kulingana na usawa wa mlango na kuwezesha wasafiri kuingia bila kulazimika kupanda ngazi. Itapendeza tuwape muda tuone nini kitatokea.
Ushauri wangu kwa wale waliopewa hili jukumu la kujenga wafanye haraka ili hatimae tuone nini hasa hiki kinachojengwa.
K.E.M.S.
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 27 September 2013, 14:15
Subject: Re: [wanabidii] Hizi zitakuwa Barabara za Mwendo Kasi au Mwendo Balaa?
Mrema
Kwanza kabla hujapata msaada wa kiufundi kutoka DART(http://www.dart.go.tz) nikujulishe kwamba hizi siyo barabara za mwendokasi bali ni barabara kwa ajili ya Mabasi yaendayo haraka (Rapid Transit is not Speedy Transit). 2013/9/27 Herment Mrema <hmrema11@hotmail.com>
--Nimenangalia kazi inayofanywa na hii kampuni ya Kijerumani ya kujenga barabara za mwendo kasi lakini nimeshindwa kupata majibu yafuatayo:
1. Wasafiri wataingiaje na kuondoka kituoni cha mabasi? Itabidi waruke barabara za mwendo kazi, barabara za magari ya kawaida na barabara za baiskeli na waenda kwa miguu. Swali usalama wao uko wapi hapa? na kuvuka kwao hakutafanya magari yasimame ili wasafiri wanaoingia kituoni waingie na kutoka?. Je hii haitafanya ile nia ya kuwa na usafiri wa mwendo kasi kuwa mwendo polepole na kusababisha ajali?
2. Barabara za kuingia na kutoka mjini zimejengwa kupitisha gari moja tu. Je itakuwaje gari likiharibika katikati ya njia. Litavutwa mpaka kituoni au litatengenezwa papo kwa hapo? Je hii haitasababisha mwendo kasi kuwa mwendo polepole?
3. Sijaelewa magari ya mwendo kasi yatakuwa juu usawa wa kituo ili wanaoingia na kutoka iwe rahisi kwao?.
4. Je walemavu na watumia baiskeli za magurudumu na mikongojo wamefikiriwa vipi kwenye mpango mzima?
Nitashukuru kuelimishwa kwani si ajabu tuko wengi tunajiuliza maswali haya lakini hatuna majibu
Shukrani
Herment A. Mrema
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment