Tuesday, 2 July 2013

Re: [wanabidii] JWTZ Yakanusha tuhuma za kuhusika na ubakaji Mtwara

Sisi wengine ambao Mungu ametujalia kuona uadilifu aliokuwa akiujenga Mwal Nyerere kwenye jeshi letu bado mpaka hivi juzi  ulikuwa mioyoni mwetu. Lakini Wanajeshi wetu ebu rudini nyuma mjiangalie upya na kujitathimini kwa mapana na marefu. Chombo ambacho kinatakiwa kuwa imara ktk kumhakikishia mtanzania usalama wake ni JESHI la WANANCHI. Lakini jeshi la wananchi nadhani tunaanza kuingiwa na hofu wengi wa sisi wananchi. Inatupa hofu kubwa tukiona hata jeshi litakapoanza kutuhumiwa kama jeshi la polisi. Mimi kama mwananchi wa kawaida ningeshauri jeshi lijitathimini kwa undani. Msione aibu kulaumiwa kwa kufanya kosa bali kuwa na Ujasili wa kujitathimini na kurejesha imani kwa watanzania. Ni vyema mkatengana na kuhusishwa na kutumika kisiasa. Kinyume na hapo sio lazima itangazwe kuwa nchi imefika pabaya. Itakuwa busara endapo jeshi mtatambua kuwa kiwe ni chombo cha mwisho kabisa kunyang'anya usalama wa mtanzania. Watu sio wa Mtwara tu bali nchi nzima wana macho wanaona, wana akili wanafikiri na kutofautisha baya na zuri mnalofanya hivyo haihitaji kuambiwa na vyombo vya habari. To maintain your credibility kama jeshi come forward tell the Tanzanian say a Big SORRY. Kwenye siasa watu wameshaumia na sasa inapokuja kwenye jeshi watu wanapoteza matumaini. Hakuna kitu kigumu ktk maisha watu kupoteza matumaini ya usalama wao wakiwa nchini kwao.
 
Solomon William Msomba-MSc
Leader,Crop Improvement Programme
Tea Research Institute of Tanzania (TRIT)
P.O.Box 2177
Dar-Es-Salaam
Tanzania
+255 784 596 649
+255 787 596 649
E-mail: msomba2000@yahoo.com
smsomba@trit.or.tz
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, July 1, 2013 3:53 PM
Subject: [wanabidii] JWTZ Yakanusha tuhuma za kuhusika na ubakaji Mtwara

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea taarifa kwamba waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara kwenda kumhoji msichana mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa JWTZ.

JWTZ  linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli  wowote zaidi  ya kuwa ni za upotoshaji.

Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu hawawezi  kuvifanya. 
Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.

Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Tunasikitika sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu ya  kulichafua JWTZ lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

SLP 92023, Simu: 0764 742161

mailto:Email%3Aulinzimagazine@yahoo.co.uk


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment