Monday, 29 July 2013

Re: [wanabidii] MTWARA, VIJANA WANNE WATEKWA WAPELEKWA KAMBI NDOGO YA JESHI YA UMOJA KWA MATESO

Muda si mrefu IGP Mwema amenijulisha kuwa ofisi yake imeingilia kati. Wale vijana wanne wameachiwa huru mchana huu baada ya kuhojiwa na RCO. Hawakupelekwa mahakamani. 

Namuomba mungu hivi sasa kila atakayekamatwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama watusaidie haraka, watimize wajibu wao.

Nimeongea na mmoja wa vijana hao hivi punde, wanashukuru kwa juhudi za kuwafuatilia, kijana huyo anasema kwamba hiyo jana walipofikishwa kambi ya UMOJA walikaa muda mfupi kisha wakapelekwa kambi ya NALIENDELE, anasema hapo Naliendele wamepigishwa PUSH UP usiku kucha, anasema askari jeshi wa NALIENDELE tangu jana usiku walikuwa wakiwahoji kuwa wao(vijana hawa wanne) ni ndugu za nani na kwamba kwa nini wakubwa wamezuia wasipigwe? Kijana huyu anasema yeye na wenzake hawajui kwa nini waliulizwa vile. 

Wanasema pale kambini wamewakuta wananchi wengine watatu ambao walikuwa wakipigwa usiku kucha na hawawajui majina. Vijana hawa wamekoswakoswa kubambikiziwa kesi kama kina Mketo walivyofanywa, hii ya sasa IGP ametimiza wajibu wake. 

Binafsi nitaendelea kupiga kelele dhidi ya mateso wanayopewa raia mahali popote, bila kujali nitamgusa nani na bila kujali nitajiweka hatarini kuwindwa kiasi gani. 

Nachojua ni kuwa, ifikapo mwaka 2100, watesaji na wateswaji wote watakuwa hawapo dunia hii. Na kama kitu cha mwisho binadamu anachokiogopa ni kifo, na kifo chenyewe hata siku moja hakina uzoefu, kwa nini tuwaogope watishiao na kuua miili wakati na wao watakufa siku moja? 

Tuijenge nchi yetu, tupambane ndani ya nchi yetu, tudai haki za wanyonge bila kurudi nyuma. 

Nawashukuru wote ambao wamekuwa na mtizamo wa kweli wa kupigania haki za wanyonge mahali popote pale walipo.

2013/7/29 denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>

MGAMBA,

Usitegemee wazalendo wet wane mapungufu hayo. Kazi ya kwanza ya mzalendo yeyote ni kuuunga mkono serikali na rais wetu no matter what..............

Yet macho. Ukarimu hauanzii nyumbani

On 29 Jul 2013 11:57, "RICHARD MGAMBA" <rmgamba2000@yahoo.com> wrote:
Jeshi liko imara, tukichokozwa tutajibu. Kumbe huku nyumbani jeshi linafanya kazi ya IGP Mwema? Katiba inaruhusu jeshi kutumika katika matumizi kama ya Mtwara? Haya watu hawataki kujadili, ila wanashabikia kauli za hatari za kupigana na majirani zetu. Kaazi ipo.

From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, July 29, 2013 10:43 AM
Subject: [wanabidii] MTWARA, VIJANA WANNE WATEKWA WAPELEKWA KAMBI NDOGO YA JESHI YA UMOJA KWA MATESO

KONGAMANO LA AMANI UDSM LILILORUSHWA NA ITV LASABABISHA BALAA MTWARA, VIJANA WANNE WATEKWA WAPELEKWA KAMBI NDOGO YA JESHI YA UMOJA KWA MATESO.

Unaweza usiamini haya yanatokea Tanzania au yanatungwa.
Nimemaliza kuongea na Mashuhuda wanne sasa hivi ambao wao wamenusurika baada ya kuwa mita chache katika eneo la tukio.

Makundi mbalimbali ya wananchi yalikuwa yanafuatilia Kongamano pale Mtwara. Majira ya saa 11 jioni vijana waliokuwa kwenye Grocery iitwayo KWATELELA(Glocery hii inaangaliana na lango KUU la mamlaka ya Bandari Mtwara) walishangilia kwa nguvu kuunga mkono baadhi ya hoja zilizotolewa kwenye kongamano, karibu yao alikuwepo askari jeshi aliyevalia kiraia ila hawakujua hilo.

Kongamano lilipokaribia kuisha, askari jeshi yule aliwatolea bastola na kuwaweka chini ya ulinzi. Alipiga simu kuwaita wenzie na mara gari ya jeshi ilifika. Vijana wanne walichukuliwa muda huohuo na kupelekwa kwenye kambi ndogo ya jeshi ya UMOJA iliyopo Mtwara.

Hadi sasa vijana hao hawajaachiwa, na haijulikani hapo kambini wanafanywaje.

Nimejaribu kumpigia waziri Nchimbi na simu yake inaita tu, IGP pia simu zake zinaita tu, nimejaribu kuwatumia ujumbe mfupi. Nafuatilia pia majina ya vijana hao.

Nchi hii inaelekea mahali kubaya sana, utawala wa sheria na kujali haki za msingi za raia sasa umeshaporwa.

J. Mtatiro.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment