Wednesday, 31 July 2013

[wanabidii] RE: [Mabadiliko] Kero za Muungano - Zanzibar

Salmini,
 
Bado napitia nyaraka mbalimbali. Umeniwahi sana, labda nitajae hizi haraka haraka labda na wewe utaongezea au kuchangia:
 
  1. Mamlaka kamili (sovereignty) Bendera ya Taifa, pesa (currency), passport, wimbo wa Taifa, kiti UN, uanachama FIFA, uanachama moja kwa moja EAC na sio kupitia mgongo wa Tanzania
  2. Mafuta na gesi asilia: Wazanzibari wanataka suala hili lisiwe la muungano
  3. Kuongezeka na tafsiri ya mambo ya muungano: Mathalani, hawaridhiki na utendaji wa Baraza la mitihani, kuna strong reservation juu ya Baraza la mithani. Huu ni mfano tu.
  4. Ajira za wazanzibari katika taasisi za muungano: Wazanzibari hawapati ajira katika Taasisi hizi. Pia hawapewi nafasi za ubalozi, hapewi nafasi za kuongoza kama vile IGP, mkuu wa majeshi n.k 
  5. Uwezo wa Zanzibar kukopa nje: Hawana mamlaka ya kukopa katika taasisi za nje. Haoa wanahitaji mamlaka zaidi, wanataka sovereignty ya Zanzibar.
  6. Gawio la Zanzibar katika mali za bodi ya sarafu ya Afrika Mashariki (EACB)
  7. Utozwaji kodi mara mbili kwa wafanyabiashara wa Zanzibar
  8. Utaratibu wa Zanzibar kuwa na ushirikiano wa kimataifa na nchi za nje na mashirika ya kimataifa kwa lengo la kunufaika na fursa za kiuchumi
  9. Ushiriki wa Zanzibar katika jumuia na hatimaye shirikisho la Afrika Mashariki
  10. Rais wa Zanzibar kutokuwa automatically Makmu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hili lilitokana na na mabadiliko ya katiba ya 11.
  11. Wazanzibari wanaona wanaminywa na hivyo kukosa fursa za kiuchumi na uchumi wao haukuo ukilinganisha ni wa Bara
  12. Mgawanyo wa fedha za misaada (GBS)
 
Mfano: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wizara 26, ambazo kati ya hizo, sita ni za Muungano, hii ina maanisha kwamba, mambo yote, ambayo si ya Muungano, yanapangiwa bajeti ndani ya serikali hiyo. Hapo Wazanzibari wanahoji kutakuwa na usawa gani katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar?
 
Pia zipo kero kwa upande wa Bara. Hizo nazo ngoja tuzifanyie kazi.
 
Kwa kusema haya sina maana naunga mkono au natetea, la hasha najaribu tu kuona ni masuala gani ambayo Tume ya Warioba iliyapokea kutoka Zanzibar na labda ndio maana wanaona kuwa njia pekee ya ku-address kero hizi ni kwenda katika muundo wa serikali ya TATU. Vinginevyo, wanaodai serikali mbili watuambie, je serikali mbili zitaweza vipi ku-adress kero hizi? na je kama wameshindwa kuondoa kero hizi kwa miaka 49, je wanahitaji muda gani kumaliza kero hizi?
 
Selemani
 
Date: Wed, 31 Jul 2013 13:22:28 +0400
Subject: RE: [Mabadiliko] Muundo wa Muungano - Nukuu Hotuba ya Warioba
From: muhemasalmini@gmail.com
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Bw Selemani,
Kama itakupendeza,naomba unitumie hizo kero za muungano za wazanzibari nizipitie na mimi
Natanguliza shukrani
On Jul 31, 2013 9:19 AM, "Selemani Rehani" <srehani@hotmail.com> wrote:
Mike,
 
Asante sana. Hii niliyotuma ni hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Mzee Warioba. Inahitaji kujibidisha kidogo kutafuta mambo. Kwa mfano, nimejaribu kukusanya kero za Muungano kwa upande wa Zanzibar, ukizitazama kwa undani kero hizo there is no way unaweza kuziondoa kwa muundo huu wa sasa. Najaribu kuzi-summarize ili niweze ku-share. Swali la msingi: Kwa muundo huu wa serikali 2, utaweza vipi kuondoa kero hizi? hicho ndio najaribu kukijibu.
 
Unajua Mike, Muundo wetu wa sasa, una-provide a separate government of Zanzibar lakini  muundo huu hautoi for a separate government of Tanganyika. Hilo lilifanywa kwa nia njema kabisa, kuhofia Tanganyika kuonekana kuimeza Zanzibar kwa sababu ya udogo wake. Sasa serikali ya muungano wa Tanzania (ambapo Zanzibar ipo ndani) ndio imepewa mandate ya kushughulikia masuala ya Tanganyika ambayo si ya Muungano. Hii inaitwa dual role. Hii dual role ndio inaleta changamoto zote hizi, ndio inaleta mistrust na tension, kwani Wazanzibari wanashindwa kujua ni wakati gani Serikali ya Jamhuri ya Muungano ina act kama serikali ya Muunganoi na ni wakati gani inatekeleza masuala ambayo si ya muungano, yaani masuala yanayoihusu Tanganyika tu. Hii structure ni ngumu sana, huwezi kuondoa malalamiko. Kwa Wazanzibari waona serikali ya MUUNGANO inapendelea upande wa Bara kwa sababu ya hii double role, hawaitazami kama inawahusu na wao. Na wanaona ni janja yetu sisi wa Bara kujifunika katika kivuli cha serikali ya muungano ili tuamue mambo wenyewe.
 
Muundo wa serikali tatu unaweza kuondoa matatizo haya ila kama ulivyosema suala ni kukubaliana iweje? hivyo basi, CCM kupinga wazo hili ni kushindwa kuwa objective na kufanya analysis kwa kina.
 
Selemani
 
Date: Wed, 31 Jul 2013 11:24:24 +0300
Subject: Re: [Mabadiliko] Muundo wa Muungano - Nukuu Hotuba ya Warioba
From: ikwalala@gmail.com
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com

Seleman,

Well done! Mimi sikuwa hata na hiyo copy ya rasimu. Kumbe "waliopendekeza serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi yote"? See? watanzania (na hasa watanganyika) hawataridhika kama wataburuzwa tena na CCM kulazimisha muundo wa serikali mbili.

Kuhusu aina ya 'muundo' sahihi wa serikali tatu, hilo tuna weza kujadili japo wengi wamekwisha lisemea sana!

2013/7/31 Selemani Rehani <srehani@hotmail.com>
Matinyi,
 
How? fafanua tafadhali. make your your case.
 
Sele
 
From: matinyi@hotmail.com

To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: RE: [Mabadiliko] Muundo wa Muungano - Nukuu Hotuba ya Warioba
Date: Wed, 31 Jul 2013 07:43:33 +0000

Serikali tatu kwa mfumo mwingine inaweza ikawa wazo linalowezekana lakini kwa mfumo uliopendekezwa na akina Warioba ni tatizo kubwa zaidi kuliko yaliyopo sasa.
 
From: srehani@hotmail.com
To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
Subject: RE: [Mabadiliko] Muundo wa Muungano - Nukuu Hotuba ya Warioba
Date: Wed, 31 Jul 2013 06:16:40 +0000

 Wana mabadiliko,

"Suala la muundo wa Muungano ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote. Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwamba hadidu za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi ya wananchi walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maoni hayo. Licha ya kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana, Tume ilichambua sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.

 Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekeza Muungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na muungano wa mkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na uzito, kwa hiyo Tume ikaamua kutopendekeza muundo huo.

 Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zao zilikuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali hali iliona ni changamoto kubwa kuwa na Muungano wa Serikali Moja.

 Wananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchi wa Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekana wazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa lakini hakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume iliona kuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitiza muungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.

 Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali walikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi hili walipendekeza mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini ya Tume ilionyesha kwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa. (Nadhani huu ndio msimamo wa CCM).

Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundi yote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito. Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huo zilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbali za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza mfumo wa Serikali tatu. Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar."

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment