Wednesday, 31 July 2013

Re: [wanabidii] SUALA LA NGO KUFUNGUA KAMPUNI ZA MIKOPO

Wandugu,
Kwani ni vibaya NGOs kufanya biashara? Ninachodhani ni kwamba hawapaswi kugawana faida. Pengine si sahihi sana kudhani kuwa kazi ya NGOs ni kuomba omba to grants. Mathalan, NGO inayosaidia watoto yatima ikafika hatua ya kumiliki mashamba na kulima kibiashara, sehemu ya mazao hayo ikatoa chakula kwa hao watoto yatima na mishahara ya wafanyakazi, nadhani ni jambo la kupongezwa na hata kuigwa. Upepo wa ufadhili umebadilika.

Mikopo midogo midogo na ya kati mahali pengine ni njia bora zaidi ya kuwawezesha watu maskini kuliko kuwapatia bure. ikifanikiwa njia hii ni endelevu zaidi.
 
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, July 31, 2013 3:28 AM
Subject: Re: [wanabidii] SUALA LA NGO KUFUNGUA KAMPUNI ZA MIKOPO

Kukusanya kodi ni ndoto na hata ikikusanywa haitofika serikalini. Ni juzi tu nimesikia radioni wakiongea masuala ya vitunguu Singida kuwa havina bei-soko; kufunga rumbesa halafu wanunuzi kutoa fedha ndogo wao kutakiwa kulipa ushuru. Usipofunga rumbesa wanunuzi wafanya biashara hawaji kununua kwako na serikali imekataza rumbesa. Kulipa ushuru mara mbili etc. Kiongozi mmoja akasema, mtu kama anauza nyanya, vitunguu katika kikopo asitozwe ushuru bali wale ktk magunua. Hii ni pumba kwani-mswahili ataweka gunia jirani atakwenda kuchota kidogo kigogo kupanga nje au sokoni mpaka gunia liishe asilipe kodi. Wanaokusanya ushuru/kodi sokodi, mitaani, bandarini huko Rufiji-Nyamisati, Kisiju Mkuranga, Pwani-baharini Soko la samaki Bagamoyo, Lindi, Pangani etc au wale wa Mwenge kituo cha basi wanakusanya mamilioni au malaki kwa siku. Baada ya muda ana kitambi kikubwa, gari na kajenga nyumba. Wana vitabu zaidi ya kimoja fedha ndogo tu huingia serikalini. Hatuna uaminifu.

Wenzetu Ulaya hulipia kodi hata kwa kuuza peni. Sisi kila siku na mwezi huu mtukufu vyakula mpoaka usiku wa manane kinauza na hakuna kodi ilipwayo. Kila nyumba nje mitaa mingine inauza vyakula baba/mama ntilie hawatoi ushuru. Hata ukipita colleges mbali mbali za wasomi kuna canteen, maduka, wauza matunda na biashara mbalimbali unanunua hupewi risiti. hata kama kuna mashine ya kodi na computer anaingiza hapo ukiomba risiti anasongoa mdomo. Na colleges hizo utaona jirani tu ya duka lisilotoa risiti ipo school of commerce wanakufundisha masuala ya biashara na revenue. Na wala usishangae bongoland kuona school of medicine sewer line au septic tanks zinafurika zinatoa rojo ya kinyesi na maji machafu, mabweni ya wasomi kuna mataka na manholes zinazofurika na kuonyesha uchafu wa matambara na viroba vya valuer zinatoka humo. Yaani akilizetu zi za kawaida.

NGO kufungua biashara au kampuni za mikopo-hii ni ulaji maana baadhia ya NGO wana masuala tumboni street. Grants hutumika vibaya kisha wapo kiudugu zaidi sio real civil societies. Nyingi zina miradi isiyokamilika kutokana na grants walizopewa ila viongozi wana magari ya anasa na maisha mazuri kuliko walengwa. NGO nyingine (national NGOs sio International) viongozi wao hawabadiliki toka ianzishwe. Ni yeye Director toka ianze hadi kiama waka aibu haoni. Halafu utaona anailaumu serikali ya CCM haina demokrasia ila yeye ni kiongozi wa kuteulia mpaka dunia iishe hiyo ndio demokrasia!! Aluta continua!!

Ila pamoja na kuwa haihusiani na suala hili la NGO-Ninalipongeza gazeti la NIPASHE sasa kuwa hasa kioo cha Jamii baada ya binafsi kuwa mstari wa mbele kulisakama kwa muda na matokeo masuri yameonekana-Page 18 ya matangazo madogo madogo imebadilika kiukweli. page hii inaonekana kwa sasa kuwa imeacha kutangaza uganga unaokiuka maadili. Yaani yale matangazo ya dawa ya biashara e.g. jini chuma ulete, dawa ya kupasi mitihani; dawa ya kuchaguliwa hata kama umefeli mtihani; kumvuta mpezi unayemtaka akutimizie asitoke milele au asikuache; kushinda kesi mahakamani; hirizi ya bahati; kukuza nonino na hamu urudie zaidi ya mara kumi kwa siku; kukuza nyota yako bosi wako akupende etc. Hongereni-haya sasa hayapo!! Aluta continua!!

NGO nazo zijirekebishe ili zisaidie maendeleo vijijini na usafi mijini. Undeni Volunteer system na hizo hela mzalishasho kwa mikopo au uwekezaji halali, muajiri vijana wakawahamasishe wananchi kufanya kweli ktk maendeleo yao wajikwamue.Kelele tu bila matendo ni mbaya. Huwezi kuwa na kelele za kuwezesha wananchi, demokrasia, maendeleo etc ambapo hapo mtaa ofisi ilipo NGO yako ya uharakati wa maendeleo kuna mitaro imejaa uchafu wa kila aina; kuna wasichana wadogo na wakubwa wanajiuza kuanzia saa 12 hadi manane mtaani hapo; kuna wananchi wanafanya makazi, wameweka garage, restaurant wazi ktk open sape na ktk uwanja wa shule au kuuza biashara ya chakula na kuweka makazi kwenye maji machafu yenye kunuka na mainzi na unaona hufanyi kitu kuwaita ukaongea nao, ukahamasisha usafi kwa ajiri ya haki za afya kwa binadamu na usalama wa watoto. nawe unakula hapo mtaani, unaruka kinyesi, unaingia ofisini au unatazama tu hao watoto wajiuzao. Mfano mzuri utoke wapi kama sio kwa NGO kimatendo? Utendaji wa NGO nao utathiminiwe sio wa Idara za GVT tu!!
Na wakifungua kampuni za mikopo-evaluation ya effectiveness ya mikopo ifanyike ili kuona hakukua na upendeleo wakapata wasiostahili ambao wanauwezo na udugu na baadhi ya NGO members needy people wakaachwa.

From: paul chilewa <poulchilewa@hotmail.com>
To: wanabidii blog <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 20 July 2013, 13:39
Subject: RE: [wanabidii] SUALA LA NGO KUFUNGUA KAMPUNI ZA MIKOPO

Nchi zilizo endelea zinahama toka kutoa msaada na sasa zinafanya biashara,iwe kwenye kilimo,miundombinu.Umesikia Obama uwekezaji kwenye umeme sio msaada bali wanayawezesha makampuni ya kimarekani kufanya biashara,sisi tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunakusanya kodi ilikujiletea maendeleo yetu,wao lengo ni faida.Mleongo huo sasa umehamia kwenye sekta zote.
 
Date: Fri, 19 Jul 2013 15:33:19 +0300
Subject: [wanabidii] SUALA LA NGO KUFUNGUA KAMPUNI ZA MIKOPO
From: oldmoshi@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com; wanazuoni@yahoogroups.com

Ndugu zangu 

Katika siku za karibuni tumeona zile NGO kubwa zilizokuwa zinatoa huduma mbalimbali kwa jamii zikifungua kampuni za kutoa mikopo kwa wananchi mbalimbali au zenyewe kuanza kutoa mikopo moja kwa moja kwenye zile jamii wanazozihudumia .

Kwa mfano halisi ni World Vision ambayo ina kampuni inayoitwa Vision Fund international kwa ajili ya masuala ya fedha na mikopo , kuna CHAI ambayo ni ya rais wa zamani wa Marekani ambayo imeanzisha programu za mikopo kwa nchi ya tanzania na malawi .

Hili suala mimi silielewi kwa NGO kujiingiza kwenye biashara haswa za mikopo kwa wananchi maskini walalahoi , ina maana sasa wanarudisha zile fedha zao walizotoa kwenye jamii hizi .

--
Find Jobs in Africa Jobs in Africa
International Job Opportunities International Job Opportunities
Jobs in Kenya Jobs in Kenya

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment