Saturday, 10 June 2017

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Mzimu Wa Brexit Unamwandama Theresa May Wa Uingereza...!

Ni kweli,naona matokeo yamekwenda kinyume na matarajio,ingawaje Bi Theresa May ataunda serikali ya mseto naungana nawe kuwa kujitoa EU ni zimwi likujualo halikuli likakwisha


On Saturday, June 10, 2017 2:24 PM, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Uingereza hayampi furaha Waziri Mkuu Theresa May.
Wahenga walisema; mchimba kisima huingia mwenyewe. Theresa May kwa kudhani kuwa uchaguzi huu ungempa sio tu uhalali wa kuwa Waziri Mkuu aliyetokana na uchaguzi, alitegemea upepo wa Brexit ungevumia upande wake na kuongeza viti zaidi Bungeni.
La hasha, viti 12 vimepungua, hivyo. Anakwenda kuunda Serikali Kondefu- Minority Goverment, tena na Chama Mshirika- DUP- Democratic Unionist Party chenyenye rekodi tata kuhusiana na masuala ya haki za wanawake na hata chama hicho kutilia shaka hatua za mataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Theresa May amepata asichokuwa amekitaka. Naam, Thereza May anawaongoza Waingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya huku akiandamwa na zimwi la Brexit, yumkini ni zimwi litakalokitafuna chama cha Wahafidhina- conservative likawesha.
Na Zimwi hili la Brexit lina maana gani kwetu Wa-Afrika?
Nimepata kuandika haya kwenye mtandao wa Mabloga wa Afrika... Soma...http://www.africablogging.org/what-does-brexit-mean-for-af…/
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye77T-WKRC%2BVP2vV3VB%2Bo2PbA_ZsL6CimohBM0ecm7uAZw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment