Friday 30 June 2017

Re: [wanabidii] MJADALA KUHUSU RASLIMALI ZETU: UMAKINI MAKINI UNAHITAJIKA KATIKA MIJADALA IJAYO

Ahsante sana Elisa. Ingawa kuna usemi wa kiswahili usemao kuwa ukitaka kula na kipofu sahani moja usimkamate mkono, watu wengi tulisha liona hilo! Baadhi tulikaa kimya si kwa kuwa ni vipofu au wapumbavu ila ni mazingira yaliyokuwepo! Sasa mzungu katukamata mkono, na kati yetu mmojawapo kafunguka macho kwa miujiza miujiza hivi na akamuona jamaa anakula chakula sehemu yetu pamoja kuwa kamaliza kula sehemu yake. Hili suala si ndoto za jinamizi ni ukweli mtupu. Katika nchi za SADC, au zamani zikiitwa Nchi za Msitari wa Mbele (The Front Line State), kuna nchi ambazo zina madini ya almasi, dhahabu, shaba, nikel n.k. nchi hizi zimenufaika na neema hizi zilizopewa na Muumba wa Mbigu na Dunia, na hizi nchi zina mikataba ya madini na hao wawekezaji!   Nchi hizi zina uzoefu wa muda mrefu na jinsi ya ku-negotiate na 'waheshimiwa wawekezaji' na mikataba hiyo haina wasi. Nchi hizi zipo humu humu SADC na zinafaidi tunu hizi walizopewa na M'nyezi Mungu. Sasa nchi yetu ambayo ni kati ya nchi za kwanza zilizoanzisha The Front Line States kupambana na Mkaburu wa Afrika ya Kusini wakati wa ubaguzi wa rangi, na Wareno kule Msumbiji na Ian Smith na kundi lake kule Zimbabwe, na kuikomboa Namibia pamoja na Angola, tunashindwa nini kuwauliza wenzetu kua hiyo mikataba ya madini mnatengenezaje na hao wawekezaji na ikafaidisha nchi zenu na wananchi wenu? Kweli hili linatushinda? 

Jamani nchi haitajengwa na watu kutoka nje itajengwa na sisi wenyewe hakuna cha njomba wala shangazi, hao hao ndio sasa wamerudi katika koti zuri la rangi ya UWEKEZAJI! Hao hao waliotutawala, na wanaendelea kututawala kwa sababu ya akili zetu na sio unyonge wetu. Tanzania sasa hivi ina wasomi wengi tu, sio zile enzi za miaka ya 60 au 70, wakati huo baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikataa kuchimba madini, hatukuwa na wataalam, kwa hiyo alijua tutaibiwa tu. Sasa tunaibiwa na wataalamu wapo!. Ushauri, tuwaulize wenzetu humu humu SADC kuhusu mikataba yao ya madini na hao 'waheshimiwa wawekezajia'. Nchi hizo ni Botswana na Namibia. Tusione aibu, kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!

    Mungu Ibariki Tanzania



Sent from Samsung tablet



-------- Original message --------
From 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date: 28/06/2017 22:16 (GMT+02:00)
To wanabidii@googlegroups.com,prudence karugendo <prudencekarugendo@yahoo.com>
Cc stanley.nshange@nsn.com,innokahwa@yahoo.com,akiobya@yahoo.com,tkiobya@yahoo.com,hkahyoza@yahoo.com,emmanuelelias2005@yahoo.com,repeatitagency@yahoo.com,stanley.nshange@nokia.com,uhalisi@yahoo.co.uk,tundu.lissu@gmail.com,pkarugendo@yahoo.com,mbowe2008@gmail.com,bilhuda2006@yahoo.co.uk,davidkafulila@yahoo.com,muddy.kiobya@gmail.com,emmanuelelisa46@yahoo.com,wilfredlwakatare@gmail.com
Subject [wanabidii] MJADALA KUHUSU RASLIMALI ZETU: UMAKINI MAKINI UNAHITAJIKA KATIKA MIJADALA IJAYO


Baada ya ripoti za rais kuhusiana na madini kutolewa na mambo yaliyofuata sasa watanzania tumerudi katika busara kubwa. Busara kubwa kwamba madini ni yetu. Busara kubwa sana kuwa haiwezekani tukaendelea kuibiwa. Busara kubwa kwamba hata waliojaribu kumpinga rais sasa wako kimya au wana lugha tofauti.
Haiepukiki kuamini kuwa huko nyuma tuliibiwa. Haiepukiki kuwa watanzania wenzetu katika ngazi mbalimbali za dhamana walizokabidhiwa, walitusaliti. Hata kama tutasema au tutanyamaza lakini kila tunapowaona na wao wanajua kuwa tunajua, kuwa walilisaliti taifa. Wapo tutakaowachukulia hatua. Wapo tutakaowaacha au kwa kuwaheshimu au kwa kuwahurumia na wengine kwa kinga tulizojiwekea bila kujua kuwa zitatuumiza. Lakini hatuamini kuwa hawajui kuwa tunajua walichokifanya. Mijadala ipo. Mfano Tutamshitaki waziri mstaafu na kumuacha aliyekuwa anamwagiza. Tunafanya hivyo huku tukijua kuwa tuliyemkamata alifanya makosa kwa sababu kuagizwa na tuliyemuacha. Lakini ukweli uko palepale. Wahaya wanasema "Empisi ekanyampila eibale. Eti olayesiza kyonka wakaulila". Yaani chui alilijambia jiwe. Akaliambia japo umenyamaza lakini umekasikia.
 
Wakati hilo likifanyiwa kazi, jingine linalosubiriwa ni mjadawa na hao "wawekezaji".
Huku nyuma walitwambia uwekezaji ni garama kubwa kiasi kwamba  inabidi watugawie kitu kidogo baada ya kuchimba madini kwa sababu kuchimba madini ni aghali sana. Tukakubali. Au niseme viongozi wetu wakakubali. Sasa hiyo haitarajiwi.
Nimekuwa nikifikiri. Ngoja niandike hicho ninachokifikiri. Kama ningechangia msingi wa kujadiliana katika marekebisho ya mikataba ya madini ningesema hivi: Kuna pande mbili:
Upande mmoja ni Tanzania yenye madini. Ni mali yake. Kwa haki nchi inaweza kuendelea kubaki nayo au kuyachimba inavyotaka.
Upande wa pili ni wa wawekezaji. Wana mitambo, Ujuzi wana wajuzi nk.
 
Pande hizi mbili zinahitaji kuungana na kufaidiana. Ilikuwa aibu kujiambia kuwa thamani ya mitambo, utaalamu na wataalamu vina thamani kuliko dhahabu dhahabu yetu. Haiwezekani kwa mfano kutumia ng'ombe kupata mbuzi. Kwa nini usikae na ng'ombe wako. Kwa nini wazungu watwambie wana mbuzi mwenye thamani kuliko ng'ombe wetu. Kama ni hivyo si wakae na mbuzi wao?!
 
Wawekezaji waje na kila walicho nacho. Nasi tukutwe na tulicho nacho. Tutumie vya kwao kuyafukua na kuyaleta juu ya ardhi madini yetu na tuambizane: Mmetumia kiasi gani? Kiasi watakachotumia wawekezaji ndicho kiasi tunachotaka kwanza. Yaani wakitumia dola milioni moja kuyachimbua tunatoa milioni mbili. Moja yetu, moja yao. Ile thamani ikibaki tunagawana kati kwa kati.
Nchi hii imedanganywa sana. Kuna wakati sheria ilikuwa inasema kila mradi wa madini asilimia ishirini na tano (25%) imilikiwe na watanzania. Wajamaa wakawa wanakuja wanamdanganya mtanzania kuwa ana hiyo asilimia lakini hawampi kiasi hicho. Tulipoanza kuandika kuwa basi hao watanzania waulizwe hiyo 25% wameiweka wapi, sheria ikabadilishwa.
Niliwahi kuona picha ya hazina ya dhahabu ya uingereza. Hazina ambayo ndiyo inasaidia kusema Uingereza ni tajili. Hazina inayosaidia kuituliza hela ya Uingereza. Zamani za Nyerere benki kuu ilikuwa inanunua dhahabu kutoka kwa watanzania wanaochimba dhahabu kwa kutumia vijiti. Sehemu ya dhahabu hiyo ilikuwa inawekwa akiba. Nina mashaka kama manyang'au waliopita waliibakiza. Umefika wakati sehemu ya dhaahabu ya Tanzania ikawekwa hakiba. Kama hapa si salama watuwekee hao wanaoweza kuitunza. Lakini iwe yetu. Jamani, tunajua kuwaiga. Tumeiga matamshi, tumeiga kuvaa, tumeiga miondioko. Tumetelekeza lugha yetu ili tusionekane washamba kuongea vizuri lugha yetu. Kwa nini tusiige ujanja wao!? Kwa nini tusiige uzalendo wao kwa nchi zao nasi tukathamini yetu?!
 
Elisa Muhingo
0767 187 507

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment