Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Uingereza hayampi furaha Waziri Mkuu Theresa May.
Wahenga walisema; mchimba kisima huingia mwenyewe. Theresa May kwa kudhani kuwa uchaguzi huu ungempa sio tu uhalali wa kuwa Waziri Mkuu aliyetokana na uchaguzi, alitegemea upepo wa Brexit ungevumia upande wake na kuongeza viti zaidi Bungeni.
La hasha, viti 12 vimepungua, hivyo. Anakwenda kuunda Serikali Kondefu- Minority Goverment, tena na Chama Mshirika- DUP- Democratic Unionist Party chenyenye rekodi tata kuhusiana na masuala ya haki za wanawake na hata chama hicho kutilia shaka hatua za mataifa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Theresa May amepata asichokuwa amekitaka. Naam, Thereza May anawaongoza Waingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya huku akiandamwa na zimwi la Brexit, yumkini ni zimwi litakalokitafuna chama cha Wahafidhina- conservative likawesha.
Na Zimwi hili la Brexit lina maana gani kwetu Wa-Afrika?
Nimepata kuandika haya kwenye mtandao wa Mabloga wa Afrika... Soma...http://www.africablogging.org/what-does-brexit-mean-for-af…/
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment