Wednesday, 9 September 2015

Re: [wanabidii] Kwa nini Rose Kamili si kamili

Elisa, Kama una uwezo, beba mimba, zaa, tunza watoto kwa style hiyo, kisha utajua nini la kufanya.Mwache Rose Kamili afanye anayoyaona yanamfaa kama mama.Wewe ni mwanamme, huwezi kuvaa uanamke hata siku moja!

SB

On Sep 9, 2015 11:12 PM, 'mpombe mtalika' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Kwa nini Rose Kamili si kamili

MALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya mke wake wa zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk. Slaa anatangaza kung'atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli.

Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya, lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri.
Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi?
Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.

Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa akishindia mihogo na familia yake ili aisadie Chadema ni lugha ya picha ambayo haikuwa na maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.

Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa kuisaidia Chadema kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia yake na hata wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni ili chama hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala njaa.

Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba alazimishe kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha Ukawa.
Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa kisiasa na CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata yeye basi anatumiwa na Ukawa kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?

Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho.

0 comments:

Post a Comment