Thursday 12 December 2013

Re: [wanabidii] Sheria kumsulubu Zitto kwa kukiri hana majina ya wenye mabilioni Uswisi

Zzk ni sawa na mfungua shampeni, keshaitikisa kwa mbwembwe na kuizibua sasa ni kazi ya mc kuendelea na sherehe,

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, December 12, 2013 9:29:01 PM GMT-0800
Subject: [wanabidii] Sheria kumsulubu Zitto kwa kukiri hana majina ya wenye mabilioni Uswisi

*Na Beda Msimbe, Dodoma *— MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema
amesema wanashughulikia kisheria suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe
Zitto kudanganya Bunge na Kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni
ya fedha Uswisi.

Werema ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya kuchunguza madai ya
mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Naibu
Spika wa Bunge kuiongezea kamati hiyo miezi sita.

Akitoa majumuisho ya taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Kamati ya Bunge
ya Katiba, Sheria na Utawala, Werema alisema
alishangaa kitendo cha Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo
majina ya watu walioficha mabilioni hayo.

Alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa fedha hizo
lakini Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya
watu walioficha hizo.

Alisema mwezi Februari, Kamati ilikutana na Zitto na kuwaeleza kuwa ana
taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka ka kwenda katika
kambi ya jeshi kwa mafunzo ambako kamati ilimfuata lakini bado aliwataka
kukutana Dar.

Alisema Mei mwaka huu amekuwa akiichenga kamati hiyo hadi Oktoba ndipo
alipokiri kwa kiapo maalumu kuwa hakuwa na jina wala akaunti ya mtu yeyote
ambaye ana fedha nchini Uswisi.

"Jambo la kushangaza ni leo kudai serikali haina dhamira na suala la
walioficha fedha Uswisi? Kwa keli Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia
kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama serikali kwa kutafuta taarifa bila
kumuonea mtu," alisema Werema.

via Lukwangule blog<http://lukwangule.blogspot.com/2013/12/zitto-katika-hili-inakuwa-shida-sasa.html>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment