Thanks!
------Original message------
From: Mathew Mndeme <mathewmndeme@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, December 7, 2013 2:04:29 AM GMT+0300
Subject: [wanabidii] PALE KANISA LINAPOJITOLEA KUKARABATI KITUO CHA POLISI OSTERBAY
Mwezi uliopita nililazimika kwenda *Kituo cha Polisi cha
Osterbay*kutimiza masharti au sheria inayohitaji gari kukaguliwa kila
mwaka kama
taratibu za usalama barabarani. Hii haikua mara yangu ya kwanza kufika
kwenye kituo hiki kwani nimekua nikifanya hivi karibu kila mwaka. Nilipokua
naelekea zilipo ofisi za Usalama barabarani ambazo ziko nyuma ya jengo
kubwa la kituo, nikashangaa kuona mabadiliko makubwa ya mwenekano wa
majengo ya kituo kile. Niliona ukarabati mkubwa uliokuwa unaendana na
majengo kupakwa rangi. Nilipofika nyuma ya jengo nilikuta jengo dogo ambalo
ndilo lina ofisi za Usalama Bararani nalo likiwa limebadilika na ofisi
imehamishwa kwenye chumba kilichokua chatumika awali. Mshangao wangu
uliendelea nilipoingia ofisini na kukuta maasifisa wa polisi waliokua mule
ndani wamekaa kwenye ofisi safi na zenye samani (furnitures) mpya, safi na
za thamani kama zilizo kwenye ofisini nyingine za kisasa.
Sikuweza kumuuliza yeyote juu ya mabadiliko yale na ndani mwangu
nikajisemea kuwa ni nafuu kama polisi wameona umuhim wa kuboresha majengo
yao na kuyafanya yawe na mvuto. Baada ya kumaliza kilichonipeleka, niliamua
kuangalia kwa karibu bango linaloonesha ujenzi unaondelea ili nijue ni nani
anafanya ukarabati ule. Kwa mshangao mkubwa, macho yangu yaligongana na
Jina la kanisa la *CHRIST EMBASSY TANZANIA *ambalo pia linaitwa LOVE WORLD
kwenye kibao kile kama mfadhili wa ukarabati ule. Kwa maana nyingine kanisa
la *CHRIST EMBASSY TANZANIA* ndio wamejitolea kukarabati *KITUO CHA POLISI
OSTERBAY*.
Nilivutiwa sana na kibao kile na nikatamani nikipige picha ili nikaitumie
nitakapoamua kuweka jambo lile kwenye maandishi. Lakini nikashtukia kuwa
niko kwenye himaya ya usalama na kama ningetimiza haja ya moyo wangu huenda
ningeshtuka baadaye sana nikiwa selo baada ya kupata mtikisiko wa ubongo
(concussion) ambao ungekua umesababishwa na "mitama ya mfululizo" ambayo
ningeipata hata kabla sijamaliza kupiga picha ya kwanza.
Nilitiwa moyo sana na kitendo hiki cha dhehebu la dini kujitolea kukarabati
kituo cha polisi. Sina hakika kama walifanya hivi kwa kuombwa au kwa
kukusudia wao wenyewe, lakini kwangu niliona ni aina mpya ya jinsi
madhehebu ya dini na hasa kanisa kuonesha upendo wa kubadilisha maisha ya
wengine kwa vitendo. Kilichonigusa zaidi kwa msaada huu ni ukweli kwamba
vituo vingi vya polisi kote nchini, ni kati ya majengo ya umma ambayo kwa
sehemu kubwa yako katika mazingira duni, machafu, na yasiyo a mvuto kabisa
jambo ambalo linavifanya visiwe rafiki sio tu kwa waonkwenda kutafuta
huduma bali hata kwa polisi wenyewe wafanyao kazi humo. Huenda hali hii ya
majengo na mazingira ya vituo vya polisi ndiyo imefanya watu wengi
kutopenda kabisa kufika katika vituo vya polisi maana mazingira yake
hayaoneshi kuwa ni maneo rafiki na salama kwa anayekwenda kutafuta haki,
kulazimika kutoa haki kwa wengine au kuwajibika kwa matendo yao. Huenda
mazingira haya ndio yanawafanya askari polisi wengi kutokua rafiki kabisa
na raia na wenye jazba na hasira muda mwingi kwa vile mazingira ya kazi
yanayowazunguka hayawaoneshi kuwa ni watu wa thamani na kazi yao ina
heshima na hivyo kulazimika kutumia njia nyingine kujitafutia heshima.
Kwa wale waliojifunza manejimenti hasa katika nadharia (concepts) za hamasa
(motivations) zinazoweza kumfanya mfanyakazi au mtumishi kutimiza wajibu
wake vizuri, wanafahamu kuwa sio ukubwa wa ujira/mshahara pekee unaochangia
hamasa bali kuna mambo (factors) mengine ambayo yako kisaikologia, kiutu na
kitamaduni zaidi. Kuthibitisha hili, unaweza kuona baadhi ya watu wanaacha
kazi nzuri zenye cheo au kipato kikubwa katika kampuni, shirika au hata
katika taasisi za serikali kwa kigezo cha kutoridhika na mazingira ya kazi.
Ndio mana ni rahisi kusikia matapeli wakidanganya watu kuwa wao ni maafisa
wa usalama wa taifa, wako TRA au BOT na sio maafisa magereza, fire au
makarani wa mahakama. Hamasa ya kazi na kuipenda kazi vinachangiwa sana na
mazingira ya ofisi au eneo la kazi kuwa na mvuto unaotokana na thamani ya
ofisi yenyewe na samani zilizoko, usafi wa ofisini na eneo ofisi ilipo.
Ndio mana ni rahisi kumsikia mtu hata isivyo kweli kuona fahari kusema
ofisi yake iko Posta au Masaki kuliko aseme anakwenda ofisini Tandale au
Mburahati.
Nawapongeza sana uongozi na kanisa la Christ Embassy Tanzania *kwa ufunuo
huu* wa kuboresha mazingira ya kituo cha polisi. Kazi yenu ni kubwa kwani
hamujasadia tu kufanya majengo yawe na mvuto, bali mumewasaidia maafisa na
askari wafanyao kazi katika kituo hiki kuona na kujisikia kazi yao ni ya
muhim, yenye thamani na ya heshima na hivyo kuongeza hamasa ya utendaji
kazi wao katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao huku wakitenda
haki. Kuna tofauti sana ya utendaji kazi kati ya askari anayetoka nyumbani
kwenye kazini huku akiwaza kuwa zaidi ya bunduki, ofisi yake ina tiles
chini, ina ukuta msafi na anakalia kiti cha kuzunguka; ukimlinganisha na
yule anayewaza bunduki iliyo kwenye ofisi chafu, isiyo na ukuta msafi na
yenye kiti cha mbao kichafu, kibaya na wanachokalia kwa kupokezana
kutegemeana na nani alitangulia kukaa.
Nawatia moyo madhehebu mengine ya Kikristo na dini zingine, kuiga mfano huu
mzuri wa Christ Embassy wa kusaidia maeneno yanaoonekana sio rafiki kwa
jamii kama Polisi. Kama kila kanisa katika eneo lililoko likijotolea
kukarabati au kujenga vituo vya polisi, ni wazi dhana nzima ya POLISI JAMII
itakua imeongezewa nguvu kwa namana ya kipekee na MATOKEO MAKUBWA SASA ya
kiusalama yatakua dhahiri kwa kila mmoja.
*Mwalim MM*
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment