Big thumb
Saidi Kindamba <saidikindamba@yahoo.com> wrote:
>Thanks!
>
>
>------Original message------
>From: Mathew Mndeme <mathewmndeme@gmail.com>
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Date: Saturday, December 7, 2013 2:04:29 AM GMT+0300
>Subject: [wanabidii] PALE KANISA LINAPOJITOLEA KUKARABATI KITUO CHA POLISI OSTERBAY
>
> Mwezi uliopita nililazimika kwenda *Kituo cha Polisi cha
>Osterbay*kutimiza masharti au sheria inayohitaji gari kukaguliwa kila
>mwaka kama
>taratibu za usalama barabarani. Hii haikua mara yangu ya kwanza kufika
>kwenye kituo hiki kwani nimekua nikifanya hivi karibu kila mwaka. Nilipokua
>naelekea zilipo ofisi za Usalama barabarani ambazo ziko nyuma ya jengo
>kubwa la kituo, nikashangaa kuona mabadiliko makubwa ya mwenekano wa
>majengo ya kituo kile. Niliona ukarabati mkubwa uliokuwa unaendana na
>majengo kupakwa rangi. Nilipofika nyuma ya jengo nilikuta jengo dogo ambalo
>ndilo lina ofisi za Usalama Bararani nalo likiwa limebadilika na ofisi
>imehamishwa kwenye chumba kilichokua chatumika awali. Mshangao wangu
>uliendelea nilipoingia ofisini na kukuta maasifisa wa polisi waliokua mule
>ndani wamekaa kwenye ofisi safi na zenye samani (furnitures) mpya, safi na
>za thamani kama zilizo kwenye ofisini nyingine za kisasa.
>
>
>Sikuweza kumuuliza yeyote juu ya mabadiliko yale na ndani mwangu
>nikajisemea kuwa ni nafuu kama polisi wameona umuhim wa kuboresha majengo
>yao na kuyafanya yawe na mvuto. Baada ya kumaliza kilichonipeleka, niliamua
>kuangalia kwa karibu bango linaloonesha ujenzi unaondelea ili nijue ni nani
>anafanya ukarabati ule. Kwa mshangao mkubwa, macho yangu yaligongana na
>Jina la kanisa la *CHRIST EMBASSY TANZANIA *ambalo pia linaitwa LOVE WORLD
>kwenye kibao kile kama mfadhili wa ukarabati ule. Kwa maana nyingine kanisa
>la *CHRIST EMBASSY TANZANIA* ndio wamejitolea kukarabati *KITUO CHA POLISI
>OSTERBAY*.
>
>
>Nilivutiwa sana na kibao kile na nikatamani nikipige picha ili nikaitumie
>nitakapoamua kuweka jambo lile kwenye maandishi. Lakini nikashtukia kuwa
>niko kwenye himaya ya usalama na kama ningetimiza haja ya moyo wangu huenda
>ningeshtuka baadaye sana nikiwa selo baada ya kupata mtikisiko wa ubongo
>(concussion) ambao ungekua umesababishwa na "mitama ya mfululizo" ambayo
>ningeipata hata kabla sijamaliza kupiga picha ya kwanza.
>
>
>Nilitiwa moyo sana na kitendo hiki cha dhehebu la dini kujitolea kukarabati
>kituo cha polisi. Sina hakika kama walifanya hivi kwa kuombwa au kwa
>kukusudia wao wenyewe, lakini kwangu niliona ni aina mpya ya jinsi
>madhehebu ya dini na hasa kanisa kuonesha upendo wa kubadilisha maisha ya
>wengine kwa vitendo. Kilichonigusa zaidi kwa msaada huu ni ukweli kwamba
>vituo vingi vya polisi kote nchini, ni kati ya majengo ya umma ambayo kwa
>sehemu kubwa yako katika mazingira duni, machafu, na yasiyo a mvuto kabisa
>jambo ambalo linavifanya visiwe rafiki sio tu kwa waonkwenda kutafuta
>huduma bali hata kwa polisi wenyewe wafanyao kazi humo. Huenda hali hii ya
>majengo na mazingira ya vituo vya polisi ndiyo imefanya watu wengi
>kutopenda kabisa kufika katika vituo vya polisi maana mazingira yake
>hayaoneshi kuwa ni maneo rafiki na salama kwa anayekwenda kutafuta haki,
>kulazimika kutoa haki kwa wengine au kuwajibika kwa matendo yao. Huenda
>mazingira haya ndio yanawafanya askari polisi wengi kutokua rafiki kabisa
>na raia na wenye jazba na hasira muda mwingi kwa vile mazingira ya kazi
>yanayowazunguka hayawaoneshi kuwa ni watu wa thamani na kazi yao ina
>heshima na hivyo kulazimika kutumia njia nyingine kujitafutia heshima.
>
>
>Kwa wale waliojifunza manejimenti hasa katika nadharia (concepts) za hamasa
>(motivations) zinazoweza kumfanya mfanyakazi au mtumishi kutimiza wajibu
>wake vizuri, wanafahamu kuwa sio ukubwa wa ujira/mshahara pekee unaochangia
>hamasa bali kuna mambo (factors) mengine ambayo yako kisaikologia, kiutu na
>kitamaduni zaidi. Kuthibitisha hili, unaweza kuona baadhi ya watu wanaacha
>kazi nzuri zenye cheo au kipato kikubwa katika kampuni, shirika au hata
>katika taasisi za serikali kwa kigezo cha kutoridhika na mazingira ya kazi.
> Ndio mana ni rahisi kusikia matapeli wakidanganya watu kuwa wao ni maafisa
>wa usalama wa taifa, wako TRA au BOT na sio maafisa magereza, fire au
>makarani wa mahakama. Hamasa ya kazi na kuipenda kazi vinachangiwa sana na
>mazingira ya ofisi au eneo la kazi kuwa na mvuto unaotokana na thamani ya
>ofisi yenyewe na samani zilizoko, usafi wa ofisini na eneo ofisi ilipo.
>Ndio mana ni rahisi kumsikia mtu hata isivyo kweli kuona fahari kusema
>ofisi yake iko Posta au Masaki kuliko aseme anakwenda ofisini Tandale au
>Mburahati.
>
>
>Nawapongeza sana uongozi na kanisa la Christ Embassy Tanzania *kwa ufunuo
>huu* wa kuboresha mazingira ya kituo cha polisi. Kazi yenu ni kubwa kwani
>hamujasadia tu kufanya majengo yawe na mvuto, bali mumewasaidia maafisa na
>askari wafanyao kazi katika kituo hiki kuona na kujisikia kazi yao ni ya
>muhim, yenye thamani na ya heshima na hivyo kuongeza hamasa ya utendaji
>kazi wao katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao huku wakitenda
>haki. Kuna tofauti sana ya utendaji kazi kati ya askari anayetoka nyumbani
>kwenye kazini huku akiwaza kuwa zaidi ya bunduki, ofisi yake ina tiles
>chini, ina ukuta msafi na anakalia kiti cha kuzunguka; ukimlinganisha na
>yule anayewaza bunduki iliyo kwenye ofisi chafu, isiyo na ukuta msafi na
>yenye kiti cha mbao kichafu, kibaya na wanachokalia kwa kupokezana
>kutegemeana na nani alitangulia kukaa.
>
>
>Nawatia moyo madhehebu mengine ya Kikristo na dini zingine, kuiga mfano huu
>mzuri wa Christ Embassy wa kusaidia maeneno yanaoonekana sio rafiki kwa
>jamii kama Polisi. Kama kila kanisa katika eneo lililoko likijotolea
>kukarabati au kujenga vituo vya polisi, ni wazi dhana nzima ya POLISI JAMII
>itakua imeongezewa nguvu kwa namana ya kipekee na MATOKEO MAKUBWA SASA ya
>kiusalama yatakua dhahiri kwa kila mmoja.
>
>
>
>*Mwalim MM*
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment