Friday 6 December 2013

Re: Re: [wanabidii] Hotuba Fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika bunge mjini Dodoma (Alhamisi Feb. 7, 2008)

Kama kuna haja ya kutukumbusha hotuba hii basi iko pia sababu ya kuletea angalau kwa muhdarari taarifa ya tume ya Mwakyembe ambayo pamoja na kuuonyesha uharifu wa aliyekuwa Waziri Mkuu lakini ilionyesha kuwa waliyobakiza yalitosha kumhukumu PM huyo na wa kupima mambo alikuwa awe Rais. Hapo wengine tuliipongeza tume na wengine wakailaumu.

----------
Sent from my Nokia Phone

------Original message------
From: Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
To: "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Friday, December 6, 2013 12:44:43 PM GMT+0300
Subject: Re: [wanabidii] Hotuba Fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika bunge mjini Dodoma (Alhamisi Feb. 7, 2008)

Asante kwa kumbukumbu nzuri ni mahali pazuri kama mtu anahoji mambo ya
Richmond atoe majibu ya maswali ya Former PM. Kama kuna mtu ana kumbukumbu
ya hitimisho ya Taarifa ya Kamati ni vizuri ikawekwa hapa jukwaani.


2013/12/6 Fakhi Karume <fkarume@gmail.com>

> Hotuba fupi aliyoitoa Waziri Mkuu Edward Lowassa katika bunge mjini Dodoma
> (Alhamisi Feb. 7, 2008) wakati wa mjadala wa taarifa ya kamati teule ya
> bunge iliyochunguza mchakato wa Zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura
> ulioipa ushindi (Richmond Development Company LLC) ya Houston, Texas,
> Marekani mwaka 2006. "Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuchukua nafasi hii
> kukushukuru sana kwa kunifanya msemaji wa kwanza katika hoja hii. Lakini la
> pili, nimpongeze Dk. Harrison Mkwakyembe, Mwenyekiti wa kamati Teule kwa
> kuwasilisha kwa mbwembwe nyingi sana taarifa yake, mbwembwe zilikuwa nzuri
> kweli. Kwa kazi nzuri kwa maoni yao, wamewasilisha vizuri. Lakini
> nimesimama kuweka kwenye kumbukumbu kutoridhika kwangu na jinsi kazi hiyo
> ilivyofanywa. Mheshimiwa Dk. Mwakyembe ni Mwanasheria, tena Daktari alikuwa
> anafundisha Chuo Kikuu. Moja ya vitu alivyokuwa anafundisha ni "Natural
> Justice". Mheshimiwa Spika, wewe ni Mwanasheria unafahamu suala la Natural
> Justice. Kwamba Kamati Teule imesikiliza watu wengine wote pamoja na
> wanaoita minong'ono ya mitaani, wamesafiri mpaka Marekani kutafuta
> mashahidi, lakini mimi ambaye ni mmoja kati ya watuhumiwa mle hawakunihoji
> hata siku moja. Mheshimiwa Spika, nimesimama kueleza masikitiko yangu.
> Ofisi ya Bunge mpaka ofisini kwangu hata kama wangeniita ningekwenda kwa
> miguu kama hamna gari na nilikuwa tayari kufanya hivyo. Hawa ni watu makini
> sana siwezi kuamini kwamba wanaweza wakafanya oversite kama hiyo. Kwa
> sababu katika kila hoja walizojenga wamesema Waziri Mkuu ilikuwa hivi.
> Kulikuwa na shida gani kuja kuniuliza Waziri Mkuu wanasema uliotoa dokezo
> hili ni sawa sawa kweli? Kulikuwa na shida gani kwa mfano kufuata utaratibu
> wa Westminster kuthibitisha hapo unaposema mwenye Richmond ni fulani
> uka-lay on the table records na ushahidi kuwa ni fulani. Mheshimiwa Spika,
> Taifa letu ni Taifa changa, lakini chombo hiki ndiyo mahali pa demokrasia
> pakubwa katika nchi pote, hapa ndipo penyewe. Kama katika chombo hiki haki
> haitaonekana kutendeka nchi yetu haitakwenda vizuri. Hapa ndipo tunategemea
> tuwaonyeshe umakini wetu, umahiri wetu katika mambo ya demokrasia. Kwa
> nhiyo nilichofanyiwa napenda kuweka kumbukumbu sawa kwamba naona si sahihi,
> nimefadhaika sana, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana katika hili. Maana
> zimechukuliwa tuhuma zikaelezwa hapa kwamba hivi ndivyo ilivyo. Mimi
> sijauliza. Kulikuwa na shida gani kuniuliza, kwa nini muamini minong'ono ya
> mitaani kuliko maelezo yangu. Sisi wote hapa ni wanasiasa tukianza kuamini
> minong'ono ya mitaani niambieni mwanasiasa atakayesimama. Hatuwezi, Tume
> imepewa muda wa kutosha lakini inashindwa kumuona mtu ambaye wanamtuhumu na
> wanamsema kwa kirefu sana. Mheshimiwa Spika, lakini hata pale
> uliponinong'oneza ukaniambia una ushahidi wowote? Nilikupa ushahidi huo wa
> maandishi. Katika taarifa yao hakuna hata moja ya ushahidi ambao umetoka
> Waziri Mkuu. Kile kitabu cha majedwali kimejaa majedwali mengi pamoja na
> magazeti mpaka ya Udaku lakini maelezo ya Waziri Mkuu hakuna hata moja.
> Mheshimiwa Spika, naamini ingekuwa ni heshima wangeiweka halafu wakasema
> tunakataa kitambulisho hiki kwa sababu hii na hii, hiyo ndiyo imejengwa
> hoja. Lakini kujenga hoja na kuja hapa Bungeni tunahutubia nchi nzima na
> kusema Waziri Mkuu amefanya hiki, amefanya hiki bila ya kumsikiliza
> nachelea kuuliza hivi mtu wa chini itakuwaje? Mheshimiwa Spika, lakini
> nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka
> watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike
> mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a
> wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri
> Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima
> au tumwajibishe. Mheshimiwa Spika, nimetafakari kwa niaba ya chama changu,
> kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba
> niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya
> uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani
> ya Bunge wa kumsingizia mtu. Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii
> kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa
> Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais. Nakushukuru
> wewe, nawashukuru Mawaziri na Manaibu Waziri, nawshukuru Waheshimiwa
> Wabunge na wanachama wa CCM tuliyosimamia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
> Mapinduzi. Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nashukuru".
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
> to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>



--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment