Saturday, 18 February 2017

[wanabidii] Re: VITA YA MADWA YA KULEVYA: WABUNGE WETU WAKO UPANDE GANI?

Nakubaliana na wewe na kila mtu anayesema "makonda alifanya kosa kuwataja watu" kuhusika na madawa ya kulevya. Ilibidi hatua za kwanza kufanyika. Hatua hizo ilikuwa kuwaita kituo cha polisi. Lakini ni ukweli uliowazi kuwa ingejulikana tu. Kosa hilo naliita kosa la kiufundi.
Kuna mawili ya kusema hapo: Nawahisi wanaotumia nguvu kubwa kumsema Makonda katika kosa lake la koiufundi, na kwa hiyo kuwafanya watu waone kosa la makonda ni kubwa kuliko ubaya wa madawa ya kulevya katika jamii; watu hao ama hawajui ubaya wa madawa ya kulevya (wabunge hawawezai kuwa wamojawao) ama wanahusika na ni wanufaika wa madawa hayo.
Pili Kumshuku mtu kuwa ni mhalifu ni wajibu wa vyombo vya serikali na kazi ya kusafishika ni ya mshukiwa. Atajisaffisha katika utaratibu wa upelelezi au Mahakamani. Gwajima kafanikiwa kujisafisha katika hatua za mwanzo na wengine wanaendelea. Ndivyo tulivyozoea kwa makosa yote na haiwezi kuwa ajabu kwa kosa hili.


Mihimili mikuu (enyomyo kwa lugha ya Kihaya) kuheshimiana ni muhimu sana. Lakini kama ikiheshimiana katika uharibifu mwisho wa mihimili hiyo ni kutimuliwa na wananchi kwa kutumia mifumo halali au haramu. Kwa hiyo heri kujitenga na uovu ukaishi kuliko kuamua kufa pamoja.

Ni kweli nimetaja Chiefdoms, na kweli zilikuwa Kingdoms zikashushwa ili awepo King.
Kusudi langu nililenga kupngelea tabia yetu ya kuheshimu vilivyotengenezwa Ulaya kuwa bora kuliko vyetu. Umenena kweli "walikaa maharamia huko Berlin". Iweje tuitetee Tanganyika ya maharamia na tuidharau Tanzania ya Nyerere na Karume?
Kama kuna mtu anauhoji muungano mimi ni mmoja wapo. Bila shaka umesoma makala yangu nikiwakosoa viongozi wastaafu. Ninauona Muungano wa Tanzania kama unavunjwa na viongozi. Kuwa na nchi moja ina watu wawili wanapigiwa mizinga ishirini na mmoja ni kuuvunja. Lakini mtu kusema Tanganyika (ambayom haiku kama nchi) inaitawala Zanzibar (ambayo nayo kama nchi haipo) ni uchochezi wala sio kuuhoji muungano. Ukisema Tundu Lisu anauhoji muungano kwa maneno hayo nitakuuliza kama kuna mahala ulimwambia kuwa kakosea. Kama sio uniache nimwambie humu na wote msikie na mnisaidie kumfafanulia.

Kwamba Czechoslovakia ilikuwa dhaifu kuliko zilivyo sasa Czech na Slovakia, sijui. Lakini huenda kama kosa la Czechoslovakia lililoleta udhaifu lingesahihishwa ikiwa pamoja ingekuwa na nguvu zaidi kuliko zilivyo zikiwa mbili. Hatuhitaji kujiuliza kama Zanzibar na Tanganyika zinaweza kuwa na nguvu zikitengana bali namna gani tuwe na taifa lenye nguvu la Tanzania.

Elisa Muhingo

--------------------------------------------
On Sat, 2/18/17, prudence karugendo <prudencekarugendo@yahoo.com> wrote:

Subject: Re: VITA YA MADWA YA KULEVYA: WABUNGE WETU WAKO UPANDE GANI?
To: "ELISA MUHINGO" <elisamuhingo@yahoo.com>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "stanley.nshange@nsn.com" <stanley.nshange@nsn.com>, "innokahwa@yahoo.com" <innokahwa@yahoo.com>, "akiobya@yahoo.com" <akiobya@yahoo.com>, "tkiobya@yahoo.com" <tkiobya@yahoo.com>, "hkahyoza@yahoo.com" <hkahyoza@yahoo.com>, "emmanuelelias2005@yahoo.com" <emmanuelelias2005@yahoo.com>, "repeatitagency@yahoo.com" <repeatitagency@yahoo.com>, "stanley.nshange@nokia.com" <stanley.nshange@nokia.com>, "uhalisi@yahoo.co.uk" <uhalisi@yahoo.co.uk>, "tundu.lissu@gmail.com" <tundu.lissu@gmail.com>, "pkarugendo@yahoo.com" <pkarugendo@yahoo.com>, "mbowe2008@gmail.com" <mbowe2008@gmail.com>, "bilhuda2006@yahoo.co.uk" <bilhuda2006@yahoo.co.uk>, "davidkafulila@yahoo.com" <davidkafulila@yahoo.com>, "muddy.kiobya@gmail.com" <muddy.kiobya@gmail.com>, "emmanuelelisa46@yahoo.com" <emmanuelelisa46@yahoo.com>, "wilfredlwakatare@gmail.com" <wilfredlwakatare@gmail.com>
Date: Saturday, February 18, 2017, 11:26 AM

Vita
dhidi ya madawa ya kulevya naikubali, ila inatakiwa
iendeshwe kwa uangalifu. Kukaa na kumtaja mtu kuwa anahusika
nayo kwa vile anayesema hivyo ana nafasi fulani au ampendi
fulani haiwezi kusaidia hata kidogo. Inabidi anayemtaja mtu
kuwa anajihusisha na madawa ya kulevya awe na uhakika beyond
reasonable doubt, vinginevyo tunaweza kujikuta tunatajana
kiujinga ili kuchafuana huku biashara na matumizi ya madawa
ya kulevya vikiendelea kwa kasi. Je, hilo linafaa?
Na
si ajabu mtu anayesema fulani anahusika na madawa ya kulevya
akawa yeye ndiye gwiji wa shughuli hiyo ila anasema hivyo
kujiweka mbali na hisia za kwamba na yeye anahusika.
Anawapumbaza watu wamuone yeye hawezi kuhusika nayo kwa vile
kawataja washukiwa. Kwa kiasi kikubwa naona hilo
linatumika.
Mfano
katajwa Askofu Gwajima, Gwajima kaenda na kuhojiwa akakutwa
hahusiki na madawa ya kulevya. Je, amfanyeje alimtaja?
Heshima ya Gwajima itarudishwa kwenye nafasi yake kwa
gharama gani? Usumbufu alioupata bei yake ni kiasi
gani?
Kama
ni suala la kumhisi mtu kutokana na ukwasi wake, yeye
Makonda mbona anasemwa kwa kipindi kifupi amekuwa na ukwasi
wa kutisha? Je, kama kipimo cha kushukiwa kujihusisha na
madawa ya kulevya ni ukwasi, mtu akisema kwamba Makonda naye
anahusika na madawa ya kulevya atakuwa amekosea
nini?
Mihimili
mikuu ya nchi yetu, enyomyo kwa lugha ya Kihaya, zinapaswa
ziheshimiane ndipo tuwe na matumaini ya kuiona nyumba yetu
ikiwa imara. Lakini inapotokea muhimili mmoja ukauona
mwingine ni wa ovyo haufai, kweli tuliomo ndani ya nyumba
tutaweza kuwa na uhakika wa usalama wa nyumba
yetu?
Elisa
umetaja kuwa kabla ya nchi yetu kuitwa Tanganyika zilikuwepo
chiefdoms mbalimbali zilizounganishwa na kutengeneza nchi
hiyo, halafu ukasema kwamba USA iliunganisha mataifa 50!
Nadhani kabla ya mkutano wa kijambazi wa Berlin kuanza
kufanyiwa kazi kwa kuigawana Afrika tulikuwa na Kingdoms na
siyo chiefdoms. Sababu wakuu wa falme zetu, abakama,
walikuwa hawana mamlaka nyingize juu yao. Wao ndio waliokuwa
Maamili Jeshi Wakuu wa himaya zao.
Kilichofanyika
mpaka wafalme wetu wakaitwa machifu ni arrogance ya
Wajerumani, kwamba hawezi kuwa na wafalme pande mbili za
nchi yao, tayari Tanganyika ilikuwa ni nchi yao, kwahiyo
wakawa demote kuwa machifu chini ya mfalme wa
Ujerumani.
Nchi
ambazo hazikutawaliwa na Ujerumani, kama Uganda,  zilibaki
na wafalme wake kina kabaka. Suala hilo niliwahi kuliongea
na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliponiambia baba
yake alikuwa chifu, nilipomuuliza alikuwa chifu chini ya
mfalme gani, kwa vile machifu ni kama wakuu wa mikoa au
wilaya, akacheka sana tukakubaliana kwamba baba yake alikuwa
mfalme wa Wazanaki na hakuwa chifu, akamalizia kwa kuniambia
kwamba "wewe Mnyamahanga una matata" alikuwa
akiniita Mnyamahanga kiutani.
Kuhusu
muungano, jambo hilo linazungumzika. Muungano uliundwa na
watu, tena wawil Nyerere na Karumei, kwahiyo mwakilishi wa
wananchi kama alivyo Tundu Lissu kuuhoji sio kosa la mauti.
Tumeshuhudia miungano mingi ikisambaratika baada ya wananchi
wa nchi hizo kutoona umuhimu wa kuziendeleza.
Czechoslovakia kwa sasa ni
mataifa mawili kama yaliyokuwa mwanzo, Czech na Slovakia,
tena yakiwa na nguvu zaidi kuliko yaliyokuwa nazo wakati
yakiwa kwenye muungano. Yapo mengine mengi yaliyoachana na
muungano yakiweo ya iliyokuwa USSR na Yugoslavia.
Prudence
Karugendo





From: ELISA MUHINGO
<elisamuhingo@yahoo.com>
To:
wanabidii@googlegroups.com; ELISA MUHINGO
<elisamuhingo@yahoo.com>
Cc:
elisamuhingo@yahoo.com; stanley.nshange@nsn.com;
innokahwa@yahoo.com; akiobya@yahoo.com; tkiobya@yahoo.com;
hkahyoza@yahoo.com; emmanuelelias2005@yahoo.com;
repeatitagency@yahoo.com; stanley.nshange@nokia.com;
uhalisi@yahoo.co.uk; tundu.lissu@gmail.com;
pkarugendo@yahoo.com; mbowe2008@gmail.com;
bilhuda2006@yahoo.co.uk; davidkafulila@yahoo.com;
muddy.kiobya@gmail.com; emmanuelelisa46@yahoo.com;
wilfredlwakatare@gmail.com; prudencekarugendo@yahoo.com
Sent: Tuesday, February
14, 2017 11:34 PM
Subject: VITA YA MADWA
YA KULEVYA: WABUNGE WETU WAKO UPANDE GANI?



Vita ya madawa ya kulevya
imeanza rasmi. Si kuwa hakukuwa na juhudi huko nyuma. La.
Ila sasa imeanza na msukumo mpya. Imeanza kwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar Es Salaam Paulo Makonda kuwataja watu wanaohisiwa
kujihusisha na madawa hayo. Mwanzoni alibezwa na kuambiwa
anacheza na dagaa. Baadaye akaongeza kwa kutaja majina
makubwa zaidi. Hapo ndipo hasa misimamo tofauti ilionekana.
Wengine wakasema hawawezi kwenda kwa sababu Mkuu wa Mkoa
hana mamlaka ya kushughulikia madawa ya kulevya. Wapo
waliotaja hasara watakayoipata kwa kuitikia wito wa Makonda
na vitisho vingine vingi.
Madawa haya
yameharibu vijana na yanaendelea kuwaharibu. Vijana wasomi,
wasanii wakishajiingiza katika madawa basi wanaharibika na
kupoteza mwelekeo. Namfahamu kijana aliyekufa baada ya
kunywa dawa za kilimo zilizokuwa zimetunzwa na wazazi wake
nyumbani. Huyo kijana alikuwa anamalizia degree yake ya
kwanza ya computer engineering. Alifukuzwa mara mbili kwa
sababu ya kuharibikiwa akili baada ya kutumia madawa ya
kulevya. Alipokosa madawa na bangi ikawa haimtoshi akaanza
kunywa dawa hiyo kidogo kidogo mpaka ilipomuua; na wazazi
waligundua baadaye sana. Madhara mengi tu huenda kila mmoja
ana mifano yake. Jingine lililo wasi ni habari kuwa wahusika
wakuu wa biashara hii ni wanasiasa; Wafayabiashara wakubwa
na wasanii. Katika orodha ya Makonda makundi hayo yote
yalitajwa.

Kati ya maneno
aliyokaririwa akitumia Ndugu Makonda ni kusema Wabunge
(Nadhani baadhi) ni wapuuzi na kuwa hufanya kazi ya kulala
bungeni.
Wakati ukweli ukiwa kama
nilivyoutia katika utangulizi, Wabunge na Bunge lilitoa
msimamo kuhusu maneno ya Makonda. Maneno yoyote aliyotamka
mtu au taasisi yanawakilisha msimamo wake kuhusiana na vita
ya madawa ya kulevya. Wabunge wetu walijibu juhudi za
Makonda kwa kuzingatia zaidi maneno yake kuhusu wabunge
badala ya lengo lake la kupiga vita madawa ya kulevya.
Sipendi kuungana na Makonda kuliudhi bunge letu lakini
nataka kujielekeza kuhusu matukio yanayoweza kutumika
kulishtua bunge (likitaka kushtuka) na kubadili mwelekeo.
Mifano:
1    Bunge limetunga
sheria kadhaa kuharamisha madawa ya kulevya ikiwemo bangi.
Siku moja mbunge mmoja alisimama bungeni na kusema kwao
bangi ni halali hivyo ihalalishwe. Je huu si upuuzi kwa
mbunge kutamka hivyo? Kama ni upuuzi; yeye aweza kuepuka
kuwa mpuuzi? Lakini Baada ya neno kama hili kutamkwa na
mbunge, wabunge wengine walipitisha azimio gani kuhusu
upuuzi huo? Reaction ya bunge zima kuhusu neno la mwenzao
ndilo linarejesha heshima ya bunge au kuiondoa.

2    Lakini tumtafakari
mwakilishi mwingine. Kama mbunge kuitwa mpuuzi ni kosa na
utovu wa heshima na madaraka ya Bunge, bila shaka viongozi
wa miimili mingine pia. Sasa mtu anasimama na kusema Rais ni
Dictator uchwara. Mtu huyo anasimama na kusema Tanzania
inaongozwa na rais wa ajabu ajabu. Kosa la rais ni kusema
taifa halijafikia mahala pa kuomba chakula kwani japo kuna
ukame lakini mvua zinazoendelea zaweza kutumika kulima
chakula kinachopungua! Maneno kama hayo japo yametamkwa nje
ya Bunge lakini kwa sababu yametamkwa na Mbunge ningetarajia
bunge kuwa na tamko. Kama Bunge likimrudi mwenzao kama
tulivyoona huko nyuma linaweka msingi wa kutoitwa bunge la
wapuuzi.

3    Nchi yetu
ilipata uhuru 1961. Kabla ya uhuru nchi hii imepitia
historia ya ajabu. Zamani za kale nchi ilikuwa ni chiefdoms
ndogo ndogo. Watu fulani wakakaa na kuziunganisha hizo
kabila na chiefdoms na kutengeneza kitu kinaitwa Tanganyika.
Baada ya uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, viongozi
tuliowachagua wakafanya uamuzi wa kuziunganisha nchi mbili
zilizokuwa huru. Sasa ni taifa moja. Linaitwa Tanzania.
Tumelitengeneza wenyewe. Lina katiba yake. Linatambuliwa
hivyo. Lina changamoto zake ndiyo maana tunajadiliaana namna
bora ya kuliimarisha na kuliendeleza. Ni mfano bora wa
kujivunia. Africa inajivunia. Ni matokeo ya kazi tuliofanya
sisi bada ya uhuru. Tanzania si ya kwanza kuungana duniani.
Mfano mmojawapo ni Marekani. Iliunganisha mataifa zaidi ya
50. Kuliwahi kutokea wapuuzi fulani wakati wa utawala wa
Abraham Linchoin wakitaka kulitenga taifa (jimbo) lao.
Walipata kichapo kikali hawajathubutu tena. Naamini hakuna
Mmarekani anaweza kuhoji muungano huo akaishi. Sisi tuna
binadamu mmoja. Tena ni mbunge wa bunge letu linalostahili
kuheshimiwa. Akasema Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika. Na
upuuzi mwingine mwingi tu. Mbunge huyo aliapa kiapo kuulinda
Muungano. Sasa je kitendo chake hicho si cha kipuuzi? Kama
ni cha kipuuzi, yeye sio mpuuzi? Bunge limetoa msimamo gani
kuhusu matamshi ya mwenzao? Je Bunge kumnyamazia mbunge wa
namna hiyo sio kitendo cha kipuuzi? Nakumbuka Speaker
aliyepita aliwahi kuwafyatukia wananchi kuwa bunge
linastahili kuheshimiwa baada ya wananchi kuwashambulia
wabunge kutoana na matamshi ya ajabu. Alitumia kifungu
hikihiki kinachombana Makonda. Alizimwa na wananchi
walipomvamia kwenye vyombo vya habari. Alichofanya ilikuwa
kuwabana wabunge wajiheshimu ili taswira yao mbele ya umma
wanaowakilishwa bungeni isiendelee kudhalilika.

4    Nchi yetu; kama
zilivyo nchi nyingine duniani, inakabiliwa na janga la
madawa ya kulevya. Vijana wetu wameharibika na kwa kweli huo
ni uharibifu wa nguvukazi ya taifa. Inatarajiwa kuwa
wananchi, viongozi wataungana kupiga vita uharibifu huu.
Sababu zi wazi kwa nini watu wote kuungana. Licha ya
uharibifu uliopo lakini wanufaika wana uwezo mkubwa kumnunua
yeyote. Katika vita kama hii lazima usemi wa Bush baada ya
shambulizi la Septemba 11 litumike: "Kama hauko nasi uko
kinyume nasi". Vita hii ngumu. Kuna waliojaribu na kuishia
kusema wanayo orodha ya wahusika. Hawakutaja hata jina moja.
Sasa amejitokeza kijana mdogo. Akawa jasiri kuwataja watu
wanaojihusisha na biashara hii. Kukanyagana ni jambo la
kawaida katika msafara wowote. Mtu kuamua kuingilia safari
kwa sababu ya kukanyagwa haiingii akilini. Kitendo cha
wabunge wetu kuungana kutaka mtu aliyethubutu aondolewe
kazini, si cha kawaida. Wabunge kusema wizara husika zipo na
Mkuu wa mkoa haimhusu, ni ishara mbaya. Haiingii akilini
kuwa viongozi wetu wanaweza kuonekana wanadhoofisha juhudi
za serikali kushughulikia janga hili.

Kimsingi kila mtu anastahili heshima.
Kuheshimiwa kukubwa huanza kwa mtu kujiheshimu. Taasisi pia.
Kama bunge haliwezi kufanya upuuzi hakuna anayeweza
kulidhania hivyo. Kama wakifanya upuuzi, hata kama hakuna
aliyewaita haimaanishi kuwa sio. Kwa kuzingatia kuwa wabunge
ni wanansiasa, na ilitarajiwa wabunge kama wanasiasa kuwa
waangalifu katiko hoja zao. La sivyo licha ya kuitwa wapuuzi
kwa haki, haiwezekani wapiga kura wasitake wawakilishi wao
kuchunguzwa. Hakuna mtu anayeweza kuwaita wabunge wapuuzi
kama hawafanyi upuuzi.
Elisa Muhingo
0767 187 507
     --
 
    
 

     Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
    
 

      
 
    
 
 
   Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
    
 
 
   wanabidii+...@ googlegroups.com 
 

    Utapata Email ya
 

     kudhibitisha ukishatuma
 
    
 

      
 
    
 
 
   Disclaimer:
 
    

 
     Everyone
posting to this Forum bears
  the sole
 
    responsibility
 
     for any legal
consequences of his or
  her postings,
 
   and
 

    hence
 
     statements and facts must be
presented
  responsibly.
 

   Your
 
     continued membership signifies that
  you agree to
 
   this
 
     disclaimer and pledge to abide by
our
  Rules and
 
    Guidelines.
 
    
 
 
   ---
 
    
 
     You received this
message because you
  are subscribed
 
   to
 

    the
 
     Google Groups "Wanabidii"
  group.
 
    
 
 
   To unsubscribe from this group and
 
stop receiving
 
 
 emails
 
     from
it, send an email to wanabidii+...@
 
googlegroups.com.
 
 
  
 
     For more
options, visit
 
    https://groups.google.com/d/
  optout.
 
    
 
 

 
 
 

  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 

  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
 
kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
 
Disclaimer:
 
  Everyone
posting to this Forum bears the sole

responsibility
  for any legal consequences
of his or her postings, and
hence
  statements and facts must be presented
responsibly. Your
  continued membership
signifies that you agree to this
 
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.
 
  ---
 
 
You received this message because you are subscribed to
the
  Google Groups
"Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
  from it, send an email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options,
visit

https://groups.google.com/d/optout.
 




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment