Saturday, 18 February 2017

[wanabidii] MCHANGO WA MUHIMILI WA MAHAKAMA KTATIKA UCHUMI WA NCHI: MAGUFULI KAMA SAMORA!

Siku za mwanzoni mwa uhuru wa Musumbiji, Serikali ya kijamaa ilimkabidhi mtaji msomi mmoja mradi wa biashara ambao siukumbuki vizuri. Sikumbuki vizuri kama kilikuwa kiwanda cha bia au kitu kingine. Kwa myaka mitatu meneja mkuu wa mradi huo alikuwa akitoa taarifa za mradi kuzalisha faida.
Siku moja (baada ya taarifa za siri) Rais wa kwanza wa Musumbiji Nugu samora Machel akapeleka wakaguzi. Wakakuta kiwanda hicho kina hasara kubwa na kwa kweli kinakaribia kufirisika. Meneja Mkuu akashtakiwa kwa kufirisi kiwanda na kuliibia taifa. Meneja akashinda kesi. Rais Samora akalihutubia taifa. Akasema: "Tulimuajiri huyu kijana. Ni msomi mwenye sifa zote kuajiriwa kwa kazi hii. Kwa myaka mitatu kijana huyu amekuwa akitwambia mradi unazalisha faida. Sasa tumekwenda kumkagua na kukuta ana hasara. Tumempeleka mahakamani. Mahakama ikamuona hana hatia. Mahakama imeshindwa kuona uharibifu wa kijana huyu. Basi mfumo huu wa mahakama hautusaidii kutupeleka tunakokwenda. Nafikiria kuufutilia mbali na kuangalia namna nyingine ya kuwapatia wana-Mozambique haki zao". Inasemekana baada ya hapo serikali iliomba rufaa na kushinda. Jamaa akafungwa na kufirisiwa mali zilizokuwa zimehamishiwa mfukoni mwake na ndugu zake.

Majuzi rais Magufuli alisema kuna mawakili wanajua ukweli. Lakini wanapindisha ukweli ili wateja wao washinde kesi. Akasema mawakili kama hao wanapokwenda kuwatetea wahalifu nao wakamatwe, walale ndani. Watatokea humo kuwatetea hao wahalifu. (Nimetumia maneno yangu kumtafsiri rais Magufuli. Kama nimekosea asikasirike, sikulenga kumuudhi). Maana ya Rais Magufuli ni rahisi kuielewa. Ikitokea Wakili katika kumtetea mfalifu, mfano akajua kuwa mshtakiwa aliua, mshtakiwa huyo anayo haki ya kutetewa. Lakini wakili hastahili kuficha ukweli kuwa mshtakiwa aliua. Anachoweza kufanya katika kumtetea ni kujenga mazingira ya kwa nini aliua ili adhabu yake iwe nyepesi. Lakini wakili kupinga kuwa hakuua wakati anajua kuwa aliua ni kinyume cha sheria. Ninaamini hao ndio alisema wakamatwe.

Tanzania ni yetu wote. Namna ya kuiendesha tumepanga sisi wote kwa utaratibu tuliojiwekea. Mgawanyo wa majukumu unaeleweka. Wajibu wawananchi unajulikana. Wa Bunge pia. Wajibu wa Serikali nao. Wajibu wa mahakama unajulikana.

Tanzania kama taifa ina malengo yake. Ina namna ya kufika huko. Tanzania lazima ina matatizo ambayo inakabiliana nayo katika kutimiza malengo yake. Mfano Tanzania ina malengo ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. Ili kufika huko nchi imepanga kurfekebisha uchumi wake uwe wa viwanda. Mkulima ili apate bei nzuri mazao anayoyazalisha yauzwe baada ya kuongezwa thamani.
Matatizo ambayo nchi inakabiliana nayo na ambayo yanachelewesha safari ya kwenda huko ni Ukosefu wa uwajibikaji, rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya nakadhalika.

Inatarajiwa kuwa taasisi zitatimiza wajibu wake ili kupambana na matatizo tunayokabiliana nayo kusudi taifa litekeleza mipango yake ili litimize malengo yake. Hapo ndipo kunakuja changamoto. Ukosefu wa uwajibikaji, rushwa, ufisadi unakuwa changamoto kubwa. Majuzi watafiti walipouwawa katika vijiji vya Dodoma, wapo waliolaumu Polisi kuwa sababu ya kuuwawa watafiti hao. Wanasema wananchi walishachoka kupeleka wahalifu Polisi. Kwsa hiyo walipofikiri warafiti hao ni wahalifu hawakuwa na pa kuwapeleka kwa sababu hawana imani na Polisi. Makala hii inalenga kujadili mchango wa mahakama katika kukwamisha maendeleo yetu.
Tukitaka kujadili mahakama na mchango wake katika maendeleo ya taifa letu uwanja ni mpana. Nakumbuka utafiti Fulani ulioorodhesha mahakama kama moja ya taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Ukienda vijijini kuongea na wananchi hukosi vituko vinavyofanywa na mahakimu. Lakini hebu twende ma matamshi ya rais kuhusu Mahakama. Serikali imepeleka kesi mahakamani na kushinda kesi. Washtakiwa wanataiwa fedha Trilion tano. Mahakama inalalamika haina fedha za kuendesha shughuli zake. Ni kwa sababu haijaipelekea fedha za kutosha. Serikali imeonyesha msimamo wake wa kutatua matatizo ya wananchi. Mahakama hivyo inachelewesha kumalizia taratibu zitakazoifanya sedrikali ikusanye fedha hizo. Washtakiwa wanaendelea kufanya kazi na bila kulipa kodi.
Ninaamini hatujasahau kesi ya kashfa iliyomkabili mtanzania mmoja kwa kum tukana rais. Ilipokwenda mahakamani wqakili akaichanganya mahakama kwa kusema mshtakiwa kuandika JPM huenda hakumaanisha John Pombe Magufuli anaweza kumaanisha Juma Paulo Munuo. Mahakama bila kutafuka kama wakati mshtakiwa alipokuwa anaandika kulikuwa na JPM huyo na anahusiana namaneno hayo yaliyoandikwa mtandaoni. Kukuta mahakama inafukuza shauri kwa sababu tarehe ilikosewa ni jambo la mahakama kwenye nchi hii. Siamini kama katika sheria hairuhusiwi kutumia common cense. Swaziland iliwahi kuwa na tangazo la kuzuia ukimwi likisema "Failure to common cense try Condom Cense". Ndiyo maana na rais akatoa angalizo kuwa 'failure to common cense try lockup cense'. Ikidhihirika kuwa wakili anajua kuwa mteja wake ni mhalifu. Lakini akaonekana kutetea uhalifu anaoujua akisingizia kutojua basi msaidie kwa lockup cense. Ninadhani inasaidia. Wapo walioingia kwa mbwembwe lakini walipotoka walionekana kurekebika.
Kumekuwa na mashauri yaliyo wazi mno kiasi cha kushangaza serikali inapotangazwa kushindwa katika shauri hilo. Wakati mwingine inakuwa si kosa la mahakama. Kuna wakayti wanaoandaa kesi wanakula njama na kuipeleka mahakama kwa vifungu vya sheria ambavyo vinalenga klumsaidia mshtakiwa. Hatujasahau kesi za "Zombe". Mtu anasimama kwenye vyombo v ya habari na kusema tumeua majambazi. Inagundulika kuwa waliouwawa ni wafanyabiashara wa madini na walikuwa na mamilioni ya fedha. Fedha zao hazionekani na aliyesimama na kutangaza kuwa 'wameua majambazi' anashinda kesi. Ninajiuliza, Kama mahakama ikigundua kuwa kesi imefunguliwa vibaya haina haki ya kuwaagiza wanaoshtaki warekebishe?
Kwa ujumla ni muhimu sana kwa idara hii ya mahakama kujua kuwa inao mchango katika kutimiza malengo ya taifa. Ikijidhalilisha kwa kutokutenda haki, wananchi watafika mahala wataidharau. Watatafuta namna nyingine ya kutendeana haki. Hapo ndipo idara itaanza kujihami kama wanavyofanya Polisi: "Msichukue sheria mkononi. Wahalifu walete mbele ya sheria". Viongozi wataendelea kuanika kesi za wazi ambazo mahakamaa inacheza nazo. Hii haitaisaidia Mahakama.
Elisa Muhingo
0767 187 507

     --
 
    
 

     Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
    
 

      
 
    
 
 
   Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
    
 
 
   wanabidii+...@ googlegroups.com 
 

    Utapata Email ya
 

     kudhibitisha ukishatuma
 
    
 

      
 
    
 
 
   Disclaimer:
 
    

 
     Everyone
posting to this Forum bears
  the sole
 
    responsibility
 
     for any legal
consequences of his or
  her postings,
 
   and
 

    hence
 
     statements and facts must be
presented
  responsibly.
 

   Your
 
     continued membership signifies that
  you agree to
 
   this
 
     disclaimer and pledge to abide by
our
  Rules and
 
    Guidelines.
 
    
 
 
   ---
 
    
 
     You received this
message because you
  are subscribed
 
   to
 

    the
 
     Google Groups "Wanabidii"
  group.
 
    
 
 
   To unsubscribe from this group and
 
stop receiving
 
 
 emails
 
     from
it, send an email to wanabidii+...@
 
googlegroups.com.
 
 
  
 
     For more
options, visit
 
    https://groups.google.com/d/
  optout.
 
    
 
 

 
 
 

  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 

  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
 
kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
 
Disclaimer:
 
  Everyone
posting to this Forum bears the sole

responsibility
  for any legal consequences
of his or her postings, and
hence
  statements and facts must be presented
responsibly. Your
  continued membership
signifies that you agree to this
 
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.
 
  ---
 
 
You received this message because you are subscribed to
the
  Google Groups
"Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop
receiving emails
  from it, send an email
to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options,
visit

https://groups.google.com/d/optout.
 




--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment