Friday, 24 February 2017

Re: [wanabidii] KIFO CHA UPINZANI TANZANIA: ZAMU HII NANI MCHAWI?

Muhingo awashauri viongozi wa chama chake waruhusu upinzani ufanye kazi usife.

Ni ajabu gedere kuwa hakimu kwenye kesi ya mahindi.
 
Jovin Bifabusha
DIRECTOR KWFF LTD
P. O. Box 313
Skype: jovin.bifabusha
+255-765-010235
Karagwe,
Tanzania




On Thursday, February 23, 2017 9:32 PM, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:


Huwa nafurahi kuona ushauri kwa Chadema kutoka kwa watu wasio wa Chadema.
em

2017-02-23 5:27 GMT-05:00 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Kama kuna nchi iliwahi kunufaika na siasa za vyama vingi vya siasa, Tanzania ni moja kati ya hizo.
Nchi hii imekuwa chini ya Chama kimoja toka miaka ya 60 hadi 92 vyama vya siasa viliporuhusiwa. Chama Cha Mapinduzi, chama chenye sera nzuri kiliharibika kwa sababu ya viongozi wake kujisahau na kudhani hakuna wa kuking'oa madarakani. Ufisadi ulilelewa na kujisahau huko, Upendeleo, Rushwa, matumizi mabaya ya mali za umma na pengine kuhalalisha jinai vilijitokeza hapa nchini na viongozi wa CCM hawakuonekana kushtuka.
Watu walichoka. Watu waliamua. Bahati nzuri kikajitokeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kuonekana kuaminiwa na wananchi kiasi cha kuamua kukikabidhiwa taifa kuliongoza kupitia uchaguzi.
Huenda kiogozi wa kwanza kushtuka alikuwa Speaker wa Bunge Samwel Sitta. Katika bunge la 2007 alijaribu kubeza hoja zilizotolewaa na wabunge wa Chama hiki (CHADEMA). Hoja moja ilitolewa na Zitto Kabwe ikihusu Kashfa ya Buzwagi. Hoja ya List of shame ikitolewa na Dr. Slaa iliondolewa bungeni baada ya Sitta kuibeza. Baaada ya bunge hilo kuahirishwa wananchi walionekana wazi kuwakandia wabunge wa CCM na kuwatukuza wabunge wa Upinzani. Hapo ndipo Sitta alipoonyesha ukomavu kwa kuhakikisha wabunge wachache wa upinzani wanasikilizwa. Sikumbuki vizuri kama hakuna wabunge wa CCM waliotupiwa mayai mabovu. Watu waliamua. Wananchi walizielewa hoja za CHADEMA na wakaziona ni mtetezi wao.
Hasira za wananchi zilijionyesha uchaguzi uliofuata 2010. Idadi ya wabunge wa upinzani iliongezeka; na wanaojua siri za matokeo halali ya urais sina uhakika kama wako huru kusema ukweli na kuendelea kuwa huru.
Kipindi chote cha 2010 hadi 2015 ilidhihirika kuwa hata wahafidhina walioamini kuwa rais Tanzania lazima atoke CCM walikuwa wamepungua na kuwa rais angeweza kutoka nje ya CCM katika uchaguzi wa 2015 kwa mara ya kwanza. Chama Cha Mapinduzi kilishtuka. Yale mategemeo kuwa kila mteule wake atashinda yalitoswa na kuamua kwenda na mabadiliko. Ndiyo mabadiliko tunayoyaona sasa. Mabadiliko ambayo kutokana na udhaifu wa Rais hayajaeleweka kwa wengi (Hili nalo naliandalia makala maalum).
Toka vyama vingi vya siasa vianze hapa nchini tumeshuhudia vyama vya siasa vikiibuka na kuzama. Tunakumbuka jinsi ambavyo NCCR Mageuzi kilivyotetemesha siasa za vyama vingi 1995. Mwaka ule ilibidi kutumia nguvu ya akiba kuhakikisha CCM inashinda. Baadaye NCCR mageuzi iliyeyuka na kuishia. Kikaibuka chama cha Wananchi-CUF. Hata kama hakikufika ilipofika NCCR Mageuzi lakini inafahamika kazi yake Bungeni na mitaani. Vyama hivi kwa jinsi vilivyodhoofika, CCM haiwezi kujifanya takatifu. Kuna hisia baina ya watanzania kuwa CCM imetumia hata vyombo vya dola kudhoofisha nguvu ya vyama hivi. Nakubaliana na hisia hizo na nilipendekeza katiba mpya iliangalie hilo, (la taasisi moja kudhoofisha nyingine). Bado natafakari na sijaamini kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni njama za kupindisha agenda ya CUF kuhusu uchaguzi wa Zanzibar.
CHADEMA sasa inadhoofika. Udhaifu wake unaonekana wazi kwa wanaotaka kuuona. Kitu kimoja tunachokubaliana haraka ni hiki: CHADEMA haina inaloliongea linalohusu wananchi. Imejikita katika kutetea maslahi ya viongozi wa chama, na kujitahidi kulumbana na uongozi (serikali) uliopo kazini (madarakani). Huu ni udhaifu mkubwa sana. Lakini ni hujuma kutoka wapi? Ni CCM inaihujumu CHADEMA? Ni vizuri kutoharakisha kujibu swali hili ila kwa hoja makini.
Lakini ninataka kujielekeza mahala ninapoona CHADEMA imeanzia kuteleza. Toka 2010 mpaka muda mfupi kabla ya uchaguzi CHADEMA ilionekana kama chama chenye raslimali watu wenye uwezo wa kuliongoza taifa. Kitendo cha kujitokeza kumchukua mgombea urais kutoka nje ya Chama katika uchaguzi wa 2015; tena mgombea ambaye chama chenyewe kiliwahi kumshtaki kama mmoja wa mafisadi wakubwa. Na sababu hiyo ikawa sababu ya CCM kumuendua. Sasa CHADEMA kumchukua; ilikuwa ishara kuwa chama hicho hakikiwa na mtu aliyestahili kugombea urais. Kwa siasa za Tanzania hili ni tatizo kubwa sana. Wakati uvumi ukipita kuwa CHADEMA inaweza kumtawaza mtu nje ya wanachama wake kugombea urais tulijitahidi bila mafanikio kuzuia janga hilo. Nakumbuka kuandika mahala kuwa CHADEMA iliyoshindwa ikiwa imemsimika Dr. Slaa itakuwa imara kuliko ile itakayoshindwa ikiwa imemsimika mgombea kutoka CCM. Sijui viongozi walilewa nini? Hawakusikia.
Katika kampeni za uchaguzi, watu walikuwa wanakusanyika kusikiliza sera. CHADEMA iliyokuwa imevuma kwa kuongelea matatizo yanayogusa hisia za watu ilikosa hicho. Ikafika mahala watu wakawa wanaangalia wingi wa watu kwenye mikutano kuwa tumaini la ushindi, badala ya nini kimeongelewa kwenye mikutano hiyo. CHADEMA ikashindwa. Kulikuwa na hoja zisemazo kiongozi Fulani wa CHADEMA ameuza chama kwa shilingi bilioni kumi. Badala ya kujibu hoja zikawa zinaachwa. Hii ikakigarimu chama kushindwa na kama kawaida kuanza kelele za 'nimeibiwa'.
Baada ya uchaguzi CHADEMA tuliyoizoea hatuioni tena. Busara ya kujua watu wanataka nini na kusemea hilo haionekani tena. Mikutano ambayo baadaye ilizuiliwa wala haikulenga kuongelea wananchi wana shida gani. Bungeni mpaka linaacha kuonekana live viongozi wetu walionekana kuikandia serikali badala ya kuikosoa na kuisahoihisha. Wengine tukawa tunauliza kama kuikashfu na kuishambulia serikali ni sehemu ya kuishauri na kuisimamia? Mfano mmojawapo ni hali ya chakula nchini. CHADEMA inaona nchi itangaze janga na taifa liombe msaada wa chakula baada ya ukame wa mwaka mmoja katika sehemu za taifa. Sudan Kusini ina myaka mitatu ya ukame ndipo inatangaza janga. Tanzania inao upungufu mkubwa wa chakula. Kutokana na ukame. Mvua zinanyesha sehemu kubwa ya nchi hii. Mvua hizi zinaweza kuwa chache. Serikali imesema na inahimiza watu walime mazao ya muda mfupi. Upinzani ulikuwa na wajibu wa kuibana serikali kutoa mbegu. Hii ingeepusha taifa kukabiliwa na njaa ambayo sasa haipo. Haya. Kwa sasa viongozi Fulani wa CHADEMA wanaona fahari kukamatwa na Polisi na kuhojiwa. Matamshi yao ni wazi kuwa wana chuki binafsi na watu Fulani ndani ya serikali. Kwa herufi kubwa KAMWE HUU HAUWEZI KUWA NDIO UPINZANI.
Kama CHADEMA si mali ya mtu inatarajiwa kuwa itakaa chini na kufanya tathmini. Mwisho wake tutaona mabadiliko makubwa katika safu za uongozi wa chama hiki. Vingine basi huu ndio mwisho wake. Hivi ni CCM kweli inahihujumu? Kama jibu ni ndiyo basi ni ukaidi wa CHADEMA kukaidi ushauri wetu kutopokea wakimbizi. Nani anajua kama kati yao kuna waliotumwa kwa kazi maalum? Vinginevyo Mchawi wa zamu hii ni njaa ya viongozi wake wakuu.
Elisa Muhingo
0767 187 507
       --
   
      
   

       Send Emails to wana...@googlegroups.com
   
      
   

        
   
      
   
   
     Kujiondoa Tuma Email kwenda
   
      
   
   
     wanabidii+...@ googlegroups.com 
   

      Utapata Email ya
   

       kudhibitisha ukishatuma
   
      
   

        
   
      
   
   
     Disclaimer:
   
      

   
       Everyone
  posting to this Forum bears
    the sole
   
      responsibility
   
       for any legal
  consequences of his or
    her postings,
   
     and
   

      hence
   
       statements and facts must be
  presented
    responsibly.
   

     Your
   
       continued membership signifies that
    you agree to
   
     this
   
       disclaimer and pledge to abide by
  our
    Rules and
   
      Guidelines.
   
      
   
   
     ---
   
      
   
       You received this
  message because you
    are subscribed
   
     to
   

      the
   
       Google Groups "Wanabidii"
    group.
   
      
   
   
     To unsubscribe from this group and
   
  stop receiving
   
   
   emails
   
       from
  it, send an email to wanabidii+...@
   
  googlegroups.com.
   
   
    
   
       For more
  options, visit
   
      https://groups.google.com/d/
    optout.
   
      
   
   

   
   
   

    --
   
    Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
   
     
   

    Kujiondoa Tuma Email kwenda
   
    wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com 
   Utapata Email ya
   
  kudhibitisha ukishatuma
   
     
   
   
  Disclaimer:
   
    Everyone
  posting to this Forum bears the sole

  responsibility
    for any legal consequences
  of his or her postings, and
   hence
    statements and facts must be presented
  responsibly. Your
    continued membership
  signifies that you agree to this
   
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
    Guidelines.
   
    ---
   
   
  You received this message because you are subscribed to
   the
    Google Groups
  "Wanabidii" group.
   
    To unsubscribe from this group and stop
  receiving emails
    from it, send an email
  to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.
   
    For more options,
  visit

  https://groups.google.com/d/ optout.
   

    


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@ googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/ optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment