UB MBIONI KUANZISHA KOZI YA MAADILI
CHUO Kikuu cha Bagamoyo ( UB) , kimesema kipo mbioni kuanzisha Taasisi ya Maadili chuoni hapo .
Hayo yamesemwa Leo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu, Profesa Costa Mahalu Katika sherehe ya kukabidhi wanafunzi ambao washindi wa shindano la kuandika Insha liloandaliwa na Taasisi ya kiraia toka nchini Kenya ya Fahamu Ikishirikiana na UB Iliyofanyika Katika madarasa ya chuo hicho Kawe Beach Dar Es Salaam Leo kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho,Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Dk.Stephen Bwana.
Profesa Mahalu alisema suala la Maadili Katika Jamii ni zito na Hakuna ubishi kwamba Jamii yetu pia inakabiliwa na tatizo la mmomonyoko wa Maadili hivyo UB Imeona ni vyema siku za usoni ianzishe Taasisi ya Maadili ambayo itakuwa na masomo ambayo yatafundishwa kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhusu suala zima la Maadili kwa wasomi hao wa fani mbalimbali.
" Wakati tunaanzisha UB mwaka 2011 ,waasisi wa UB tuliona Kuwa UB iwe na somo la " Leadership and Good Governance' , kwasababu tulikuwa tunafahahamu Nchi za Afrika bado zinakabiliwa na tatizo la viongozi bora , hivyo tukaanzisha somo Hilo ambalo nilazima mwanafunzi anayesoma UB wa ngazi yoyote asome hilo somo ambalo linamsaidia mwanafunzi kutambua kiongozi mahali popote pale aweje,mambo gani afanye na yapi asifanye .
Alisema Tayari mchakato wa kuanzisha Taasisi hiyo unaendelea na upo Katika Hatua nzuri na Pindi utakapokamilika ,wataufahamisha umma na Jamii ya wasomi wa chuo hicho.
Kwa upande wake Mhadhiri wa Kozi ya 'Leadership and Good Governance ' , Dk.Asia Mwanzi alisema Lengo la mashindano hayo yaliyofadhiliwa na Taasisi ya FAHAMU ni kuwajengea wanafunzi wa chuo hicho uwezo wa kukaa chini na kuandika mambo mbalimbali yanayohusu Jamii Yao bila woga ili mamlaka husika Iweze kuyafanyiakazi mawazo Yao .
Akizungumza baada ya kukabidhiwa na Jaji Mstaafu Dk.Bwana Tuzo ,Dola Mia Moja za Kimarekani, vitabu mshindi wa kwanza ambaye ni Mwanafunzi Baraka Samuel alisema amefurahishwa na ushindi huo Kwani washiriki walikuwa ni Wengi lakini Insha yake ikaibuka Kuwa mshindi.
Baraka alisema Insha yake Ameandika kuhusu sera Taasisi ya Vyuo Vikuu ( TCU) ya kuinua viwango ya kudahili wanafunzi wanaojiunga kujiunga na Vyuo vikuu nchini ambapo ameshauri TCU na serikali kwanza iboreshe elimu za Msingi na Sekondari ikishafanikiwa Katika ngazi hizo ndiyo ije iongeze viwango Vya udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Vyuo Vikuu.
Mshindi wa pili ni Mwanafunzi wa Shahada ya pili ya Sheria ambaye pia ni Wakili wa Serikali ,Frola Massawe ambaye naye amepewa Tuzo.
Imetolewa na Ofisa Habari wa UB
happiness Katabazi
28/1/2017.
Sent from my iPad
0 comments:
Post a Comment