On Tuesday, March 13, 2012 at 8:58:39 AM UTC+3, Mohamedi Mtoi wrote:
> Fred.
> Nashukuru sana kwa ufafanuzi, lakini bado hujanipa mfano japo mmoja wa
> kuniondelea ugagaziko, Hivi kwa mfano kama nikitega Mizinga ya kufuga
> nyuki na hatimae kuanza kulina Asali siwezi kuingia kwenye kundi la
> wajasilia mali? Hapo sijaratibu njia mpya maana ufugaji wa nyuki na
> ulinaji asali hadi kuweka kwenye vifungashio bado si kitu kipya maana
> kimeshafanyika na wengine, vinginevyo dhana ya neno kipya isitumike
> kama jinsi inavyo maanisha UPYA.
>
> Vinginevyo naendelea kupata shida hapa uliposema kuwa mfanyabiashara
> hana tofauti na mchuuzi kwani nimeshuhudia watu wengi wakifanya
> biashara ndogondogo na kujiita wajasiliamali, au wakati mwingine hata
> mamlaka za serikali kuwaita wajasiliamali wadogowadogo, hii imenifanya
> nitafsiri kuwa wafanya biashara wakumbwa wakubwa wakati mwingine
> wanaweza kuitwa wajasiliamali wakubwawakubwa.
>
> Unasemaje?
>
> On 3/12/12, Fred Matola Msemwa <fredmsemwa@yahoo.com> wrote:
> > Mtoi,
> >
> > swali zuri sana,
> >
> > Mjasiriamali: ni mtu anayebuni na kuratibu njia MPYA ya kuzalisha mali au
> > utoaji huduma ili kukidhi mahitaji ya jamii kwa lengo la kupata FAIDA
> > huku akiwa tayari kwa kiasi cha hasara (calculated risk)
> > itakayojitokeza. Kuna wajasiriamali wa aina nyingi wakiwemo business
> > entrepreneurs (wajasiriamali wa biashara), wajasiriamali wa siasa
> > (political entrepreneurs), wajasiriamali katika dini (religious
> > entrepreneurs) nk.Mjasiriamali wa biashara anaweza ama kubuni na kuzimamia
> > mchakato wa
> > kuzalisha bidhaa mpya au namna bora ya utoaji huduma ili kukidhi
> > mahitaji ya jamii.
> >
> >
> > Mfanyabiashara: hana tofauti sana na mchuuzi. Huyu anaweza kutengeneza
> > bidhaa kwa
> > kukopi, kununua na baadaye kuuza bidhaa kwa faida au kutoa huduma ambayo
> > tayari ipo. Mfano ni utitiri wa maduka au
> > baa zinazotoa huduma inayofanana.
> > Baadhi ya tofauti kuu kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara ni UBUNIFU,
> > MTIZAMO JUU YA FAIDA na UTAYARI WA KIASI CHA HASARA.
> >
> > Kwa maana nyingine unaweza kusema wajasiriamali wote ni wafanya biashara
> > lakini SI WAFANYA BIASHARA WOTE NI WAJASIRIAMALI.
> >
> > Fred Msemwa
> > Book Author (Ujasiriamali na Mbinu za Biashara, 2007).
> >
> >
> >
> > ________________________________
> > From: Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>
> > To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
> > Sent: Friday, March 9, 2012 10:51 AM
> > Subject: [wanabidii] NI IPI TOFAUTI KATI YA MFANYA BIASHARA NA MJASILIAMALI?
> >
> > Wakuu.
> > Neno ujasiriamali limekuwa kwa kasi sana kiasi kwamba kwangu naona
> > limepoteza mpaka maana ya neno mfanyabiashara.
> >
> > Naomba kujuzwa, mjasiliamali ni nani na mfanya biashara ni nani.
> > Naomba maelezo ya kina na mifano ili mniondolee utata ulio nigubika.
> >
> > --
> >
> > *"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia
> > Mtema**.**
> > *
> >
> > --
> > Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> > Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> > ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> > consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> > presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> > this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> >
> > --
> > Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> > Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> >
> > Kujiondoa Tuma Email kwenda
> > wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> > ukishatuma
> >
> > Disclaimer:
> > Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> > consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> > presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> > this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> >
>
>
> --
>
> *"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema**.**
> *
Katika uchumi tunavyo vyanzo ya kiuchumi 4 ambavyo ni ardhi ,Mtaji,Wataalam,Mjasiliamali.
Hivi vanzo ndivyo tunavihitaji ili kuweza kuzalisha bidhaa na huduma katika jamii.
Vyanzo hivi ni vichache havipo kila mahali kwa lengo unalotaka kufanyia kazi kukutana na mahitaji ya jamii yasyo na kikomo (Unlimited needs and Wants).
Neno mjasiliamali kwa nchi zetu limeibuka tu kama uyoga lkn ndicho chanzo kikuu katika uchumi imara wa nchi.Wajasiliamali ndio wanaoinua nchi zao na ukikuta inchi imeendelea ni kwa sababu ya watu hawa.
Tatizo ta Ulimwengu wa nchi zinazoendelea kama sisi sio kwamba hatuna vyonzo tajwa hapo juu tunapungukiwa na wajasiliamali.
Mjasiliamali ni nani? ni mtu anayeona tatizo/uhitaji katika jamii flan akafikiri namna ya kulitatua kwa faidakutokana na kuvileta kwa pamoja vyanzo vya kiuchumi(Ardhi ,Mtaji,Wataalamu) ili kuzalisha bidhaa au huduma katika jamii husika.
Mjasiliamali huangalia fursa(uhitaji) katika jamii anafikiri namna ya kuweza kuziba huo uhitaji kwa faida.
Furaha ya mjasilia mali ni kuziba gap lililopo ktk jamii kwa kuvileta pamoja vyanzo vya kiuchumi ambavyo ni mtaji,ardhi na wataalamu.
Mfano wa Mtu kama Mengi alitazama akaona kuna fursa ktk tasinia ya habari akafikri ni kwa namna gani nitaweza kuziba hii fursa akaanzisha ITV, haikuwa ndiyo TV ya kwanza kulikuwa na TVT tayari ,tunavosema kuanzisha kitu kipya kiswahili kinaleta maana ingine, Wenzetu wanamwita (innovator, Reformer, modernizer,Visionary).
Siyo lazima ufanye kitu ambacho hakijakuwepo,angalia kuna uhitaji ?kama ndiyo,maana yake kuwepo kwako kutaleta jawabu katika jamii na kwa hiyo tasnia unayotaka kujikita utaleta mabadiliko ,utaleta unafuu kwa maisha ya watu na ladha mpya.
Bill Gate alikuwa mwanzilishi wa microsoft akafanikiwa sana kwenye mambo ya mitandao na kompyuta ,haikumzuia Steve Jobs kuja kwa tasnia ileile lkn ujio wake ulionekana na ukaleta radha nyingine katika tasinia ileile.
Huyo ndiye mjasiliamali.
Umeona kuna uhitaji wa asali kwenye jamii uhitaji huo ni upi?kwa sababu kama umeona uhitaji na wakati tayari kuna asali ingine tayari ipo sokoni ni lazima unakuja tofauti, japo katka bidhaa ileile .
Mimi nataka kufungua shule na tayari zipo zingine nakuja na kitu gani ladha gani itakayoonyesha nipo japo si kama wengine?
Tofauti na hapo cyo ujasiliamali, ni kitu ingine.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment