Sunday 22 January 2017

RE: [wanabidii] WAKUBWA KUMDHIBITI MAGUFULI: WANAANZIA PENYEWE?


Nimesoma habari zinazoonyesha kuwa viongozi wastaafu wanataka kumdhibiti Rais Magufuli kwa nia njema na kwa manufaa ya umoja wataifa letu. Habari hizo nimezisoma katika gazeti ambalo si hili ninalotumia kuandika makala haya na kwa kweli isichukuliwe kuwa woga kutolitaja. Ni nidhamu ya kawaida.
Wastaafu hao wanataka kumdhibiti Rais kutokana na kitendo chake chz kutoshiriki sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyokuwa yakiadhimishwa huko Zanzibar. Kosa jingine analolaumiwa Rais ni kule kutoa matamshi yanayohusiana na mapinduzi bila kuwa eneo zinakofanyika sherehe hizo. Wastaafu wanamlaumu kwa kwenda kinyume na 'Mila' yetu kama taifa.
Katika matamshi yake, Rais, akiwahutubia wananchi Mkoani Simiyu siku hiyo ya Mapinduzi, alisema siku hiyo ingeweza kuadhimishwa hata Tanzania bara kuhakikisha ni siku inayowagusa wananchi wa pande zote mbili za Muungano kinyume na sasa ambapo wananchi wa Zanzibar na viongfozi wote wa bara na Visiwani ndio hushiriki sherehe hizo. Anasema kuwa kama sio Mapinduzi ya wananchi wa Zanzibar kusingekuwa na Tanzania. Yaani hili taifa kubwa la mfano Africa lisingekuwepo. Sasa anataka mapinduzi iwe siku ya maana kwa wananchi wa pande zote za Muungano.
Kwa maana hiyo kwa mujibu wa viongozi hao wastaafu, heri siku hiyo iendelee kuadhimishwa Zanzibar hata kama kinyume chake watanzania wa pande zote wangeshiriki lakini isiwe hivyo na wananchi wa Zanzibar na viongozi wa pande zote ndio waendelee kushiriki siku hiyo muhimu. Hiyo ni sababu yake kutaka wananchi wa Tanganyika wanashiriki sherehe hizo. Kwa viongozi wastaafu kwo ushiriki wa wananchi wa pande zote si muhimu kama "mila iliyozoeleka".
Kuhakikisha mila hii inatunzwa, Viongozi hao wastaafu wanaona dawa ni kutunga sheria. Sheria itakayomdhibiti rais huyu na mwingine mwenye mawazo potofu kama yeye ikitokea wakawepo.
Ninafahamu kuwa sheria hiyo ikitungwa itatungwa na Bunge. Bila shaka ili kuepuka mgogoro na rais ataiwekea sahihi ili ikamilike.
Basi nataka kujua (katika mjadala huu) kama bunge litafanya hivyo kwa maslahi ya watanzania au viongozi wastaafu. Ninawatenganisha viongozi hao na wananchi na lazima kila mmoja atanielewa.
Wananchi waliliona hilo tatizo wakati wa mjadala wa katiba mpya. Wakaja na pendekezo litakaloondoa migongano katika uendeshaji wa muungano. Viongozi wastaafu wakakataa na kubadili maoni ya wananchi. Kumbe walitaka kulinda "mila" zao?
Katika sherehe zilizokuwa zikiendelea huko Zanzibar Rais wa Zanzibar alipigiwa mizinga 21 ambayo kwa kawaida ya mila za nchi zote duniani hupigiwa mkuu wa nchi. Kwa sababu Tanzania ni nchi moja iliyotokana na nchi mbili kuungana basi ni mtu mmoja anayestahili kupigiwa mizinga hiyo naye ni Rais wa jamhuri ya muungano. Hata kama haikuwa sababu ya rais Magufuli kutokwenda Zanzibar lakini si kero kuwa na watu wawili katika nchi moja wanaopokea heshima ya ukuu wa nchi?
Majuzi alipoitembelea nchi yetu waziri Mkuu wa India alipigiwa mizinga 19 kwa sababu ni mkuu wa serikali si nchi Hata akija hapa waziri mkuu wa Uingereza atapokea mizinga 19. Sio 21.
Wananchi kwa kuona utata huo katika muungano wao wakaandaa katiba yenye ufumbuzi ja janga hilo. Wakapendekeza mfumo wa nchi moja serikali tatu. Moja ikiwa inasimamiwa na mkuu wa nchi mmoja na serikali mbili zikiongozwa na uongozi usio na madaraka ya ki-nchi.
Viongozi wetu ambao wengi sasa ni wastaafu wakagoma. Wakabadilisha sheria inayoongoza utafutaji wa katibu kudhoofisha tume iliyoongoza ukusanyaji wa maoni. Moja kati ya mabadiliko ya ajabu ni kuifuta tume hiyo mara baada ya kukabidhi rasimu ya mwisho. Yaani wakawa kama mtaalamu mmoja aliyeamua kuung'oa usukani halafu akaamua kuendesha gari. Litakaloishia ndiko. Wastaafu hao wakaingia bungeni wakawa wanaulizana maswali ambayo yangejibiwa na tume waliyoivunja. Tukasema sana wakaziba masikio. Wakaleta kinachoitwa rasimu ya Sitta. Imelemaaa sidhani kama hata wao wanaielewa.
Hata kabla ya rasimu kupigiwa kura wastaafu hao ambao gazeti liliwaficha wanajitokeza kumsaidia rais anayetatizwa na mfumo huo uliolelewa na "mila' yao. Kama Magufuli hatatizwi na hilo aseme tumsikie. Hivi aende kwenye sherehe hizo. Jeshi analoliongoza limpigie mtanzania mwingine mizinga 21 anyamaze kama wengine walivyonyamaza kulinda Mila?
Akisita na akaendelea kuuheshimu uharibifu huo kwa kutoshiriki sherehe hizo azibwe midomo kutozizungumzia sherehe hizo? Hivi pendekezo lake la kulea uzalendo kwa watanzania wote kuzijali siku muhimu kama siku ya mapinduzi ni haramu kiasi hicho? Kwao tuendelee na Muungano wa viongozi?
Ninawaza mswada wa sheria ukija utafananaje? Utakusudia kutetea nini? Ninafikiri wastaafu hao wana haja ya kufikiri mara mbili kabla ya kulitumia bunge letu kurundika sheria zisizoondoa kero za msingi. Badala yake wawaache watanzania kutengeneza Katiba inayowafaa. Kama Magufuli akitaka awaongoze watanzania kuitengeneza waitakayo. Kama hataki anyamaze wataitengeneza tu. Yeye aendelee kutenda yanayowafaa watanzania. Ni mtaji tosha kwao kujitengenezea Katiba waitakayo.
Elisa Muhingo
0767 187 507

  --
 
  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
   
 
  Kujiondoa Tuma Email kwenda
 
  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
  Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma
 
   
 
  Disclaimer:
 
  Everyone posting to this Forum bears the sole
  responsibility
  for any legal consequences of his or her postings,
and
  hence
  statements and facts must be presented responsibly.
Your
  continued membership signifies that you agree to
this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.
 
  ---
 
  You received this message because you are subscribed
to
  the
  Google Groups "Wanabidii" group.
 
  To unsubscribe from this group and stop receiving
emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 
  For more options, visit
  https://groups.google.com/d/optout.
 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment