Thursday 26 January 2017

[wanabidii] Re: NEEMA NA MAJANGA YA BODABODA

Umenikumbusha mbali ndugu. Ni kipindi hicho tulikuwa tunaweka magogo kuzuia Fast Track kuelekea shirikisho la Afrika Mashariki.
Ngoja niongeze faida zaidi za biashara ya Bodaboda.
Maduka ya vipuri ni mengi sana. garage ziko za kutosha pia. mama ntilie ni wengi sana katika maeneo hayo. Hayo yote yanatokana na biashara ya boda boda.
Majanga yanayoletwq na bodaboda ni mengi. Mengi yakitokana na mifumo ya usalama. kweli waendesha bodaboda wenye liseni ni waachache.
Ukiangalia Polisi wanafanya nini Bodaboda umekuwa mti wa maembe. kazi ya polisi ni kuwakamata na kuwatia fine na kuwaachia tayuari kukamatwa wiki ijayo. Nimemuuliza mmoja kama wanakamatwa mbona hawaisji kama kila anayekamatwa pikipiki yake ingezuiliwsa mpaka apate liseni? wanakiri wanafanya kukusanya mapato. Hii si sahihi. Kazi ndogo ya kudhibiti ni kumkamata mwendesha pikipiki bila liseni akafuatwa na mwenye pikipiki. Kwa nini aajiri mtu asiye na liseni. Hii ingemaliza kwa kiasi kikubwa janga hili.
Jingine ni kufanya operation wakati wa kushughulika na pikipiki. Pikipiki zinawapita trafic barabarani wakiwa wamebeba watu watatu na wala hawashughuliki nao. Eti pikipiki zinashughulikiwa na askari fulani. Kama Pikipiki nji chombo cha moto kwa nini Trafic wasishughulike nao?
mwisho ni elimu. Enzi zetu nakumbuka kulikuwa na tuvitabu tudogo tunafundisha sheria za barabarani. <watu walizijua hata kabla ya kumaliza shule ya msingi. Tulitumia picha. Kila mmoja anakasoma.
Mimi niliipata elimu ya udreva nikisoma Sekondari uganda. Kwenye daftari nyuma kulikuwa na maelezo kwa ufupi ya sheria za barabarani. Hizi ni nyenzo zinazoweza kutumiwa kuwapa watu elimu hata kabla ya kwenda vyuo maalum.
Madereva wetu wa pikipiki na magari wanapatikana kirahisi ndiyo maana tunapata majanga ya ajali na ujinga wa sheria mkononi.
Sijui nani anayehusika anasoma haya?
Muhingo
--------------------------------------------
On Wed, 1/25/17, prudence karugendo <prudencekarugendo@yahoo.com> wrote:

Subject: NEEMA NA MAJANGA YA BODABODA
To: "Nshange Stanley (NSN - TZ/Dar es Salaam)" <stanley.nshange@nsn.com>, "Inno Kahwa" <innokahwa@yahoo.com>, "Amri Kiobya" <akiobya@yahoo.com>, "Tunk Kiobya" <tkiobya@yahoo.com>, "Herman Mushumbusi" <hkahyoza@yahoo.com>, "Emmanuelelias2005" <emmanuelelias2005@yahoo.com>, "Anthony Kahwa" <repeatitagency@yahoo.com>, "Nshange Stanley (Nokia - TZ/Dar es Salaam)" <stanley.nshange@nokia.com>, "Siyovelwa P. Hussein" <uhalisi@yahoo.co.uk>, "tundu.lissu" <tundu.lissu@gmail.com>, "Pkarugendo" <pkarugendo@yahoo.com>, "Freeman A. Mbowe" <mbowe2008@gmail.com>, "Bilhuda Mbowe" <bilhuda2006@yahoo.co.uk>, "davidkafulila@yahoo.com" <davidkafulila@yahoo.com>, "Muddy Kiobya" <muddy.kiobya@gmail.com>, "ELISA MUHINGO" <elisamuhingo@yahoo.com>, "Emmanuel Elisa" <emmanuelelisa46@yahoo.com>, "Wilfred Lwakatare" <wilfredlwakatare@gmail.com>, "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>, "akihaule@gmail.com" <akihaule@gmail.com>, "Jovi Kamuntu" <jbifabusha@yahoo.com>
Date: Wednesday, January 25, 2017, 5:34 PM



Neema
na majanga ya Bodaboda hapa
nchini

 

Na
Prudence Karugendo

 

Biashara
ya
kusafirisha watu kwa njia ya pikipiki, 
maarufu kama bodaboda, imeleta neema na majanga sawia
hapa nchini.
Biashara hiyo inaonekana kuwaneemesha wale wanaoiendesha,
 hususan
vijana ambao wanazidi kuongezeka huku
ajira kikiwa ni kitendawili kinachokosa mteguzi hata pale
inapotolewa ahera
kama mji kwa atakayekitegua.

 

Usafiri
wa
bodaboda, ukiangaliwa kwa jicho jepesi, unaonekana
ulivyoleta neema mara mbili
kwa maana ya wanaosafirishwa na wanaosafirisha.

 

Kwa
wanaosafirishwa usafiri huo ni wa haraka kwa vile unaweza
kumfikisha abiria
anakotaka kwenda bila kusubiri abiria wengine wapatikane
kama ilivyo kwa
usafiri wa mabasi na aina nyingine za usafiri ambazo si
rahisi kumsafirisha mtu
mmoja ikiwa ni lazima chombo kijae kwanza ndipo
kiondoke.

 

Kwa
maana
hiyo watu kwa sasa wana uhakika wa kusafiri kwa muda
waliojipangia kwenda
wanakokutaka na kufanya shughuli zao kisha kurudi walikotoka
bila kukwamishwa
na chochote.

 

Usafiri
wa
haraka uliozoeleka ni wa kutumia taxi ambao nauli yake sio
rafiki kwa wananchi
walio wengi, pia taxi zinashindwa kufika katika baadhi ya
sehemu kulingana na
mazingira ya sehemu nyingine  kutotoa
nafasi kwa magari hayo kuzifikia, wakati bodaboda
zikijitahidi kuyafikia kwa
wepesi.

 

Lakini
wakati limejitokeza wazo la kuanzisha biashara hiyo ya
usafiri wa bodaboda pia
kulijitokeza vigingi vingi vilivyowekwa na vyombo vya
serikali ikidaiwa kwamba
usafiri huo haufai, kwamba pikipiki hazifai kukodishwa kama
taxi. Zilitolewa sababu
mbalimbali ikiwa ni pamoja na madai ya kwamba chombo kisicho
na matairi mawili
nyuma hakipaswi kufanya biashara ya kukodishwa.

 

Lakini
watetezi wa wazo hilo la kuanzisha biashara ya bodaboda
tukiongozwa na
aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera kwa muda
mrefu, Pius
Ngeze, 
tulijifunga kibwebwe tukitumia
hoja za uhakika mpaka biashara hiyo
ikahalalishwa.

 

Pamoja
na
mambo mengine tulisema kwamba kama pikipiki imetengenezwa
kwa ajili ya usafiri
ikiwa inaruhusiwa kubeba abiria, kwa nini ionekane tofauti
linapokuja suala la
kukodishwa? Ugumu wa jibu la swali hilo ndio ukawa mwanzo wa
mamlaka husika
kulegea na kutoa ruksa kwa biashara hiyo ya
bodaboda.

 

Lakini
kutokana na biashara hiyo kuruhusiwa shingo upande
haukufanyika utaratibu
maalumu wa kuiendesha, kinachoonekana mpaka sasa ni kama
"potelea mbali
watajijua wenyewe"!

 

Baada
ya
hapo vijana wengi waliokuwa hawana ajira wakaivamia biashara
hiyo bila ukaguzi
wowote, kijana anajifunza kuendesha pikipiki siku moja na
kesho yake anakuwa
dereva wa bodaboda, akikaguliwa hana leseni na wala hajui
sheria hata moja ya
barabarani!

 

Matokeo
yake
ni ajali za kila dakika ambazo zimewageuza vijana wengi
viwete kwa kukatwa
miguu, mikono na sehemu nyingine za viungo vyao achilia
mbali vifo vingi vya
kutisha vinavyosababishwa na uzembe huo.

 

Nimesikitika
sana baada ya kufika sehemu moja Bukoba Vijijini ambayo ina
bodaboda
zisizopungua 35 na kugundua kuwa hakuna kijana yeyote kati
ya hao wanaoendesha
bodaboda anayejua leseni ni kitu gani!

 

Wao
walichojipangilia ni umoja, akitokea mmoja wao akasababisha
ajali wanamuandama
yule  aliyehusika
kwenye ajali, iwe ni
pikipiki, gari au baiskeli, wanajichukulia sheria mikononi
kwa kumuadhibu kwa
kutumia wingi wao 
bila kujali kwamba
mwenzao ndiye mwenye makosa.

 

Siku
chache
zilizopita katika maeneo ya Rwamishenye kwenye viunga vya
manispaa ya Bukoba,
dreva mmoja wa bodaboda alichomoka kama ilivyo kawaida yao,
na kujichomeka
kwenye gari dogo na kusagika mguu.

 

Aliyekuwa
anaendesha gari hilo ikabidi ajaribu kukimbia kwa usalama
wake baada ya kuona
idadi ya vijana wa bodaboda inaongezeka na kila mmoja wao
akidai mtu huyo  amemgonga
mwenzao. Vijana hao wakalikimbiza
gari hilo na kulizuia, kisha wakamtoa dreva na kuanza
kumpiga vibaya na baadaye
 wakamsukumiza
chini ya gari ili waliwashe
moto na kumuunguza.

 

Mungu
bariki
alikuwepo askari akamnusuru mtu huyo na kumpeleka kituo cha
polisi. Lakini gari
liliharibiwa vibaya sana kwa kuvunjwa vioo vyote pamoja na
kuiba kila
kilichokuwemo kwenye gari hilo ikiwa ni pamoja na simu na
pesa zote za jamaa
huyo.

 

Majanga
ninayoyaeleza katika biashara hiyo ya bodaboda ni kama hayo,
pamoja na kwamba
ajali nyingi zinazohusu bodaboda zinasababishwa na watu
wenyewe wa bodaboda
lakini wao wamejiwekea utabatiri wa kuwahukumu wale wengine
wanaohusika kwenye
ajali hizo bila kujali kuwa wenzao ndio
wanaozisababisha.

 

Majanga
ya
bodaboda yako hivi, wao wanasababisha ajali za barabarani
kutokana na kutozijua
sheria za barabarani pamoja na kutohalalishwa kuendesha
vyombo vya moto, kwa
maana ya kutokuwa na leseni, lakini wao ndio wanaogeuka watu
wa kuhukumu mahali
inapotokea ajali inayomhusu mwenzao!

 

Haiwezekani
wakawakamata waliohusika kwenye ajali na kuwapeleka
kunakohusika sababu wanajua
wazi kuwa mwenzao ndiye atakayekuwa kwenye hatia. Hivyo
hukumu wanaitoa wao
palepale hata kama mwenzao atakuwa kapoteza viungo au
maisha.

 

Kitu
ambacho
serikali ingekifanya baada ya kuzidiwa hoja kwenye usafiri
wa bodaboda
kingekuwa ni kuwasajili waendesha biashara hiyo wote na
kuwapangia maeneo
wakiwa na sare pamoja na namba za kuwatambulisha. Kabla ya
hapo wote
wangetakiwa kuwa na leseni ambazo zingekuwa zinafanyiwa
uhakiki wa mara kwa
mara.

 

Hiyo
ingefaa
kuonyesha kuwa serikali inayajali maisha ya watu wake ikiwa
imewanusuru na
majanga yaletwayo na biashara ya bodaboda. Ni kweli bodaboda
zimekuwa na neema
sanjali na baraa. Bila kuliangalia hilo kwa umakini tujue
kwamba maisha ya
wananchi wengi yamewekwa rehani.

 

prudencekarugendo@yahoo.com

0784
989 512



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment