Thursday 26 January 2017

Re: [wanabidii] Re: WAKUBWA KUMDHIBITI MAGUFULI: WANAANZIA PENYEWE?

Habari hizi ziliandikwa kwenye habari makini linalomilikiwa na kupongozwa na watu makini la Raia Mwema. Si rahisi kuwa uvumi.
--------------------------------------------
On Tue, 1/24/17, Mpita Njia <akihaule@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Re: WAKUBWA KUMDHIBITI MAGUFULI: WANAANZIA PENYEWE?
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: elisamuhingo@yahoo.com, stanley.nshange@nsn.com, innokahwa@yahoo.com, akiobya@yahoo.com, tkiobya@yahoo.com, hkahyoza@yahoo.com, emmanuelelias2005@yahoo.com, repeatitagency@yahoo.com, stanley.nshange@nokia.com, uhalisi@yahoo.co.uk, tundu.lissu@gmail.com, pkarugendo@yahoo.com, mbowe2008@gmail.com, bilhuda2006@yahoo.co.uk, davidkafulila@yahoo.com, muddy.kiobya@gmail.com, emmanuelelisa46@yahoo.com, wilfredlwakatare@gmail.com, prudencekarugendo@yahoo.com
Date: Tuesday, January 24, 2017, 1:42 AM

Kama hili
ni la kweli , basi ninadhani hawa Viongozi wastaafu
wamepungukiwa !    Wamepungukiwa fikara!  Huwezi badiri
kipengere cha katiba kwa lengo la kumdhibiti 'Joji au
Issa '! Wala huwezi tunga sheria kwa nia ya kumuadhibu
au kumdhibiti 'Alufonsi tu, au Mayasa peke
yake';

Ninadhani , kuna mambo ya msingi
wanayopaswa kuzishauri Serikali zetu mbili na sio kuingilia
maamuzi ya Marais walio madarakani!
Hili halikubaliki!


" Ukiwa kipofu Usitege Mtego wa
Panya Nyumbani mwako!"

 
On Monday,
23 January 2017 00:18:27 UTC+1, ELISA MUHINGO
wrote:

Nimesoma habari zinazoonyesha kuwa viongozi
wastaafu wanataka kumdhibiti Rais Magufuli kwa nia njema na
kwa manufaa ya umoja wataifa letu. Habari hizo nimezisoma
katika gazeti ambalo si hili ninalotumia kuandika makala
haya na kwa kweli isichukuliwe kuwa woga kutolitaja. Ni
nidhamu ya kawaida.

Wastaafu hao wanataka kumdhibiti Rais
kutokana na kitendo chake chz kutoshiriki sherehe za miaka
53 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyokuwa
yakiadhimishwa huko Zanzibar. Kosa jingine analolaumiwa Rais
ni kule kutoa matamshi yanayohusiana na mapinduzi bila kuwa
eneo zinakofanyika sherehe hizo. Wastaafu wanamlaumu kwa
kwenda kinyume na 'Mila' yetu kama taifa.

Katika matamshi yake, Rais, akiwahutubia
wananchi Mkoani Simiyu siku hiyo ya Mapinduzi, alisema siku
hiyo ingeweza kuadhimishwa hata Tanzania bara kuhakikisha ni
siku inayowagusa wananchi wa pande zote mbili za Muungano
kinyume na sasa ambapo wananchi wa Zanzibar na viongfozi
wote wa bara na Visiwani ndio hushiriki sherehe hizo.
Anasema kuwa kama sio Mapinduzi ya wananchi wa Zanzibar
kusingekuwa na Tanzania. Yaani hili taifa kubwa la mfano
Africa lisingekuwepo. Sasa anataka mapinduzi iwe siku ya
maana kwa wananchi wa pande zote za Muungano.

Kwa maana hiyo kwa mujibu wa viongozi hao
wastaafu, heri siku hiyo iendelee kuadhimishwa Zanzibar hata
kama kinyume chake watanzania wa pande zote wangeshiriki
lakini isiwe hivyo na wananchi wa Zanzibar na viongozi wa
pande zote ndio waendelee kushiriki siku hiyo muhimu. Hiyo
ni sababu yake kutaka wananchi wa Tanganyika wanashiriki
sherehe hizo. Kwa viongozi wastaafu kwo ushiriki wa wananchi
wa pande zote si muhimu kama "mila iliyozoeleka".

Kuhakikisha mila hii inatunzwa, Viongozi
hao wastaafu wanaona dawa ni kutunga sheria. Sheria
itakayomdhibiti rais huyu na mwingine mwenye mawazo potofu
kama yeye ikitokea wakawepo.

Ninafahamu kuwa sheria hiyo ikitungwa
itatungwa na Bunge. Bila shaka ili kuepuka mgogoro na rais
ataiwekea sahihi ili ikamilike.

Basi nataka kujua (katika mjadala huu) kama
bunge litafanya hivyo kwa maslahi ya watanzania au viongozi
wastaafu. Ninawatenganisha viongozi hao na wananchi na
lazima kila mmoja atanielewa.

Wananchi waliliona hilo tatizo wakati wa
mjadala wa katiba mpya. Wakaja na pendekezo litakaloondoa
migongano katika uendeshaji wa muungano. Viongozi wastaafu
wakakataa na kubadili maoni ya wananchi. Kumbe walitaka
kulinda "mila" zao?

Katika sherehe zilizokuwa zikiendelea huko
Zanzibar Rais wa Zanzibar alipigiwa mizinga 21 ambayo kwa
kawaida ya mila za nchi zote duniani hupigiwa mkuu wa nchi.
Kwa sababu Tanzania ni nchi moja iliyotokana na nchi mbili
kuungana basi ni mtu mmoja anayestahili kupigiwa mizinga
hiyo naye ni Rais wa jamhuri ya muungano. Hata kama haikuwa
sababu ya rais Magufuli kutokwenda Zanzibar lakini si kero
kuwa na watu wawili katika nchi moja wanaopokea heshima ya
ukuu wa nchi?

Majuzi alipoitembelea nchi yetu waziri Mkuu
wa India alipigiwa mizinga 19 kwa sababu ni mkuu wa serikali
si nchi Hata akija hapa waziri mkuu wa Uingereza atapokea
mizinga 19. Sio 21.

Wananchi kwa kuona utata huo katika
muungano wao wakaandaa katiba yenye ufumbuzi ja janga hilo.
Wakapendekeza mfumo wa nchi moja serikali tatu. Moja ikiwa
inasimamiwa na mkuu wa nchi mmoja na serikali mbili
zikiongozwa na uongozi usio na madaraka ya ki-nchi.

Viongozi wetu ambao wengi sasa ni wastaafu
wakagoma. Wakabadilisha sheria inayoongoza utafutaji wa
katibu kudhoofisha tume iliyoongoza ukusanyaji wa maoni.
Moja kati ya mabadiliko ya ajabu ni kuifuta tume hiyo mara
baada ya kukabidhi rasimu ya mwisho. Yaani wakawa kama
mtaalamu mmoja aliyeamua kuung'oa usukani halafu akaamua
kuendesha gari. Litakaloishia ndiko. Wastaafu hao wakaingia
bungeni wakawa wanaulizana maswali ambayo yangejibiwa na
tume waliyoivunja. Tukasema sana wakaziba masikio. Wakaleta
kinachoitwa rasimu ya Sitta. Imelemaaa sidhani kama hata wao
wanaielewa.

Hata kabla ya rasimu kupigiwa kura wastaafu
hao ambao gazeti liliwaficha wanajitokeza kumsaidia rais
anayetatizwa na mfumo huo uliolelewa na "mila' yao. Kama
Magufuli hatatizwi na hilo aseme tumsikie. Hivi aende kwenye
sherehe hizo. Jeshi analoliongoza limpigie mtanzania
mwingine mizinga 21 anyamaze kama wengine walivyonyamaza
kulinda Mila?

Akisita na akaendelea kuuheshimu uharibifu
huo kwa kutoshiriki sherehe hizo azibwe midomo
kutozizungumzia sherehe hizo? Hivi pendekezo lake la kulea
uzalendo kwa watanzania wote kuzijali siku muhimu kama siku
ya mapinduzi ni haramu kiasi hicho? Kwao tuendelee na
Muungano wa viongozi?

Ninawaza mswada wa sheria ukija
utafananaje? Utakusudia kutetea nini? Ninafikiri wastaafu
hao wana haja ya kufikiri mara mbili kabla ya kulitumia
bunge letu kurundika sheria zisizoondoa kero za msingi.
Badala yake wawaache watanzania kutengeneza Katiba
inayowafaa. Kama Magufuli akitaka awaongoze watanzania
kuitengeneza waitakayo. Kama hataki anyamaze wataitengeneza
tu. Yeye aendelee kutenda yanayowafaa watanzania. Ni mtaji
tosha kwao kujitengenezea Katiba waitakayo.

Elisa Muhingo

0767 187 507



   --

  

   Send Emails to wana...@googlegroups.com

  

    

  

   Kujiondoa Tuma Email kwenda

  

   wanabidii+...@ googlegroups.com 

  Utapata Email ya

   kudhibitisha ukishatuma

  

    

  

   Disclaimer:

  

   Everyone posting to this Forum bears
the sole

  responsibility

   for any legal consequences of his or
her postings,

 and

  hence

   statements and facts must be presented
responsibly.

 Your

   continued membership signifies that
you agree to

 this

   disclaimer and pledge to abide by our
Rules and

  Guidelines.

  

   ---

  

   You received this message because you
are subscribed

 to

  the

   Google Groups "Wanabidii"
group.

  

   To unsubscribe from this group and
stop receiving

 emails

   from it, send an email to wanabidii+...@
googlegroups.com.

  

   For more options, visit

  https://groups.google.com/d/
optout.

  





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment