Tulipopata uhuru wetu tuliainisha maadui tunaotaka kuondokana nao kuwa ni Umaskini, Ujinga na Maradhi.
Kupitia dira ya Ujamaa na Kujitegemea; NA demokrasia ya chama kimoja tulijitahidi kufikia hatua fulani na hatuwezi kuidharau. Lakini baadaye tuligeukana na kuanza kuhujumiana na vita ya maadui hao ikasimama.
Kutokana na mminyo kutoka nje mambo mawili yalitokea:
1) Tuliutelekeza ujamaa, NA
2) Tulibadilisha mfumo wa demokrasia kutoka wa chama kimoja na kuuingia huu wa vyama vingi.
Nakumbuka mminyo uliokuwepo kwa mataifa yetu kuukubali mfumo wa vyama vingi. Lengo lilikuwa kuweka ushindani ili serikali zetu ziwajibike kwa wananchi ambao ikibidi (wananchi) wabadili uongozi kupitia sanduku la kura.
Tanzania ni moja kati ya mataifa yanayonufaika/yaliyonufaika na mfumo huu. Siamini kama bila mfumo wa vyama vingi CCM ingeweza kubadilika. Wote tunakumbuka sekeseke lililokuwepo mwaka 1995 Lyatonga Murema alipohamia NCCR Mageuzi kutoka CCM. Wananchi walimshabikia Mrema kwa sababu ya kuyaelewa na kuyashughulikia matatizo ya wananchi. Naamini hatujasahau lile la 2005 Pale Mbowe alipopambana na JK. Wakati huo wananchi waliguswa na mminyo wa kiuchumi na ufisadi uliokuwa umeanzakustawi na CCM kukumbatia matajiri. Wananchi walitaka mageuzi. Ni kwa sababu walifikiri JK anaweza kuleta mageuzi kutokea CCM la sivyo 2005 Mbowe angeubeba urais. Hata 2010 licha ya kuwa JK alikuwa anagombea akiwa madarakani lakini wengi tunaamini mbinu za ''rangi fulani'' zilitumika kumzuia Dr. Slaa kwenda Ikulu 2010. Watu waliichoka CCM na hakukuwa na namna ya kuinusulu bila 'gori la kiganja'. Lakini zaidi ngoma ilinoga sana kati ya 2010 na 2015. Serikali ya CCM ilikuwa na uhakika wa kutorudi madarakani. Upinzani uliidhibiti serikali Bungeni, vyombo vya habari na mitaani. Tunakumbuka matamshi ya viongozi wa CCM kutoa matamshi ya kujiandaa kushindwa uchaguzi. Hayo yote ni matunda ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi.
Ikaja 2015. Vitu viwili viliisaidia CCM kushinda:
1) Mteule wao wa urais Dr. Magufuli) kuwa na rekodi inayomtofautisha na mwenendo wa CCM wa kukumbatia matajiri na kutelekeza matakwa na shida za wanyonge.
2) La pili. Watu waliokuwa wanatuhumiwa kuwa vinara wa ufisadi kuhamia upinzani na watarajiwa wenye sifa za uadirifu kujitoa katika vyama vya upinzani na kwa hiyo agenda iliyouinua upinzani kutelekezwa (wao wanaita kubadili gea angani). Wakati huo tayari watanzania walishasema potelea kote CCM iondoke. Ukweli bado kuna watanzania hawajaona kuwa CCM inabadilika kwa jinsi walivyoichukia. MTU YEYOTE ASIYEUPONGEZA UPINZANI KUTUFIKISHA HAPO basi ana upofu fulani na wa wazi.
Umuhimu wa demokrasia uliimbwa na kueleweka Tanzania. Kuna waliotaka kuwaaminisha waTanzania kuwa vyama vilivyopigania uhuru lazima viondoke. Kuna aloichukia CCM na wala hawajawahi kuona kuwa CCM mbovu ilihamia upinzani na kuvifanya vyama hivyo kuwa vibovu kuliko CCM na kuwa sasa CCM inabadilika.
Uchaguzi ukaja. Kwa malengo watanzania tukapiga kura. Sasa tunao viongozi. Kwa sababu za wazi CCM imeshinda. Inaongoza Bunge, na Inaongoza serikali.
CCM imeunda serikali na imempata rais ambaye anaitekeleza Ilani ya Chama ambayo ni bora na wala haikuwahi kuwa mbovu. Ubovu ulikuwa ni utekelezaji wa Ilani hiyomvipindi vilivyopita. Wapinzani waliposema Serikali sasa inatekeleza Ilani yake wala hawakusema uwongo. Haya serikali inayoyafanya upinzani uliyapigania kwa kipindi cha myaka kumi.
Kinachoshtua ni hiki: wapinzani sasa wanapinga serikali inayotekeleza waliyokuwa wanayaimba.
Watu wenye akili za kutosha wanaushangaa upinzani. Madai wanayoyadai hayaeleweki. Maadui wetu wako palepale. Ni Ujinga, Maradhi, na Umaskini. Matumizi mabaya ya raslimali yaliyosababisha serikali kutoyafanyia kazi maadui wetu yanashughulikiwa sasa. Wao wanapinga. Wanataka wakigoma kuingia bungeni; bunge lisimame liwasikilize liwabembeleze, baada ya muda warudi ndipo mambo yaende mbele. Yaani walipa kodi wagarimie kipindi hicho cha kujadiliana. Wanasimama wanataka 'kuilinda demokrasia'. Demokrasia itakayoulea umaskini, kwa kutumia posho kubwa kuwalipa bila kuingia bungeni. Yaani badala ya kutumia demokrasia kujenga uchumi wetu tutumie hata kidogo kilichopo kugarimia demokrasia. Yaani fedha za kununua madawa na madawati zitumike kulipia posho katika vikao vya kuwapatanisha wabunge wa upinzani na Naibu Speaker anayesimamia kanuni ambazo wabunge hao hawakuzoea kuzifuata. Yaani sasa agenda ya upinzani imegeuk kutoka kupinga ufisadi, rushwa na kutokusanya kodi; ikawa kutetea demokrasia. Demokrasia ambayo wao wanataka mtu anayekwepa kodi kinyume cha sheria aulizwe kuwa ''Mzee uko tayari kulipa lini kodi ya serikali'. Mtu akihisiwa ameiba; demokrasia yao asiguswe mpaka atakapodhibitika mahakamani kuwa kaiba. Uchunguzi ufanyike bila kumsimamisha. Kweli hiyo ndiyo demokrasia tuliyoilenga mwaka 1992? Hata waliotushauli tuanzishe mfumo wa vyama vingi walilenga hilo? Watu wasifanye kazi bali washiriki mikutano ya kuhoji kwa nini rais kamtimua mteule wake? Kuna watu wanajiuliza kama CCm itafanya mkutano wake wa kumkabidhi Rais mamlaka ya uenyekiti. Hivi hiyo ni agenda ya kusimamisha? Wapinzani wanatoka bungeni wakitarajia mapokezi kama waliyoyapokea 2008 baada ya Zitto kutolewa Bungeni baada ya njadala wa Buzwagi?
Elisa Muhingo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment