Thursday, 28 July 2016

[wanabidii] CHADEMA: Kwerea kwerea wa kisiasa???

Ninajua kuwa Tanzania ni nchi maskini. Kwa maneno ya kistaarabu ni nchi inayoendelea. Ni lazima tushukuru msukumo uliojitokeza myaka ya 1990 iliyoleta mageuzi ya vyama vingi. Kwa kusema waziwazi kama sio CHADEMA na vyama vingine, CCM haikuwa na mpango wa kubadilika. Ni CHADEMA iliyoitia adabu CCM mpaka (CCM) ikauvunja mtandao ulioanza kutengeneza mkakati wa uongozi kiasi cha kufikia watu kuamini kuwa 'baada ya fulani mimi ndiye nafuata kwa urais'. Jeuri ya mtu kuaga jimboni mwake kuwa ''Naacha ubunge nakwenda kuwa rais. Wewe ndiwe utakuwa mbunge baada yangu na fulani nitakupa cheo Fulani baada ya kuwa rais''. CCM ili kuepukaa kuanguka ikalazimika kuuvunja mtandao. Ni CHADEMA iliyoifanya CCM kuwarudia wanyonge. Ilishakuwa ya matajiri. Ufisadi; rushwa; uholela kwa watendaji yalielekea kuwa mila ya/utamaduni wa Tanzania. CHADEMA iliyashupalia mpaka sasa tunaona neema. Hongera CHADEMA.

Sasa baada ya CCM kuwaaminisha watanzania kuwa inabadilika, na kwa kweli ikaanza kuonyesha mabadiliko hayo, watanzania wa ngeli zote tunahitaji kuungana na kujikomboa kutoka umaskini. Tunaiona mikakati ya Serikali iliyopo madarakani. Imeanza kuyaondoa magogo yaliyoziba barabara ya maendeleo; yaani Rushwa, ufisadi nakadhalika. Tunahitaji kule mwishoni tuishinikize serikali kutuongoza kutengeneza Katiba inayotufaa kwa wakati huo angalau kwa myaka 30-50. Baada ya hapo tutakuwa tumejijenga kiuchumi na kijamii kiasi cha kutengeneza katiba nyingine kukabiliana na hali ya myaka hiyo. Ndiyo. Demokrasia inakua kadri uchumi unavyokua. Hatuwezi kutaka kuwa na demokrasia ilivyo katika nchi zilizoendelea tukiwa bado hatujaendelea.

Kitu cha kushangaza ni mwenendo wa CHADEMA wa sasa. Mtu unashindwa kuelewa. CHADEMA ya kabla ya 2015 May imekwenda wapi? Kama serikali inashughulikia ufisadi na rushwa kiasi hiki, CHADEMA inataka nini? Kama ilikuwa inatetea wanyonge, sasa wanapoanza kuhudumiwa inapinga nini? Tunajua pamoja na uchumi wetu mdogo bado tunaigarimia demokrasia. Jiji la Dar Es Salaam liliwahi kuongozwa na tume badala ya baraza la madiwani. Lilisonga mbele kiasi cha kufikiri kuwa mabaraza yote ya madiwani yavunjwe. Lakini ili kuongeza ushirikishwaji wananchi tunaendelea na mabaraza hayo. Tunagarimia demokrasia kwa kulilisha bunge. Majuzi wabunge wachache walifanya maamuzi muhimu wakati wenzao wamegoma. Hiyo ni kipimo kuwa kumbe tunaweza kupunguza ukubwa wa bunge.
CHADEMA inataka nini? Na uchumi wetu mdogo. Walitaka tusimamishe mijadala ya bunge ili kushughulikia mambo yanayoshughulikiwa na serikali. Kwa kupitia taratibu za kawaida wakakataliwa. Wakasusia Bunge. Wamekaa nje ya bunge huku wakilipwa posha na uchumi wetu wa kimaskini. Wamevumiliwa. (Najua kuwa janga Fulani likitokea, ambalo liko out of Control inaweza kusababusha kuahirishwa mijadala bungeni ili kulijadili. Sio kila kitu). Wakakwama licha ya kufanya vitimbwi mara wafunge midomo na bandage, mara wavae mavazi meusi. Wakakwama. Mwaka 2008 walipogoma bungeni kwa sababu zinazogusa maslahi ya wananchi walipotoka bungeni walipokelewa kama mashujaa. Zamu hii wamerudi kama wachezaji wa timu iliyofungwa. Wananchi wakawaangalia kama sanamu ya 'Bunena'.
Sasa ETI wanaanzisha operation UKUTA. Mtu mzima wa myaka na sifa nyingine anasimama na kuwahimiza watu wa aina zote. Wakulima, wafanyakazi, wanasiasa, waandishi wa habari, wanasheria, wavivi, wote. Waache kufanya kazi ili kuingia maandamano ya kuipinga serikali inayowaondolea vikwazo ili wajiendeleze, kupinga serikali inayopiga vita rushwa na ufisadi. Kupinga serikali inayopunguza matumizi ya kipuuzi. Kupinga serikali iliyoamua kupunguza ukubwa wake na matumizi ya anasa. Watu watoke kupinga serikali hiyo!?!
Astafurlahi!!! Sababu ya kupinga serikali hiyo: 'Inaziba demokrasia'. Yaani waliotaka serikali isifuje mali. Sasa imeamua kupunguza fujo. Eti sasa tuwaunge mkono kuilazimisha serikali ifuje mali. Tunahitaji kutumia uchumi wetu kidogo kujenga demokrasia au tunahitaji kutumia demokrasia kujenga uchumi??
Kwa kweli CHADEMA imegeuka kuwa kwerea kwerea. Makundi ya kwerea kwerea yakivamia mashamba hayaachi jani kwenye mti au mmea. Na CHADEMA wanataka kusimamisha nchi isiendelee na hawana sababu ya kitanzania. Kama makundi ya ndege wa kwerea kwerea yanamiminiwa sumu iki kuokoa janga la njaa, ipo haja ya makundi ya kwerea kwerea hawa kuwamiminia upupu. Na katika hili ni kazi ndogo. Hakuna kushughulika na mayai. Hayana hatia. Matetea tu ndiyo yashughulikiwe. Mbowe amesimama na kuagiza wote niliowataja kuandamana. Inafaa kumsaidia atangaze yeye kuwaomba wanaoandamana warudi manyumbani. Inawezekana. Magari mapya ya ''zimamoto'' kuelekeza kwake na kumuwekea kipaza saiti karibu. Atasema tu.

Elisa Muhingo
0767 187 507
 --



 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



  



 Kujiondoa Tuma Email kwenda



 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya

 kudhibitisha ukishatuma



  



 Disclaimer:



 Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility

 for any legal consequences of his or her postings, and
hence

 statements and facts must be presented responsibly.
Your

 continued membership signifies that you agree to this

 disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.



 ---



 You received this message because you are subscribed to
the

 Google Groups "Wanabidii" group.



 To unsubscribe from this group and stop receiving
emails

 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.



 For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com



Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma



Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment