Wednesday 29 April 2015

[wanabidii] Mwl hakuwahi kumkataa Lowassa tuache kutunga uongo

Mwl hakuwahi kumkataa Lowassa tuache kutunga uongo

Mimi mwaka 1997 tuliwahi kwenda na Mwl Burundi na wakati wote alipenda kuniita katika sehemu ya ndege ile iliyokuwa ikiitwa ya CCM tunakaa nae niliwahi kumuliza mawaziri wa Mkapa ambao anadhani ni wachapa kazi.

Alimtaja Lowassa hapo nakumbuka tulikuwa na walinzi wake Mlazabi na Tendewa...pia mwanzoni mwa mwaka 1999 tukiwa na Mzee Butiku na Mh Mkono wakati huo hakuwa mbunge nakumbuka alikuwa amekuja balozi mmoja
pale Butiama waliambatana na MH Kikwete

Cha kwanza alimsalimia Kikwete alisema naridhishwa na utendaji wa Edward kisha alitania tumsaidie kusomba tofari za ujenzi wa shule ya sekondari ya Chief Wanzagi wakati hakujua kama ingejengwa na Mh Mkono na kuitwa jina hilo hapo ndipo alipomtania pia Mkono kuwa uchaguzi wa mwaka 2000 ajitokeze kugombea ubunge ili aweze kumaliza ukabila na kusaidia uboreshaji wa sekta ya elimu..

Sasa uzushi unasemwa eti Mwl alimkataa Lowassa ujinga wa kupindukia,nimewataja watu hapo juu na wapo watafuteni wawape ukweli...tuache siasa za maji taka kwa kutumia vibaya jina la Mwl.Nyerere.

G.Marato wa ITV

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment