Thursday 30 April 2015

Re: [wanabidii] RE: Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

Sio kwamba wakubwa hawajui ' ila sum ya rushwa tuliyolishwa' sijui na nani ila ni kukosa uthubutu wa kusema basi,  tuanze upya! Tunahitaji 'mwendawazimu' na atakayekubali kulaumiwa na walarushwa papa na ikibidi kuwa tayari kuyatoa maisha yake kukabili rushwa Tanzania. 


Sent from Samsung Mobile


-------- Original message --------
From: "Bubelwa E. Kaiza"
Date:01/05/2015 00:02 (GMT+03:00)
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] RE: Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

Hello tujadili uchumi wa Tanzania na namna ya kuuokoa badala ya kuishia kulinganisha tu na mafanikio ya kiuchumi ya nchi nyingine. Ni vizuri wachumi wakachukua nafasi yao maana hisia na mipasho ya kisiasa haitatusaidia. Let's talk openly.

 

Kwa taarifa ya wengine, uchumi wa Kenya umejengewa katika msingi imara wa a strong manufacturing and professional services industries. Kenya ni nchi ya tatu kwa Africa kuwa na a very strong manufacturing industry baada ya Africa Kusini na Egypt. Bajeti za kila mwaka za Serikali ya Kenya hutokana na/hutegemea kodi (hasa kutoka tasnia ya usindikaji na kilimo) na other internal pubic financing strategies such as monetary instruments kwa asilimia 95. Serikali ya Kenya huachia mashirika ya nje (BWs) kuchangia asilimia 5 tu ya bajeti na hii ni baada ya BWs kuomba kuchangia bajeti ya Serikali ili wasiwe useless/irrelevant.

 

Nakumbuka wakati wa Kibaki BWs walitaka kuleta mambo ya GBS ya hapa kwetu, kujadili michango yao ya ku-finance bajeti ya Serikali hadharani, Kibaki aliwaeleza kuwa Serikali yake haijadili mambo ya budget financing hadharani, kwamba siyo utamaduni wa Kenya na iwapo BWs wangeshindwa kuvumilia utamaduni huo wa Kenya, Serikali ilikuwa radhi kutopokea hiyo asilimia 5 yao ya nyongeza katika bajeti ya Serikali ya Kenya. BWs waliufyata mpaka leo.

 

Lakini pia sekta ya fedha ya Kenya inasimamiwa vilivyo siyo holela kama hapa kwetu. Huwezi kuona wananchi waki-transact kwa kutumia dola au euro bali Ksh. Export component ya Kenya ni kubwa na nchi ina comprehensive strategy ya uchumi, mfano tujiulize kiasi cha dola kinachoingizwa nchini humo kutokana na travel service export ya KQ. Tujiulize maduka kama ya NAKUMATI, Mabenki, manunuzi yanayofanywa na Ofisi za Umoja wa Mataifa (Giligili?) na kadhalika, yanayouza bidhaa na/au huduma nje ya Kenya yanaingiza dola/euro kiasi gani nchini humo. Kenya ina mkakati mkubwa unaotekelezwa na kila Mkenya kuhakikisha uchumi wa nchi unabaki imara.

 

..... mwaka 2008 Serikali ya Zambia ilifuta mikataba (MDAs) yote ya uchimbaji madini iliyokuwepo baada ya kuona nchi yao hainufaiki na mauzo ya shaba nje ya nchi. Sheria mpya ya madini ilitungwa na kuachana na mambo ya MDAs (ushauri wa BWs). Kampuni zinazotaka kuwekeza nchini Zambia hufuata taratibu za kisheria za kupewa/kununua leseni za uchimbaji na kuingia kazini. Hakuna misamaa ya kodi wala ruzuku kwa makampuni ya wawekezaji kama Tanzania inavyofanya. Zambia inadhibiti mauzo yote ya shaba nje ya nchi. Leo hii nilipokwenda kununua ZKwacha hapa Lusaka nimekuta Kwacha 7 zinanunuliwa kwa dola 1.

 

Tunachojifunza kutoka Zambia ni kuwa Serikali ikifanya maamuzi sahihi na kuweka sera sahihi, uchumi wetu unaweza tena kurudi kwenye reli; hata shilling 5 kununua dola moja ya Marekani kama ilivyokuwa mwanzoni mwa miaka ya 1980.

 

Salam kwa MNEC Magesa.

 

Kaiza

 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment