Thursday 30 April 2015

Re: [wanabidii] OIC na AZIMIO LA ABUJA LINAPOPOTOSHWA KUENEZA CHUKI BAINA YA WATANZANIA

Dada Happines...jiulize kwa nini nchi kama morroco, tunisia, misri, iraq nk zilizokuwa za kikristo kwa sasa ni nchi za kiislam....jiulize uislam ulienezwaje katika nchi hizo na sera za waislam katika kueneza dini zikoje?.. ..jiulize what is OIC, kwa nini ilianzishwa na ajenda kuu zake ni nini?....ukipata majibu sahihi..tutajadili mantinki ya mada kwa ulinganifu sahihi...Ngupula

'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

>ambo haya magumu sana kuyaelewa na kuyajadili. Padri Mapunda amesema ambacho kinaonwa na wengi na mimi nikiwemo. Taabu sana ni jinsi ya kukisemea.
>Ukweli ni huu kwamba mambo yanayosemekana kuwemo ndani ya azimio la abuja hayawezi kutekelezwa kama ambavyo tunatekeleza ilani ya chama. Nikama yanatekelezwa kwa siri na ni rahisi kuyakana. Fadhiri hapa ndipo penye shida. Kunamambo yanaeda kichinichini na ni rahisi wanaohusika kuyakana. Tutaibukia kwenye shida kwa sababu tulikosa watu kama mapunda kuyasemea.
>Vituko vya kukuta watoto wamefungiwa wanapata mafunzo fulani huko Mosho ni utekelezaji wa azimio la Abuja.
>Sehemu mbalimbali tunaona mashule ambayo kuna tetesi kuwa usiku kunafundishwa judo nakadhalika. haijulikani kama ndio mwanzao wa kuimafrisha dola la kiislamu. Uchinjaji wa wakristo huko Libya na Syria. ni utekelezaji wa mikakati hiyo.
>Twaweza kusema tunaishi kwa kuchekeana kumbe wengine wanalo wanalolisubiri. Huenda kuyasema yakajadiliwa ndipo tunaweza kusema -ahaa hebu tujipekue.
>fadhili usikanushe kila kilichoandikwa na Padri mapunda, labda kama una siri fulani. amesema ukweli na ni vizuri tukashirikiana kurekebisha mambo.
>Niliwahi kusikia kuwa katika mkutano wa abuja Tanzania iliwakirishwa na waziri wa mambo ya nje wa wakati huo sikumbuki alikuwa nani. nakumbuka kuandika makala nikitaka serikali ikane haikuwahi kukana.
>Hatasasa haitakana.
>--------------------------------------------
>On Thu, 4/30/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:
>
> Subject: [wanabidii] OIC na AZIMIO LA ABUJA LINAPOPOTOSHWA KUENEZA CHUKI BAINA YA WATANZANIA
> To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Thursday, April 30, 2015, 4:41 PM
>
>
>
> Nikiwa 
> mpenzi wa "ukweli usiyotiliwa shaka",
> nimeshawishika katika kuonyesha upungufu yaliyomo kwenye
> makala  ya Padri Baptiste Mapunda
> iliyochapishwa
> kwenye Toleo Na. 230 la Machi 14 hadi 20, 2012, ukurasa wa
> 5, Raia Mwema (ISSN
> 1821 – 6250)  yenye kichwa,
> "TANZANIA NA
> OIC: ambapo leo hii kila mwenye ajenda ya siri na OIC
> anaitumia makala hiyo ktk
> uchambuzi wake.
>
>  
>
>  Lijue lengo
> kuu la Azimio la Abuja" kama
> ilivyoandikwa na Padri Baptiste Mapunda (wa Kanisa
> Katoliki).Padri Mapunda
> ameanza kwa utangulizi
> wenye kulielezea tamko (linaloitwa
> Abuja Declaration) na taathira ya tamko hilo kwa
>
> Tanzania! Ili kupata matini ya
> dhamira ya utangulizi wake tutazame ushahidi huu:
>
>  
>
>  "Baada ya
> kulisoma, nikaridhika na
> nikaunganisha yanayotokea katika nchi yetu ya Tanzania, juu ya harakati
> za
> wenzetu Waislamu ikiwa ni utekelezaji wa tamko hilo muhimu
> la Abuja." Bila ya
> kuonyesha harakati za Waislamu wa Tanzania na taathira ya
> moja kwa moja ya
> tamko hilo (kama limeridhiwa na Waislamu wa Tanzania au la),
> Padri Mapunda ameridhika
> na kuunganisha na kutoa hukumu ya moja kwa moja.
>
>  
>
> Hapa kuna hoja mbili muhimu ambazo
> Padri Mapunda alihitajika (kwa mujibu wa uchunguzi na
> mantiki inayoufanya
> utafiti uwe wa kisayansi). Kwanza, kwa kuwa tamko la Abuja
> (Abuja Declaration)
> lililotolewa tarehe 28, Novemba 1989
>
> nchini Nigeria limekuwapo kwa
> takriban miaka 22 sasa; na kwa kuwa (kama anavyodai Padri
> Mapunda) lengo lake
> lilikuwa kuzifuta imani nyingine zisizokuwa
>
> Uislamu;
>
>  
>
>  nadhani
> ilikuwa vema aonyeshe jinsi tamko hilo
> lilivyoathiri Ukristo katika Tanzania na au hata aonyeshe jinsi
> lilivyotafsiriwa na kufanyiwa kazi na Waislamu wa Tanzania.
> Pili, (Waislamu wa)
> Tanzania si miongoni mwa nchi zilizoshiriki na au hata
> kuridhia tamko hilo; kwa jinsi hiyo,
> Padri Mapunda alitakiwa aoneshe kisayansi jinsi tamko hilo
> lilivyowaathiri
> Waislamu wa Tanzania hata yeye (Padri Mapunda)
> kufikia hatua ya
> kuunganisha yale aliyoyaita
> matukio yanayotokea Tanzania na "tamko la
> Abuja.".
>
>  
>
> Padri Mapunda, katika kusisitiza
> dhamira ya uandishi wa makala yake, anaandika hivi:
> "Inadaiwa kwamba katika
> yote hayo lengo kuu la OIC na hasa kupitia Azimio la Abuja
> ni kuona kwamba Bara
> lote la Afrika linakuwa la Kiislamu."
>
> Nilistushwa sana na maelezo haya kwa vile
> mantiki inaonesha kwamba mwandishi (Padri Mapunda) anaandika
> hapa kwamba,
> "inasadikiwa" kana kwamba yeye aidha
>
> hajasoma malengo ya OIC au ameamua
> kwa makusudi kuwapotosha wasomaji wasielewe dhana hizi
> mbili; yaani OIC na
> tamko (Azimio) la Abuja."
>
>  
>
> Katika hali hii imenifanya kufanya
> upitizi kwa mara nyingine ili nijiridhishe juu ya malengo ya OIC; kwa ujumla,
> malengo ya OIC kwa mujibu wa Hati Idhini (OIC Charter)
> hayajabadilika tangu
> yalipoidhinishwa na wanachama wake.
>
>  
>
> Akitumia uandishi wa "ujanja wa
> mbuni kuficha kichwa mchangani ilhali mwili wake uko nje", Padri
> Mapunda
> anaandika hivi: "Huu ndio ukweli wa mambo wala si
> uchochezi wala si
> propaganda ukitaka ukweli nenda tu kwenye internet utaupata
> najisomee maandishi
> mbalimbali juu ya umoja huo wa nchi za Kiislamu, yaani
> OIC."
>
>  
>
>  Nadhani
> mwandishi huyu alijua kwamba
> alichoandika ni"uchochezi" kwa kuwa suala la Tanzania kujiunga na OIC
> limekuwa likipigwa danadana na serikali yaTanzania kwa
> shinikizo la Kanisa
> Katoliki (hili linafahamika). Na vilevile Padri Mapunda
> anafahamu kwamba
> alichoandika ni "propaganda;" yaani, uongo uliokolezwa
> chumvi nyingi dhidi ya
> OIC!Kwa kujaribu kumuweka sawa Padri Mapunda na "uchochezi" na
> "propaganda" zake naomba hapa nichore mifano michache ya
> nchi wanachama wa OIC
> na demografia yake kidini.
>
>  
>
> OIC (kwa mujibu wa takwimu za
> karibuni) ina nchi wanachama zinazokadiriwa kufikia 57 na
> miongoni mwa nchi
> hizo ni: Msumbiji (Mozambique); Togo; Lebanon; Uganda; Burkina Faso;
> Cameron; na Nigeria.
>
>  
>
> Kwa nchi zilizotajwa tujaribu
> kuangalia nchi nne (4) kwa uwiano wa kidini kwakurahisha
> ufafanuzi. Msumbiji
> ilijiunga mwaka 1994 ina Wakristo asilimia 56.1(%), Waislamu
> asilimia 17.9 (%)
> na dini nyingine asimilia 26 (%). Kwa maana hiyo Msumbiji ni
> nchi yenye
> Wakristo wengi na iliamua kujiunga na OIC, siyo?
>
>  
>
>  Togo
> ilijiunga na OIC mwaka 1997 ina dini za
> kienyeji asilimia 51 (%), Wakristo asimilia 29 (%) ilhali
> Waislamu asilimia 20
> (%). Hii ina maana kwamba, Togo si nchi ya Kiislamu lakini
> ni mwanachama wa
> OIC! Na kielelezo kingine ni Cameroniliyojiunga mwaka 1975
> ina Wakristo asilimia
> 69 (%), Waislamu asilimia 21 (%) na dini nyingine asilimia
> 10 (%). Kwa udondozi
> huu Cameron ni nchi yenye Wakristo wengi kuliko dini
> nyingine na ni mwanachama
> wa OIC.
>
>  
>
> Tumalizie kwa mfano kutoka Afrika ya
> Mashariki; Uganda ilijiunga mwaka 1974 (inawezekana hoja ikawa kwamba
> wakati huo ilikuwa ikitawaliwa na Idd Amin Dada ambaye
> alikuwa
> Muislamu) ina Wakristo asilimia 84 (%) na Waislamu wakiwa
> asilimia 12 (%).
> Uganda ni nchi yenye Wakristo wa madhehebu ya Roman Katoliki
> kama asilimia 41.9
> (%) na kwa kujiunga kwake tangu 1974 hadi leo (ni mwanachama) na hatujasikia
> nchi hiyo imekuwa ya Kiislamu kama
>
> anavyodai Padri Mapunda!
>
>
>
> Nadhani kungekuwa na hoja nyingine
> juu ya "Islamization of Africa"lakini kwa kutumia uandishi wa
> uchochezi na au propaganda zilizopitwa na wakati kwa kutumia
> ukweli "ghushi"
> unaotengenezwa na mashine za propaganda
>
> kama "The
> Ministry."
> Katika kuweka
> dhana na kuthibitisha falsafa ya
>
> uchochezi na propaganda dhidi ya
> Waislamu na Uislamu, Padri Mapunda anaandika hivi, "Sehemu ya
> madhumuni
> ya OIC, kupitia tamko la Abuja ni kufuta katika hali zote
> imani ya
> dini isiyo ya Kiislamu katika nchi wanachama.
>
>  
>
>  Na imani
> ambazo zitabidi zifutwe ni dini ya
> Kikristo, na nyinginezo ambazo hazikubaliani na imani ya
> Kiislamu." Haya ni
> madai mazito sana kuandikwa na mtu anayedhaniwa kwamba ni
> "kiongozi wa kiroho" na padri wa Kanisa
>
> Katoliki linaloamini juu ya makosa
> dhidi ya kweli kama inavyobainishwa kwenye fungu la 2475 la
> Katekisimu ya
> Kanisa Katoliki!Kwa ujumla, Uislamu unakataza kumlazimisha
> mtu yoyote kuingia
> kwenye Uislamu kwa nguvu (tazama Qur'an 2:
> 256).
>
>  
>
>  Kwa katazo
> hilo, vilevile Uislamu umeweka wazi
> juu ya dhana ya kila mtu kuwa na dini yake (tazama Qur'an
> 109: 1 – 6) kwa
> falsafa na matini ya aya hizo sidhani kama alichonukuu Padri
> Mapunda ndio
> ufafanuzi wa kweli na haki juu ya malengo ya OIC, kama
> inavyodai makala yake.
>
>  
>
> Padri Mapunda amejaribu kuonyesha
> vurugu na sintofahamu zinazotokea Nigeria na lile analoliita Azimio
> la
> Abuja! Nadhani hapa pana hoja chaparare inayohitaji (hata
> hivyo) kujibiwa; kama
> tamko la Abuja (Abuja Declaration)
>
> liliasisiwa miaka 22
> iliyopita,
>
>  
>
>  Boko Haram
> iemanzishwa na tamko hilo?Je, kwa
> kila vurugu za kidini na au sintofahamu na mauwaji ya kidini
> chanzo chake ni
> tamko la Abuja? Nadhani hii haitakuwa sahihi kwa kuwa suala
> la vurugu,
> sintofahamu, songombingo na hata
>
> mauwaji ya kidini yamekuwa yakitokea
> duniani kutokana na sababu za kibinafsi zaidi
>
> kuliko za dini yenyewe.
>
>  
>
> Tuchukuwe mfano wa vita vya kidini
> ndani ya dini moja moja na kwa madhehebu tofauti, kama
> mfano! Waislamu wa
> madhehebu ya Sunni na wa madhehebu ya Shia wamekuwa
> wakipigana na hata kuuwana
> sehemu tofauti za dunia ya Waislamu; kama wanavyouwana waamini wa
> madhehebu ya Kikristo (rejea mauwaji yaliyokuwa yakitokea
> Ireland ya Kaskazini
> kati ya Wakatoliki na Waprotestant); na hapa napo
> tusemeje?
>
>  
>
>  Cha kusikitisha sana Padri Mapunda
> anaandika kwa uangalifu mkubwa sana kwamba:
>
> "Ukichunguza kwa kina unaweza
> kubaini kwamba utekelezaji wa Azimio la Abuja unakuja
> polepole, hauna haraka.
>
>  
>
> Na ninasema wazi kwamba katika
> uchunguzi wangu nchini Tanzania, mipango hii pia imeanza
> kutekelezwa kimya
> kimya na kwa uangalifu mkubwa sana." Hapa inaonyesha
> kwamba Padri Mapunda
> amefanya utafiti wa kina na wa kutosha na anazo data (na taarifa) rasmi juu ya
> matokeo ya taathira ya lile analodai ni Azimio la
> Abuja.
>
>  
>
> Padri Mapunda, kama muamini na
> kiongozi (kwa ngazi ya upadri) anapaswa kufuata vema na kwa
> makini fungu la
> 2478 la Katekisimu ya Kanisa Katoliki
> linalotamka kwamba: Ili
> kuzuia hukumu ya haraka,
> kila mmoja awe mwangalifu kadiri inavyowezekana kutafsiri
> mawazo, maneno, na
> matendo ya jirani yake kwa namna nzuri.
>
>  
>
> Hapa naomba nieleweke kwamba jirani
> ya Wakristo katika Tanzania ni Waislamu (tunaishi ndani ya
> paa moja la Tanzania) kwa hiyo ni vema na hakitukiheshimiana
> kwa tofauti za dini zetu,
> tukipendana kama watoto wa Baba Mmoja (Adam) na tukiabudu
> kwa kila mmoja na
> dini yake ilhali wote tunamuelekea Mungu Mmoja kwa imani
> tofauti.
>
>  
>
>  Uislamu,
> kama mfumo maisha, hauwezi kumlazimisha yoyote kuingia
> kwenye dini (Qur'an
> 2: 256) na dini inayotumia
> zaidi hekima na mawaidha mema (Qur'an 16:125)
>
>  
>
>  
>
>
>
>
>
> --
>
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>  
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
> kudhibitisha ukishatuma
>
>  
>
> Disclaimer:
>
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
> for any legal consequences of his or her postings, and hence
> statements and facts must be presented responsibly. Your
> continued membership signifies that you agree to this
> disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> ---
>
> You received this message because you are subscribed to the
> Google Groups "Wanabidii" group.
>
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails
> from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>
> For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
>
>
>--
>Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>---
>You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
>To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
>For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment