Wednesday 29 April 2015

Re: [wanabidii] RE: Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

Bubelwa  

jinsi  gani  wizi  wa pesa kama escrow  unachangia  kupanda  kwa  thamani  ya dola.  Hili  naona linaingizwa  kisiasa  na  sisis  tunacopy  na kupaste.  

Hebu  fafanua  zaidi  dola  milioni  260  tu zisababishe  kushuka kwa  shilingi.

2015-04-29 22:53 GMT+03:00 Bubelwa E. Kaiza <bubelwa.kaiza@fordia.org>:

Mrema,

Umeongea kiasi fulani ila sababu za kushuka kwa Tzs. dhidi ya dola ya kimarekani ni hizi zifuatazo:-

1.  Kuvuja kwa uchumi (economc leakage)/matumizi holela ya dola kwenye mzunguko wa ndani ya nchi wa fedha. Duniani kote, kuendesha uchumi imara kunahitaji mikakati na taasisi imara za kusimamia sera, sheria na kanuni za fedha. Nchini Ufaransa, kwa mfano, hairuhusiwi kubadilisha/kununua Euro taslim zenye thamani ya zaidi ya dola 1000! Afrika ya Kusini hairuhusiwi kutumia dola/euro isipokuwa rand tu unaponunua mali au huduma yoyote (hotelini, ticket za ndage n.k). Hapa nchini kwetu hali ni shaghala baghalamamlaka zinazopaswa kusimamia uchumi wa nchi hazifanyi chochote; bureaux de change zinahamisha mauzo ya kila siku ya madukani kwenda nje ya nchi.

 

2.  Watu, hasa mafisadi, kutorosha/kuhodhi dola nje ya nchi kutokana na hofu ya uchuguzi mkuu. Hali hii inasababisha uhaba wa dola hivyo kutengeneza artificial appreciation ya dola kutokana na msingi mkuu wa uchumi wa demand vs. supply.

 

3.  Tanzania kutokuwa na dhahabu ya kuuza nje ya nchi (dhahabu inayochimbwa siyo ya kwetu bali ni ya makampuni yanayochimba (wawekezaji) na zaidi ya 90% ya mauzo ya dhahabu na madini mengine nje ya nchi hairudishwi nchini bali yanabaki huko (clauses za MDAs zinatoa fursa hizo kwa makampuniya madini) nyumbani kwao na wawekezaji. Kwa kifupi Tanzania siyo gold mining country bali ni source of gold, hivyo haimiliki madini yanayochimbwa nchini kwake bali madini husika humilikiwa na nchi mama wa makampuni ya wawekezaji.

 

4.  Kuwa na weak manufacturing, construction and professional services industries hivyo nchi kutegemea imports zaidi kuliko uwezo wa kuuza huduma na bidhaa nje ya nchi. Aidha mauzo ya mazao ya kahawa, pamba, katani na chai nje ya nchi yamepungua kufikia negligible value. Nchi isipouza bidhaa na huduma za kutosha nje ya nchi haiwezi kuwa na akiba ya kutosha ya fedha ya kigeni. Na kwa mukhtadha huu, thamani ya fedha ya nchi haiwezi kuimarishwa na pesa ya misaada au mikopo kutoka kwa wafadhali au mashirika ya Bretton Woods.

 

5.  Impact ya wizi wa pesa ya akaunti ya Tegeta Escrow (wafadhili kuzuia pesa ya misaada ya kibajeti). Zipo sababu nyingine pia zinazoathiri uchumi wa nchi (kuwa wa hovyo) kama Tanzania ambazo watu wake wengi bado hawategemei maarifa na ujuzi, bali ardhi na bidhaa, hususan kutokana na tasnia ya uziduaji.

 

Najua MNEC-CCM Magesa anatafuta hoja za ku-pacify hali mbaya inayokikabili chama chake ila ukweli ndio huo (free consultancy).

 

Kaiza      

 

 

From: wanataaluma@googlegroups.com [mailto:wanataaluma@googlegroups.com] On Behalf Of Herment Mrema
Sent: 29 April 2015 20:25
To: wanabidii@googlegroups.com; wanataaluma TPN Group
Subject: [TPN] RE: [wanabidii] Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania

 

Magesa et al

Ninavyoelewa na kama Gavana w Benki Kuu alipokwisha kuitolea maelezo kuhusu kushuka kwa thamani ya shillingi sababu kubwa ni kukua kwa uchumi wa marekani kwa kasi kubwa labda nitoe ya kuongezea.  Kwa ujumla confidence ya public kwenye hali ya uchumi wetu ni ya chini hasa kutokana na ukweli kuwa kutakuwa na change of regime.  Hata kama Chama tawala kikiwa kitaendelea kuongoza nchi lakini inaelekea kutakuwa na mabadiliko makubwa ya msingi, kisera na strategically au kimkakati.  Hiyo inafanya wafanyabiashara wengi kuoperate uchumi kwenye kiwango kidogo. Hata production kwa ajili ya kuexport imepungua labda Benk kuu watujuze hali ya exports ikoje.  Vile vile wakati dola inapanda ni kawaida kwa dhahabu kushuka bei hivyo dola tonazopata kutokana na mauzo ya dhahabu ni chache.

Kuchelewa kwa CCM kutoa mwanga ni nani anaweza kuwa Raisi kwa kipindi kijacho nayo imechangia woga wa watu kuhusu stability ya nchi hasa kwa vile kunaonekana kuna msuguano ndani ya chama au makundi ndani ya chama.  Watu wanahisi kuwa hwenda CCM ikagawanyika kutokana na makundi kitu ambacho sio chema kwa nchi kwani CCM legelege itafanya nchi kuwa legelege.

Sababu nyingine ni kuwa mauzo yetu ya nje bado sio mengi kiasi cha kupambana na dola iliyo na nguvu.  Tungekuwa na dola nyingi kwenye soko kutokana na mauzo mengi ya bidhaa, madini na mazao mengine kungefanya dola ziwe nyingi kwenye soko kuliko mahitaji ikiwa na maana kuwa bei ingeshuka

Sababu ingine ambayo ninaifikiria na kuwa licha ya kuwa uchumi wa marekani umekuwa kwa kasi na manunuzi ya mafuta bado ni ya chini kwa upande wa Marekani labda kuna watanzania wachache wanahamisha fedha kuogopa kuwa matokeo ya uchaguzi ujao unaweza ukawaathiri kibiashara au kukawa na regime change ambayo itakuwa na policy change ambayo hawana uhakika itawalinda wenye mitaji yao nchini.

Kuna sababu nyingi lakini kwa elimu yangu ndogo ya uchumi huo ni mchango wangu

Herment A. mrema


From: magesa@hotmail.com
To: wanataaluma@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania
Date: Wed, 29 Apr 2015 08:43:57 -0600

Wanataaluma,

 

Habari za siku ndugu zangu Wazalendo !

 

Nadhani kila mmoja ameona ambavyo thamani ya fedha yetu ilivyoshuka thamani katika historia ya nchi yetu tangu tupate uhuru.

 

Kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi yoyote haina maana ya kuonyesha moja kwa moja kuwa uchumi wa nchi husika umeshuka au umeathirika, hivyo basi  kushuka au kupanda kwa thamani ya fedha kuna faida na hasara kulingana na mfumo na mpangilio wa kiuchumi wa nchi husika. Ziko nchi hufaidika kwa kushusha thamani ya fedha zake makusudi kwa malengo ya kupandisha kiwango cha mauzo ya nje na kuuza zaidi.

 

Mengi yanasemwa kuhusu sababu za kushuka kwa thmani ya fedha yetu dhidi ya dola ya Marekenai sasa nikaribishe michango kama kuna mdau yoyote ndani ya jukwaa hili anaweza kutuelimisha zaidi.

 

Noamba tuchangie mada hii kwa lengo la kuelimishana sababu, faida na hasara na nini kifanyike,  labda kupitia jukwaa hili kuna mambo yanaweza yakachukuliwa na watunga sera wetu ambao baadhi yao ni wanchama wa mtandao huu ili kusaidia kujenga uchumi wetu.

 

Maana taarifa muhimu wananchi wasipoelimishwa vizuri kwa kupewa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi inaweza ikasababisha wananchi kupaniki na kuleta athari zaidi kwenye uchumi , mfano ni jinsi uchumi wa dunia ulivyoyumba miaka ya 2008/2009  sababu moja ilichangiwa na wananchi wa Marekani na Uingereza kutopata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na ikapelekea wengi wao kufanya maamuzi yasiyo sahihi ya kiuwekezaji/kifedha yaliyosababisha kuyumba kwa uchumi wote wa dunia.

 

Hivyo basi naomba nitoe wito kwa wote tuwe huru kutumia jukwaa hili na majukwaa mengine kwa lengo la kuelimishana na kupashana habari mbali mbali zilizo sahihi kwa faida yetu wote.

 

Wasalaamu.

 

Phares Magesa ,

B.Sc,PGDSE,MBA, IEng.,MIET
----------------------------

Mtaalamu na Mshauri wa TEHAMA, Menejimenti na Uongozi

 

Rais -  Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN)

www.tpntz.org

 

Cell: +255 (0784/0713/0767) 618320

 

E-mail:   magesa@tanzaniaports.com

                pmages@gmail.com

                magesa@hotmail.com


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanataaluma wa Tanzania" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanataaluma+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
XAVERY  LANGA KAPECHA NJOVU

0783 662681

" Smooth seas don't make skilful sailors. "

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment