Thursday 30 April 2015

Re: [wanabidii] OIC na AZIMIO LA ABUJA LINAPOPOTOSHWA KUENEZA CHUKI BAINA YA WATANZANIA

ambo haya magumu sana kuyaelewa na kuyajadili. Padri Mapunda amesema ambacho kinaonwa na wengi na mimi nikiwemo. Taabu sana ni jinsi ya kukisemea.
Ukweli ni huu kwamba mambo yanayosemekana kuwemo ndani ya azimio la abuja hayawezi kutekelezwa kama ambavyo tunatekeleza ilani ya chama. Nikama yanatekelezwa kwa siri na ni rahisi kuyakana. Fadhiri hapa ndipo penye shida. Kunamambo yanaeda kichinichini na ni rahisi wanaohusika kuyakana. Tutaibukia kwenye shida kwa sababu tulikosa watu kama mapunda kuyasemea.
Vituko vya kukuta watoto wamefungiwa wanapata mafunzo fulani huko Mosho ni utekelezaji wa azimio la Abuja.
Sehemu mbalimbali tunaona mashule ambayo kuna tetesi kuwa usiku kunafundishwa judo nakadhalika. haijulikani kama ndio mwanzao wa kuimafrisha dola la kiislamu. Uchinjaji wa wakristo huko Libya na Syria. ni utekelezaji wa mikakati hiyo.
Twaweza kusema tunaishi kwa kuchekeana kumbe wengine wanalo wanalolisubiri. Huenda kuyasema yakajadiliwa ndipo tunaweza kusema -ahaa hebu tujipekue.
fadhili usikanushe kila kilichoandikwa na Padri mapunda, labda kama una siri fulani. amesema ukweli na ni vizuri tukashirikiana kurekebisha mambo.
Niliwahi kusikia kuwa katika mkutano wa abuja Tanzania iliwakirishwa na waziri wa mambo ya nje wa wakati huo sikumbuki alikuwa nani. nakumbuka kuandika makala nikitaka serikali ikane haikuwahi kukana.
Hatasasa haitakana.
--------------------------------------------
On Thu, 4/30/15, fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] OIC na AZIMIO LA ABUJA LINAPOPOTOSHWA KUENEZA CHUKI BAINA YA WATANZANIA
To: "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, April 30, 2015, 4:41 PM



Nikiwa 
mpenzi wa "ukweli usiyotiliwa shaka",
nimeshawishika katika kuonyesha upungufu yaliyomo kwenye
makala  ya Padri Baptiste Mapunda
iliyochapishwa
kwenye Toleo Na. 230 la Machi 14 hadi 20, 2012, ukurasa wa
5, Raia Mwema (ISSN
1821 – 6250)  yenye kichwa,
"TANZANIA NA
OIC: ambapo leo hii kila mwenye ajenda ya siri na OIC
anaitumia makala hiyo ktk
uchambuzi wake.

 

 Lijue lengo
kuu la Azimio la Abuja" kama
ilivyoandikwa na Padri Baptiste Mapunda (wa Kanisa
Katoliki).Padri Mapunda
ameanza kwa utangulizi
wenye kulielezea tamko (linaloitwa
Abuja Declaration) na taathira ya tamko hilo kwa

Tanzania! Ili kupata matini ya
dhamira ya utangulizi wake tutazame ushahidi huu:

 

 "Baada ya
kulisoma, nikaridhika na
nikaunganisha yanayotokea katika nchi yetu ya Tanzania, juu ya harakati
za
wenzetu Waislamu ikiwa ni utekelezaji wa tamko hilo muhimu
la Abuja." Bila ya
kuonyesha harakati za Waislamu wa Tanzania na taathira ya
moja kwa moja ya
tamko hilo (kama limeridhiwa na Waislamu wa Tanzania au la),
Padri Mapunda ameridhika
na kuunganisha na kutoa hukumu ya moja kwa moja.

 

Hapa kuna hoja mbili muhimu ambazo
Padri Mapunda alihitajika (kwa mujibu wa uchunguzi na
mantiki inayoufanya
utafiti uwe wa kisayansi). Kwanza, kwa kuwa tamko la Abuja
(Abuja Declaration)
lililotolewa tarehe 28, Novemba 1989

nchini Nigeria limekuwapo kwa
takriban miaka 22 sasa; na kwa kuwa (kama anavyodai Padri
Mapunda) lengo lake
lilikuwa kuzifuta imani nyingine zisizokuwa

Uislamu;

 

 nadhani
ilikuwa vema aonyeshe jinsi tamko hilo
lilivyoathiri Ukristo katika Tanzania na au hata aonyeshe jinsi
lilivyotafsiriwa na kufanyiwa kazi na Waislamu wa Tanzania.
Pili, (Waislamu wa)
Tanzania si miongoni mwa nchi zilizoshiriki na au hata
kuridhia tamko hilo; kwa jinsi hiyo,
Padri Mapunda alitakiwa aoneshe kisayansi jinsi tamko hilo
lilivyowaathiri
Waislamu wa Tanzania hata yeye (Padri Mapunda)
kufikia hatua ya
kuunganisha yale aliyoyaita
matukio yanayotokea Tanzania na "tamko la
Abuja.".

 

Padri Mapunda, katika kusisitiza
dhamira ya uandishi wa makala yake, anaandika hivi:
"Inadaiwa kwamba katika
yote hayo lengo kuu la OIC na hasa kupitia Azimio la Abuja
ni kuona kwamba Bara
lote la Afrika linakuwa la Kiislamu."

Nilistushwa sana na maelezo haya kwa vile
mantiki inaonesha kwamba mwandishi (Padri Mapunda) anaandika
hapa kwamba,
"inasadikiwa" kana kwamba yeye aidha

hajasoma malengo ya OIC au ameamua
kwa makusudi kuwapotosha wasomaji wasielewe dhana hizi
mbili; yaani OIC na
tamko (Azimio) la Abuja."

 

Katika hali hii imenifanya kufanya
upitizi kwa mara nyingine ili nijiridhishe juu ya malengo ya OIC; kwa ujumla,
malengo ya OIC kwa mujibu wa Hati Idhini (OIC Charter)
hayajabadilika tangu
yalipoidhinishwa na wanachama wake.

 

Akitumia uandishi wa "ujanja wa
mbuni kuficha kichwa mchangani ilhali mwili wake uko nje", Padri
Mapunda
anaandika hivi: "Huu ndio ukweli wa mambo wala si
uchochezi wala si
propaganda ukitaka ukweli nenda tu kwenye internet utaupata
najisomee maandishi
mbalimbali juu ya umoja huo wa nchi za Kiislamu, yaani
OIC."

 

 Nadhani
mwandishi huyu alijua kwamba
alichoandika ni"uchochezi" kwa kuwa suala la Tanzania kujiunga na OIC
limekuwa likipigwa danadana na serikali yaTanzania kwa
shinikizo la Kanisa
Katoliki (hili linafahamika). Na vilevile Padri Mapunda
anafahamu kwamba
alichoandika ni "propaganda;" yaani, uongo uliokolezwa
chumvi nyingi dhidi ya
OIC!Kwa kujaribu kumuweka sawa Padri Mapunda na "uchochezi" na
"propaganda" zake naomba hapa nichore mifano michache ya
nchi wanachama wa OIC
na demografia yake kidini.

 

OIC (kwa mujibu wa takwimu za
karibuni) ina nchi wanachama zinazokadiriwa kufikia 57 na
miongoni mwa nchi
hizo ni: Msumbiji (Mozambique); Togo; Lebanon; Uganda; Burkina Faso;
Cameron; na Nigeria.

 

Kwa nchi zilizotajwa tujaribu
kuangalia nchi nne (4) kwa uwiano wa kidini kwakurahisha
ufafanuzi. Msumbiji
ilijiunga mwaka 1994 ina Wakristo asilimia 56.1(%), Waislamu
asilimia 17.9 (%)
na dini nyingine asimilia 26 (%). Kwa maana hiyo Msumbiji ni
nchi yenye
Wakristo wengi na iliamua kujiunga na OIC, siyo?

 

 Togo
ilijiunga na OIC mwaka 1997 ina dini za
kienyeji asilimia 51 (%), Wakristo asimilia 29 (%) ilhali
Waislamu asilimia 20
(%). Hii ina maana kwamba, Togo si nchi ya Kiislamu lakini
ni mwanachama wa
OIC! Na kielelezo kingine ni Cameroniliyojiunga mwaka 1975
ina Wakristo asilimia
69 (%), Waislamu asilimia 21 (%) na dini nyingine asilimia
10 (%). Kwa udondozi
huu Cameron ni nchi yenye Wakristo wengi kuliko dini
nyingine na ni mwanachama
wa OIC.

 

Tumalizie kwa mfano kutoka Afrika ya
Mashariki; Uganda ilijiunga mwaka 1974 (inawezekana hoja ikawa kwamba
wakati huo ilikuwa ikitawaliwa na Idd Amin Dada ambaye
alikuwa
Muislamu) ina Wakristo asilimia 84 (%) na Waislamu wakiwa
asilimia 12 (%).
Uganda ni nchi yenye Wakristo wa madhehebu ya Roman Katoliki
kama asilimia 41.9
(%) na kwa kujiunga kwake tangu 1974 hadi leo (ni mwanachama) na hatujasikia
nchi hiyo imekuwa ya Kiislamu kama

anavyodai Padri Mapunda!



Nadhani kungekuwa na hoja nyingine
juu ya "Islamization of Africa"lakini kwa kutumia uandishi wa
uchochezi na au propaganda zilizopitwa na wakati kwa kutumia
ukweli "ghushi"
unaotengenezwa na mashine za propaganda

kama "The
Ministry."
Katika kuweka
dhana na kuthibitisha falsafa ya

uchochezi na propaganda dhidi ya
Waislamu na Uislamu, Padri Mapunda anaandika hivi, "Sehemu ya
madhumuni
ya OIC, kupitia tamko la Abuja ni kufuta katika hali zote
imani ya
dini isiyo ya Kiislamu katika nchi wanachama.

 

 Na imani
ambazo zitabidi zifutwe ni dini ya
Kikristo, na nyinginezo ambazo hazikubaliani na imani ya
Kiislamu." Haya ni
madai mazito sana kuandikwa na mtu anayedhaniwa kwamba ni
"kiongozi wa kiroho" na padri wa Kanisa

Katoliki linaloamini juu ya makosa
dhidi ya kweli kama inavyobainishwa kwenye fungu la 2475 la
Katekisimu ya
Kanisa Katoliki!Kwa ujumla, Uislamu unakataza kumlazimisha
mtu yoyote kuingia
kwenye Uislamu kwa nguvu (tazama Qur'an 2:
256).

 

 Kwa katazo
hilo, vilevile Uislamu umeweka wazi
juu ya dhana ya kila mtu kuwa na dini yake (tazama Qur'an
109: 1 – 6) kwa
falsafa na matini ya aya hizo sidhani kama alichonukuu Padri
Mapunda ndio
ufafanuzi wa kweli na haki juu ya malengo ya OIC, kama
inavyodai makala yake.

 

Padri Mapunda amejaribu kuonyesha
vurugu na sintofahamu zinazotokea Nigeria na lile analoliita Azimio
la
Abuja! Nadhani hapa pana hoja chaparare inayohitaji (hata
hivyo) kujibiwa; kama
tamko la Abuja (Abuja Declaration)

liliasisiwa miaka 22
iliyopita,

 

 Boko Haram
iemanzishwa na tamko hilo?Je, kwa
kila vurugu za kidini na au sintofahamu na mauwaji ya kidini
chanzo chake ni
tamko la Abuja? Nadhani hii haitakuwa sahihi kwa kuwa suala
la vurugu,
sintofahamu, songombingo na hata

mauwaji ya kidini yamekuwa yakitokea
duniani kutokana na sababu za kibinafsi zaidi

kuliko za dini yenyewe.

 

Tuchukuwe mfano wa vita vya kidini
ndani ya dini moja moja na kwa madhehebu tofauti, kama
mfano! Waislamu wa
madhehebu ya Sunni na wa madhehebu ya Shia wamekuwa
wakipigana na hata kuuwana
sehemu tofauti za dunia ya Waislamu; kama wanavyouwana waamini wa
madhehebu ya Kikristo (rejea mauwaji yaliyokuwa yakitokea
Ireland ya Kaskazini
kati ya Wakatoliki na Waprotestant); na hapa napo
tusemeje?

 

 Cha kusikitisha sana Padri Mapunda
anaandika kwa uangalifu mkubwa sana kwamba:

"Ukichunguza kwa kina unaweza
kubaini kwamba utekelezaji wa Azimio la Abuja unakuja
polepole, hauna haraka.

 

Na ninasema wazi kwamba katika
uchunguzi wangu nchini Tanzania, mipango hii pia imeanza
kutekelezwa kimya
kimya na kwa uangalifu mkubwa sana." Hapa inaonyesha
kwamba Padri Mapunda
amefanya utafiti wa kina na wa kutosha na anazo data (na taarifa) rasmi juu ya
matokeo ya taathira ya lile analodai ni Azimio la
Abuja.

 

Padri Mapunda, kama muamini na
kiongozi (kwa ngazi ya upadri) anapaswa kufuata vema na kwa
makini fungu la
2478 la Katekisimu ya Kanisa Katoliki
linalotamka kwamba: Ili
kuzuia hukumu ya haraka,
kila mmoja awe mwangalifu kadiri inavyowezekana kutafsiri
mawazo, maneno, na
matendo ya jirani yake kwa namna nzuri.

 

Hapa naomba nieleweke kwamba jirani
ya Wakristo katika Tanzania ni Waislamu (tunaishi ndani ya
paa moja la Tanzania) kwa hiyo ni vema na hakitukiheshimiana
kwa tofauti za dini zetu,
tukipendana kama watoto wa Baba Mmoja (Adam) na tukiabudu
kwa kila mmoja na
dini yake ilhali wote tunamuelekea Mungu Mmoja kwa imani
tofauti.

 

 Uislamu,
kama mfumo maisha, hauwezi kumlazimisha yoyote kuingia
kwenye dini (Qur'an
2: 256) na dini inayotumia
zaidi hekima na mawaidha mema (Qur'an 16:125)

 

 





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment