Ndugu zangu,
Hakika, mwaka 1995 unabaki kuwa ni uliokuwa na matukio mengi makubwa; mengine ya kushangaza na hata kustaajabisha.
Na matukio makubwa kwenye siasa hutanguliwa na ishara. Kwa tuliokuwepo, tuliziona mapema ishara za mwaka huo kutawaliwa na matukio makubwa. Ikumbukwe, mwaka 1995 ndio nchi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi tangu sheria ya vyama vingi ifutwe mwaka 1964 na kurudishwa tena Julai 2, 1992.
Kwenye maktaba yangu naweza kuona, kuwa hata wakati huo, ndani ya CCM, kulikuwa na Kangi Lugora wake, wakati huo alikuwa Mbunge aliyeitwa Tuntemeke Sanga. Huyu alikuwa Mbunge machachari sana na aliyeaminika kuwa alikuwa ni msomi sana. Akiwa Dar, mara kadhaa nilimwona pale iliyokuwa Agip Hotel.
Kuelekea Bunge la Aprili 1995, Tuntemeke Sanga alijipanga kuisulubu Serikali ya Chama chake, CCM, iliyokuwa chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi. Ni kuhusu sakata la Chavda na mpango wa taifa wa ununuzi wa madeni ya taifa. Ilisemekana kulikuwa na ufisadi kwenye mradi huo. Waziri Mkuu Msuya aliahidi kulishughulikia suala hilo huku Waziri wa Fedha, Profesa Kighoma Malima akiweka wazi kuwa hakukuwa na cha fedha za umma zinazodaiwa kwa Mfanyibiashara Chavda.
Tuntemeke Sanga alitishia kuhamasisha Wabunge wenzake wapige kura ya kukosa imani kwa Serikali. Hivyo, kuangusha Serikali ya Mzee Mwinyi.
Bunge la Aprili likafanyika na Waziri Mkuu Cleopa Msuya alihimili tetemeko lile la Tuntemeke Sanga. Na hivyo, Serikali ya Mzee Mwinyi ilibaki salama.
Tumetoka Mbali.
Maggid,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment