Tuesday, 27 January 2015

Re: [wanabidii] PROF: SOSPETER MUHONGO SHUJAA WANGU SERIKALI YA AWAMU YA NNE



Ukweli huyu Profesa alinikera sana kwa tabia yake ya kutojua mambo. Aliposema  kwamba watanzania hawana mitaji ya kuingia kwenye soko la gesi kwa sababu ya mitaji hilo linaweza kuwa kweli, na pia akasema kwamba wanaweza kuwekeza kwenye miradi ya kutengeneza Juice tu, hili ndilo lililoniudhi sana pamoja na kwamba ni la kweli. Swali ni kwamba, NANI KAWFANYA WATANZANIA WAWE HIVYO?????

Kule uarabuni, kama wewe ni mgeni ukitaka kuwekeza lazima uwe na mbia ambaye ni mwarabu na umpe share, hili ni suala la policy, na wananchi wanafaidi raslimali zao bila kujali wana mitaji au elimu kiasi gani. Ni kutokana na policy kama hiyo wananchi wa huko wameweza kuwa na mitaji na kununua technologia na kuwekeza wao wenyewe bila kutegemea wageni.

Kuna siku nilimshuhudia Rais mstaafu Mkapa akimuuliza Engineer wa ujenzi kwenye daraja la Mkapa kama kuna engineer mtanzania angeweza kujenga hilo daraja na jamaa akajibu kwamba hakuna baada ya Rais kurudia mara tatu kumuuliza suali hili hilo.

Ninachotaka kuonesha hapa ni kwama Profesa amejaa kiburi, majivuno na dharau na hii ipo kwa viongozi wetu wengi, kudharau watanzania kwamba hawawezi chochote wakati wenyewe ndio walitakiwa kuweka mipango mizuri ya elimu, na uwezeshaji ili baada ya muda, watanzania hawa waweze. Badala yake viongozi haohao wanawakatisha tamaa watanzania na kuwaona kwamba kuwa si lolote si chochote!!!

Kwenye uchaguzi ujao, tuwatake Watanzania waangalie kwa umakini sera za wagombea na vyama ili wachague viongozi watakao waheshimu na kuwaendeleza na siyo hawa ambao kila kukicha ni kashfa za wizi tu.







2015-01-24 16:49 GMT+03:00 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>:

PROF: SOSPETER MUHONGO SHUJAA WANGU SERIKALI YA AWAMU YA NNE

Kama mtanzania wa kawaida nimesikitishwa na taarifa za kujiuzuru kwa Prof. Sospeter Muhongo waziri wa nishati na madini ni wazi kwamba maamuzi haya yamekuja kutokana na shinikizo la watu wanaolazimisha kusikia wanachotaka kusikia na kuukataa uhalisia. Huu ni ushindi kwa baadhi ya mabwanyenye wanaotaka kunufaika na gas kwa kigezo cha uzawa ilhali hawana sifa na uwezo wa kuwekeza, watu ambao wanamaslahi yao binafsi ila wakatumia rasilimali zao kuuaminisha umma kuwa wanapambana kwa maslahi ya Taifa.

Ni huzuni kubwa, itachukua miaka mingi sana kwa Wizara hii kupata waziri thabiti kama Prof. Muhongo, kitendo hiki kinaonesha wazi kwamba ukiwa na msimamo wa kupambana na mabepari huna nafasi katika kuiongoza Tanzania. Wasomi wanaipenda nchi yao ila wanakatishwa tamaa kwani siasa za Tanzania hazitoi fursa kwa wasomi kuzitumia taaluma zao objectively. Mabepari wanapambana kuhakikisha wazalendo wanafutika katika mfumo wa serikali.

Ili uonekane mwanasiasa bora Tanzania Muhitimu wa kidato cha nne anataka kusikia kwamba anao uwezo wa kufundisha chuo kikuu kwasababu ni mzawa. Watanzania wamezowea viongozi wanaowadanganya na kuwapa moyo hata kwenye vitu ambavyo haviwezekani.

NITAMKUMBUKA MUHONGO KWA:

1. Uwazi wake kwa Watanzania bila kujali mihemko ya walioukataa ukweli
2. Kusimamia kazi ya kusambaza umeme vijijini kwa kasi ya ajabu 
3. Kudhibiti tatizo la mgao wa umeme
4. Uwezeshaji kwa wachimbaji wadogo
5. Kuweka mbele maslahi ya Taifa dhidi ya maslahi binafsi
6. Ujasiri wa kukata mirija ya wanyonyaji wizarani bila kujali utajiri wao.
7. Kusimamia kigezo cha kuwa na mtaji kwenye mradi wa gas 
8. Ni waziri ambaye bajeti zake zilikuwa clear zimejaa miradi ya msingi na si porojo za kisiasa

Kutokuwa tayari kuwadanganya watanzania na kuwapa matumaini kwa vitu ambavyo haviwezekani, kukata mirija ya mapepari uchwara wa ndani, kuwana msimamo kwa anayoyaamini haya ndiyo yaliyomuondoa Muhongo. Watanzania tumekubali kuwapa ushindi ni watu wabadhirifu waliomuona Prof. Muhongo ni kikwazo kwao kwasababu walinyimwa vitalu vya familia kwa maslahi ya umma.

Any way Hongera kwa kazi nzuri, hongera kwa msimamo kwa tunaotambua uwezo wako tumesikitishwa na jambo hili. Hakika ulikuwa waziri wa kutiliwa mfano wewe ni shujaa uliyesimamia na kuitendea haki taaluma yako na kukataa kuburuzwa na wababaishaji.

Kwa hali hii tusitegemee wasomi wengine wa Tanzania ambao wanafanya kazi kwenye mashirika makubwa duniani kukubali kuziacha nafasi zao kwa kigezo cha uzalendo wa kuja kuisaidia nchi yao ilhali nchi inaendeshwa kutokana na mihemko na mfumo haupo tayari kuona wala kusikia uhalisia wa mambo.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment