Inahitajika ardhi yenye rutuba uliko bustani ya Eden kuweza kustawisha viongozi wa aina ile. Tunaona Kinana anavyojikumbusha enzi hizo za kuwatumikia wananchi. Tunaona wababaishaji wanavyojaribu kuudhalilisha uwezo wa uongozi wa enzi hizo za Akina msuya. Tukumbushe na jingine msuya huyu huyu akiwa fedha na Salim waziri mkuu wakihimili vishindo vya mjadala wa kuungua benki kuu. Ndugu Sitta alivyowanyanyasa kwa kuondoa shilingi. Bahati mbaya Sitta amelambishwa nini sijui
--------------------------------------------
On Tue, 1/27/15, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:
Subject: [wanabidii] Makubwa Ya 1995: Waziri Mkuu Msuya Alivyohimili Tetemeko La Tuntemeke Sanga!
To: "mabadilikotanzania" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, January 27, 2015, 9:14 AM
Ndugu
zangu,Hakika,
mwaka 1995 unabaki kuwa ni uliokuwa na matukio mengi
makubwa; mengine ya kushangaza na hata
kustaajabisha.Na matukio makubwa kwenye siasa
hutanguliwa na ishara. Kwa tuliokuwepo, tuliziona mapema
ishara za mwaka huo kutawaliwa na matukio makubwa.
Ikumbukwe, mwaka 1995 ndio nchi iliingia kwenye Uchaguzi
Mkuu wa kwanza wa vyama vingi tangu sheria ya vyama vingi
ifutwe mwaka 1964 na kurudishwa tena Julai 2, 1992.Kwenye maktaba yangu naweza kuona,
kuwa hata wakati huo, ndani ya CCM, kulikuwa na Kangi Lugora
wake, wakati huo alikuwa Mbunge aliyeitwa Tuntemeke Sanga.
Huyu alikuwa Mbunge machachari sana na aliyeaminika kuwa
alikuwa ni msomi sana. Akiwa Dar, mara kadhaa nilimwona pale
iliyokuwa Agip Hotel.Kuelekea
Bunge la Aprili 1995, Tuntemeke Sanga alijipanga kuisulubu
Serikali ya Chama chake, CCM, iliyokuwa chini ya Mzee Ali
Hassan Mwinyi. Ni kuhusu sakata la Chavda na mpango wa taifa
wa ununuzi wa madeni ya taifa. Ilisemekana kulikuwa na
ufisadi kwenye mradi huo. Waziri Mkuu Msuya aliahidi
kulishughulikia suala hilo huku Waziri wa Fedha, Profesa
Kighoma Malima akiweka wazi kuwa hakukuwa na cha fedha za
umma zinazodaiwa kwa Mfanyibiashara Chavda.Tuntemeke Sanga alitishia
kuhamasisha Wabunge wenzake wapige kura ya kukosa imani kwa
Serikali. Hivyo, kuangusha Serikali ya Mzee Mwinyi.Bunge la Aprili likafanyika na
Waziri Mkuu Cleopa Msuya alihimili tetemeko lile la
Tuntemeke Sanga. Na hivyo, Serikali ya Mzee Mwinyi ilibaki
salama.Tumetoka Mbali.Maggid,http://mjengwablog.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment