Saturday, 3 January 2015

Re: [wanabidii] HONGERA GEORGE MASAJU KUTEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU

Mi nafikiri Happy kuhusu ushauri kapewa wa kutosha labda tubadili jinsi ya kumshauri...most women sometimes they cant change unless uwabembelezee......Jamani my da Happiness, mi habari zako huwa nazipendaga sana lkn tu spelling huwa tunanikwaza kidogo tu lakini...rekebisharekebisha basi wangu...ntafurahije ukijitahidi next time...ntasoma habari yako mpk nisinzie...Ngupula.

'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Happy;
Hariri taarifa zako kabla ya kuziweka public,makosa ya kisarufi yanakupunguzia sana heshima yako ktk fani yako.
Ni jambo la msingi kulizingatia usiweke pamba masikioni,au unakuwa na haraka sana?
Kuna siku utaona umuhimu wa ushauri unaopewa lkn nakuombea usiuone usije kuuona ktk hali ya kujutia,unaweza kosa tuzo ya muhimu kwajili ya vitu vdg sana.

Reuben

Sent from Huawei Mobile

'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:






HONGERA GEORGE MASAJU KUTEULIWA KUWA MWANASHERIA MKUU
Na Happiness Katabazi

HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amemteua aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche Masaju Kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Ikulu kwa umma iliyotolewa Leo inasema Masaju  ataapishwa Jumatatu.

Hongera sana Mtani wangu Masaju kwa Kupanda Cheo. Ila Kupanda Cheo kwako huko hivi sasa kutasababisha usionekane tena Katika Mahakama za wazi za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani nchini kwaajili ya kuendesha Kesi kubwa ambazo Serikali akiwemo Mwanasheria Mkuu alikuwa akishitakiwa.

Masaju ni miongoni mwa Wanasheria wa serikali wazalendo na wanaowaaminiwa kiutendaji na ndiyo maana zilipokuwa zikifunguliwa Kesi ambazo zilikuwa zikivuta hisia za watu Wengi Masaju alikuwa akivaa suti na gauni lake la uwakili na kutinga Mahakama ya Rufaa, Mahakama Kuu na kuiendesha Kesi hiyo yeye Mwenyewe akisaidiwana na vijana wake.
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment