Monday, 1 July 2013

Re: [wanabidii] Breakingnews: Kada wa Chadema 43 wafutiwa kesi na Mahakama ya Mafinga:YALIYOJIRI

Wote huo ni woga wa sisiem kuondolewa madarakani, nafikiri kwa sasa hakuna cha kuangalia sheria wala nini bali tukio lolote linaloonekana kuwaimarisha wapinzani ni kulizuia tu bila kuangalia sheria au taratibu zinasemaje. Mzee piga piga, ua ua upo? Uelewe siyo kila unayoita amri halali au sheria ni halali, angalia sasa sheria zinavyowaumbua mchana kweupe. Nchi ingekuwa na akina hakimu Nyakunga wengi watakaoangalia sheria bila kukiogopa chama tutapiga hatua kubwa katika mambo ya kisiasa na demokrasia.

2013/7/1 mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>
 
Wasalaam,

Yaliyojiri Mahakama ya Wilaya ya Mufindi hapa Mafinga leo asubuhi:

1.   Sheria ambayo ingetumika kuzuia shughuli za kisiasa ili kupisha sensa ni Sheria ya Sensa, (The Census Act) na sio Sheria ya Vyama vya Siasa (The Political Parties Act) inayosomwa kwa pamoja na ile ya Polisi na Huduma Saidizi(The Police Force and Auxiliary Services Act), kwa maana sheria hizo mbili hazitajwi kuwa na nguvu kuliko sheria nyingine ya Bunge. Ndio maana siku hiyo hiyo, vyama vingine viliendelea kufanya shughuli zao za kisiasa, ikiwemo uzinduzi wa kampeni kule Zanzibar(Bububu)

2.    Amri ya kusitisha mkutano hutolewwa na ofisa husika aliyetoa kibali cha kufanywa huo mkutano. Kwa hyo haikuwa sahihi kwa RPC Kamuhanda kuagiza kufutwa kwa shughuli zilizokwisha pewa kibali.

3.    Amri ya kusitisha mkutano na kutaka waliokusanyika kutawanyika, inatakiwa kutoa muda ili kuwawezesha walioamriwa kuondoka kuweza kufanya hivyo, ikiwemo walio kwenye magari, kupewa muda kutawanyika, jambo ambalo katika tukio lile la tar.2/9/2012 halikufanyika.

4.  Kosa la kukusanyika bila halali haliwi kosa mpaka waliokusanyika kuataa kuondoka, hata baada ya muda wa kutosha kupita tangu walipoamiwa kuondoka. Washtakiwa 36(Red brigade) na wengine 2 (dreva na kondakta) walikamatiwa Mbeya na kuletwa kesho yake kuunganishwa kwenye kesi. Aidha, washtakiwa wengine, akiwamo Naibu Katibu Mkuu-Zanzibar, Hamad Yusuf, walinyofolewa kutoka ofisi walioizindua baada ya mlango wa kutokea kuzibwa.

5.   Aidha, kitendo cha watu kukutana ni lazima kisababishe hofu kwa watu shupavu, sio watu wowote tu, au ambao wanachukizwa na shughuli ya waliokusanyika.

Badala ya kujibu hoja zilizozaa uamuzi huu, Jamhuri waliwasilisha hati ya kuwafutia mashtaka washtakiwa watano. Upande wa utetezi ukakiri mamlaka ya DPP kufuta mashtaka, lakini ukapinga utaratibu uliotakiwa kutumika kuwa ni abuse ya discretion. Hakimu alikubali hoja hiyo ya utetezi.

Jamhuri haikujibu neno lolote kati ya hoja zilizo wasilishwa na utetezi, hivyo Hakimu Nyakunga kuamua kutupilia mbali mashtaka hayo.

Jamhuri haikusema kama itakata rufaa.

Wakatbahu,

MJL

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment