Saturday, 26 December 2015

[wanabidii] Katuni Bora Ya Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com...


Katuni ilivyotafsiriwa na mhariri wa mtandao wa mjengwablog.com..

Msanii amefanikiwa kufikisha ujumbe muhimu kuhusiana na maisha ya kisiasa. Ieleweke, kuwa maisha ya kisiasa ni magumu. Hata hivyo, kama yalivyo mengine, nayo huendelea. 
Samwel Sitta katamka kuachana na siasa na atabaki kuandika vitabu. Huko nako kuna siasa. Mzee Sitta afuate nyayo ya Mzee Msekwa na hayati Baba wa Taifa, kwa kuwataja wachache. Hawa wamekuwa wakiandika makala za magazetini, si vitabu tu. Tatizo katika nchi yetu anayeandika makala gazetini husemwa kuwa ni mwandishi wa habari!

Kuna waandishi wa habari na waandishi wa makala. Mzee Edward Lowassa yeye hajakata tamaa, na mwanasiasa hupaswi kuwa mtu wa kukata tamaa. Hata hivyo, kama Mzee Lowassa angeamua kuandika kitabu kuhusu maisha yake kisiasa, basi, naamini kingesomwa sana. Angalia katuni nyingine kwenye http://mjengwablog.com
Maggid,
Mwenyekiti/Mhariri
Mjengwablog.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment